KWELI Profesa Assad alisema Sitapiga kura hadi nchi hii tuanze kupiga kura kidigitali

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Ni kweli Profesa Assad alisema hatapiga kura hadi nchi hii ianze kupiga kura kidigital?

Alisema lini na akiwa wapi? Maana naona kauli hiyo tu watu wanashare ila sioni wakisema chanzo.

20240825_093824.jpg
 
Tunachokijua
Uchaguzi ni mchakato wa kidemokrasia ambapo watu hupiga kura ili kuchagua viongozi au wawakilishi wao katika ngazi au nyanja mbalimbali za serikali, kitaasisi au vikundi mbalimbali kwenye jamii. Kwa upande wa kiserikali huchagua viongozi kama vile Rais, wabunge, madiwni, wenyeviti wa mitaa, na nyinginezo. Uchaguzi unaweza pia kufanyika ili kuamua masuala muhimu ya umma, kama vile kura za maoni kuhusu sera au katiba. Kimsingi, uchaguzi ni njia ya wananchi kushiriki katika maamuzi yanayowahusu na kuhakikisha kuwa viongozi wanapatikana kwa njia ya haki na uwazi.
Zanzibar%20ballot%20box.jpg
Profesa Mussa Juma Assad ni mchumi na msomi maarufu kutoka Tanzania. Aliwahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa Tanzania kutoka mwaka 2014 hadi 2019. Katika nafasi hiyo, aliongoza juhudi za ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma na kutoa ripoti ambazo mara nyingi zilifichua matumizi mabaya ya rasilimali za umma, hivyo kuchangia katika mijadala mikubwa kuhusu uwajibikaji na utawala bora nchini Tanzania

Kumekuwepo na nukuu inayoonesha kusemwa na Profesa Asadi ikidai kuwa aliwahi kusema hatashiriki uchaguzi mpaka pale uchuguzi huo utakapoanza kufanyika kidigitali maana kwa sasa watu hushiriki uchaguzi ila hawachaguani. (Tazama hapa, hapa, hapa na hapa)

Ukweli ni upi?
Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao Jamiicheck imetafuta na kupata nukuu hiyo kuwa ni kweli Profes Mussa Assad aliwhi kuto kauli hiyo kuwa hatashiriki uchaguzi mpaka pale uchaguzi huo utakapokuwa wa kidigitali.

Kauli hiyo aliitoa 10, Aprili 2021 akiwa Muslim University Of Morogoro, akiwasilisha mada kuhusu Rushwa kwenye sekta za umma, ambapo aligusia mambo mbalimbali, baada ya kumaliza kuwasilisha akatoa wasaa wa kuulizwa maswali ndipo moja ya swali aliloulizwa lilizaa majibu ambayo ndio nukuu hii iliyoulizwa na mdau wa JamiiCheck. Tazama video, kuanzia 01:42:04 ambapo muuliza swali aliuliza naye kuanza kujibu kuanzia 1:55 hadi 1:5735.

Assad alisema amejiwekea ahadi ya kutoshiriki kupiga kur mpaka hapo mchakato wa upigaji kura utakapokuwa wa kidigitali ili akipiga kura iende kwa aliyemkusudia, aliongeza watanzania huwa wanapiga kura lakini hawashiriki Uchaguzi.

1724849113121-png.3081438

Attachments

  • 1724849113121.png
    1724849113121.png
    885 KB · Views: 11
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom