Tee Bag
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 7,200
- 5,553
PROF ASSAD AMEBEBA FUNZO KWA VIONGOZI VIJANA
Na Thadei Ole Mushi
Nimesoma hii tweeter kuhusu Hawa vijana kukutana na Prof Assad aliyekuwa CAG kukutana naye kwenye daladala naona Kuna funzo kwa huyu mtu.
Vijana ambao ni Viongozi waiombe Hekima ya Mungu Sana na waishi maisha ambayo baada ya kuachia nafasi zao za uongozi wataendelea kuishi katikati ya jamii bila bodyguards wala hofu.
Huyu mzee atakuwa anaishi maisha ya furaha Sana japokuwa kwa jicho la kawaida unaweza fikiria anaishi kwa shida. Ni Viongozi wachache Sana wanaomaliza muda wao wa uongozi na kuweza kuishi kwa furaha.
Wengi huishi maisha ya wasiwasi na hofu, wengi hubakia kuhesabu maovu aliyoyafanya akiwa kiongozi matokeo yake hupatwa na magonjwa ya msongo wa mawazo matokeo yake wanakufa wakiteseka Sana.
Yuda baada ya kufanya Usaliti au Ubaya kwa Yesu alitumikia mateso, mfadhaiko Hadi akaamua kujiua. BASHIRU wa Sudani, Ben Ali wa Tunisia, Mubarak wa Misri, Gagbo wa Ivory Coast na wengineo hawakuwahi kuishi kwa amani baada ya uongozi wao.
Unafikiri katika Viongozi tulionao Sasa kwa ngazi zote Nani unafikiri anaweza kuishi maisha Kama haya baada ya kustaafu?
Ole Mushi
0712702602
Sent using Jamii Forums mobile app