Profesa Assad amkabidhi ofisi CAG mpya, hakuona haja ya kupiga danadana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,644
218,092
FB_IMG_1572934481783.jpg

Hiki ni kitendo kilichofanyika bila kuchelewa , hajataka kuleta longolongo ili waseme kuna mafaili yametoroshwa .

Kila la heri Profesa Assad
******

Prof. Assad:
"Hii ni taasisi na makabidhiano ya taasisi yanaenda kwa maandishi, kwa hiyo makabidhiano kwa maandishi yatafanyika Dodoma kwa sababu ndiyo kule makao makuu yetu yalipo"

"Kazi ya CAG ni kusaini ripoti lakini ripoti unachukua wajibu wa kazi ya watu wengi sana, ambao waliifanya maeneo mbalimbali hapa Tanzania, kwa hiyo nukta yangu ni kuwatazama vizuri sana watu hawa"

"Kama kuna yeyote nilimkosea kwenye utendaji wetu wa kazi basi anisamehe na mimi kuna kuna mambo alinikosea nimemsamehe."

"Baada ya hapa mimi nitafanya kazi ya kulima kwa sababu miezi 2 iliyopita nilianza kuwekeza kwenye kulima, wakinihitaji watu wa Mjini nitakuja, kuhusu changamoto ni nyingi nimepitia mnataka niseme hapa nitatia ukakasi hakuna haja ya kutia ukakasi."

"Nimepokea ofisi hii kutoka kwa Uttoh miaka mitano iliyopita naamini sikufanya uharibifu wowote mimi naamini mabadiliko yanaweza kutokea, lakini yatokee kwenye namna ilivyopangwa vizuri."


CAG Kichere :
"Kama kutakuwa na mabadiliko yatafanyika kwa umakini mkubwa ili tusiharibu mfumo wa utendaji kazi."

"Nimefanya kazi TRA najua ugumu wa kukusanya mapato, nimekuja kulinda mapato, tena nitalinda kwa wivu mkubwa sana, sitakuwa na simile kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya."

"Kama kulikuwa na mahusiano hafifu nitaimarisha mahusiano kati ya Ofisi ya CAG na Bunge."
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG apumzike aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG

Muda wake umeisha apumzike amefanya kazi yake

Aache kutumika na wanasiasa wasaliti wa nchi
 
Back
Top Bottom