Profesa Assad afuate nyayo za Prof. Safari kuliko kuumia na kinyongo

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Saikolojia unasema "ukiona mtu anazungumzia jambo lililomponyoka mara kwa mara ujue bado analitamani" kwa mfano mtu kaachwa lakini kuwa kucha badala ya kufanya kazi nyingine anafatilia maisha ya mtu aliyemwacha ujue suala limemuuma.

Profesa Mussa Assad alipoondolewa "u-CAG" alifungasha na akaondoka kuendelea na shughuli zake mara hii akitumia gari aina ya IST akiwa tofauti na Assad niliyemjua UDSM akitumia Benz jekundu na Nisssan Patrol rangi ya jeshi.

Baada ya "u-CAG" alifanya mihadhara kadhaa ya kitaaluma iliyoandaliwa na taasisi za kiislam na baadaye kuteuliwa kuwa VC wa chuo kikuu cha kiislam.

Kwa vijana msiomjua Prof.Safari si mwanasheria tu bali ni mwanadiplomasia aliyekuwa Mkuu wa chuo cha diplomasia,Kurasini. Alipoondolewa wadhifa wake alijiunga na chama cha CUF na baadaye CHADEMA ambapo alistaafia siasa.

Prof. Assad ana mengi namshauri kuliko kubaki na kinyongo apande jukwaani atoe hoja zake la sivyo anaonesha umma kuwa yeye ni "coward" anazungumza na kumsengenya mtu asiyeweza kumjibu.
 
Mwache aseme kuna wengi hawajui "vituko " vya MwendaKuzimu, na kupitia hivyo inawafunza vijana kuukataa utawala wa Kiimla.

Kuhusu Pro Safari kutoka kwake CUF na Chadema hakukuwa kimya kimya alitumia muda kuwasema hovyo hovyo Maalim Seif na Mbowe baada ya kushindwa kupata uenyekiti wa vyama hivyo
Kwa taarifa yako alitomboka Sana jinsi alivyo msaidia Lipumba hadi akafukuzwa kazi UDSM
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚mwenyewe namshangaa mzee wetu Jafari
Jafari anazingua sana bana now naanza kumuona kama nae ni mlemavu wa akili tofauti na sifa alizojinyakulia awali kuwa ni mjasiri!

Si alisema anakwenda kulima kwa mbwembwe zote au na huko shambani wamempiga spana. Maana CCM wakikuamulia lazma uombe poo!
 
Jafari anazingua sana bana now naanza kumuona kama nae ni mlemavu wa akili tofauti na sifa alizojinyakulia awali kuwa ni mjasiri!

Si alisema anakwenda kulima kwa mbwembwe zote au na huko shambani wamempiga spana. Maana CCM wakikuamulia lazma uombe poo!
πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom