Wakati akiweka jiwe la msingi miradi ya ujenzi wa nyumba za shirika la nyumba la Taifa Prof. Anna Tibaijuka amesema wameiomba serikali ipunguze kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili shirika hilo liweze kujenga nyumba za garama nafuu kwa watanzania. Hoja hii kwa mara ya kwanza ilitolewa na Dr. Slaa kama moja ya ahadi zake wakati anaomba urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kama hili jambo ni jema kwa namna hii kwanini serikali iendelee kuona kigugumizi kwa sababu tu ya kuogopa watakuwa wanatekeleza ahadi za Dr. Slaa. Na kama ni punguzo la kodi kwenye vifaa vya ujenzi iwe kwa watu wote na siyo kwa NHC ili kila anayetaka kujenga afaidike na hilo punguzo.
Hakuna sababu ya punguzo la kodi kwenye vifaa vya ujenzi kushindikana kwa sababu kuna maeneo chungu nzima tunatoa misamaha ya kodi ambayo hayana maslahi kwa mtanzania. Na kwa jambo kama hili ndio dhana nzima ya maisha bora kwa kila mtanzania itatekelezeka kwa vitendo na siyo nadharia kama ilivyo sasa. Kama mtu alikuwa anaishi kwenye nyumba ya tembe akienda kwenye nyumba ya bati na tofali za udongo walau unaweza sema ndiyo maisha bora.