Prof. Waziri Anna Tibaijuka anafanyia kazi ahadi ya Dr. Slaa ya punguzo la kodi vifaa vya ujenzi

critical

Member
Apr 4, 2012
17
0
Wakati akiweka jiwe la msingi miradi ya ujenzi wa nyumba za shirika la nyumba la Taifa Prof. Anna Tibaijuka amesema wameiomba serikali ipunguze kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili shirika hilo liweze kujenga nyumba za garama nafuu kwa watanzania. Hoja hii kwa mara ya kwanza ilitolewa na Dr. Slaa kama moja ya ahadi zake wakati anaomba urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kama hili jambo ni jema kwa namna hii kwanini serikali iendelee kuona kigugumizi kwa sababu tu ya kuogopa watakuwa wanatekeleza ahadi za Dr. Slaa. Na kama ni punguzo la kodi kwenye vifaa vya ujenzi iwe kwa watu wote na siyo kwa NHC ili kila anayetaka kujenga afaidike na hilo punguzo.

Hakuna sababu ya punguzo la kodi kwenye vifaa vya ujenzi kushindikana kwa sababu kuna maeneo chungu nzima tunatoa misamaha ya kodi ambayo hayana maslahi kwa mtanzania. Na kwa jambo kama hili ndio dhana nzima ya maisha bora kwa kila mtanzania itatekelezeka kwa vitendo na siyo nadharia kama ilivyo sasa. Kama mtu alikuwa anaishi kwenye nyumba ya tembe akienda kwenye nyumba ya bati na tofali za udongo walau unaweza sema ndiyo maisha bora.
 

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
1,195
Uzuri wa chama ambacho ni well focused... Chadema ikiongea leo CCM wanakuja kutambua baada ya miaka3...
Dr.Slaa rais wetu wa moyoni endelea kuinyoosha nchi! mwisho wa siku CCM wataelewa tu... maana UMMA ulishakufaham... Keep it up.

Mawaziri endeleeni kudesa kutoka kwa Kichwa Dr, huyoo msanii mpuuzeni ili 2015 mrudi majimboni...
 

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
966
250
unajua serikali hii ya sasa haiwezi kujishughulisha kutatua kero za wananchi kwa kuwa walioiweka madarakani ni mafisadi.Wao wananufaika na hiyo kodi so hawawezi kuondoa ama kupunguza kwa kuwa kwa jicho la pili wataona kama wanawajenga wapinzani.Tumekuwa na viongozi wa hovyo sana nchi hii kiasi hawajali matatizo ya wananchi!
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,032
2,000
simenti itakua 5000? Bati je,misumari, bila kusaha rangi..tunataka vitendo sio siasa.!
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,892
2,000
Kwa hiyo ulitakaje, watu waishi maalisha magumu kwa kuogopa kuiga au kuchukua vilivyosemwa na Dr. Slaa? Huo ni upofu wa kisiasa eti watu waishi maisha magumu hadi pale CHADEMA itapochukua nchi. Acha ushabiki pongeza kila hatua itayopunguza ukali wa maisha iwe imefanywa na CDM au chama chochote.
 

Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Nov 3, 2012
139
0
Tunachohitaji ni unafuu wa maisha bila kujali ni nani kasema au ka-copy wapi maadamu ni kitu chenye maslahi na wananchi.BIG UP MAMA.

kweli mkuu,ccm wangekuwa wanatekeleza tunayotaka yafanyike wangeendelea kuongoza hii nchi wala tusingerumbana nao lakn kwa sasa hawatekelezi kwa vitendo ndo maana wanatakiwa wapigwe political technical knockout 2015
 

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,050
2,000
Huyu mama hakubaliani na usemi 'kandamizi' wa wanawake wakiwezeshwa wanaweza. Kufanya kazi UN si mchezo, ana akili sana na mkweli daima. Tatizo ANAVUTWA.
 

Etairo

JF-Expert Member
Jan 17, 2012
244
0
Critical
Katika hili kuna ubaya? Siasa ni maisha kwa wananchi haijalishi kuwa lililosemwa na upinzani awe slaa au mwingine yeyote basi lisifanywe na ccm kwa madai kuwa anafanyia kazi hoja ya slaa, inashangaza kwa wapenzi wa cdm kuona kila kinachofanyika kizuri lazima kiunganishwe na cdm, nchi haiendi hivyo.
Hata kama kuna wazo zuri linatolewa au liliwahi kutolewa na kaburu-achilia mbali slaa ambaye ni mtanzania halisia, litafanyiwa kazi kwa maslahi ya nchi. Hivyo hoja kuwa serikali inafanyia kazi mawazo au hoja za slaaa (cdm) hazina mashiko.
Tujadili masuala yenye maana kwa watanzania kwa lengo la kujenga uwezo wa wananchi kupambana na ugumu wa maisha.
 

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,589
2,000
Tunachohitaji ni unafuu wa maisha bila kujali ni nani kasema au ka-copy wapi maadamu ni kitu chenye maslahi na wananchi.BIG UP MAMA.

Hata kampeni kwakutumia Helicopta CCM waliiga kutoka Chadema! Na hiyo sio Copy & Pest!
 

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
2,731
0
najaribu kuangalia kauli ya mfuko wa cement kuwa utauzwa 5000tsh labda dr slaa alikua ana lengo la chadema kujenga kiwanda cha cement pale ofsi zao kinondoni
 

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,050
2,000
Rais wa awamu ya tatu alituambia sisi ni 'wavivu wa kufikiri' hatukumuelewa na hatutaki kumwelewa.
najaribu kuangalia kauli ya mfuko wa cement kuwa utauzwa 5000tsh labda dr slaa alikua ana lengo la chadema kujenga kiwanda cha cement pale ofsi zao kinondoni
Tungekuwa makini na KAULI za wanasiasa tungemuona Dr Slaa ni vipi angetekeleza ahadi hiyo, lakini tunarukia vitu KIVYEPESI VYEPESI tuu.
 

kingwipa1

JF-Expert Member
Jul 2, 2008
334
225
Tunachohitaji ni unafuu wa maisha bila kujali ni nani kasema au ka-copy wapi maadamu ni kitu chenye maslahi na wananchi.BIG UP MAMA.

Big Up kwa lipi? Kusema bila kutenda wakati uko madarakani? Huku ni kusifia ujinga.
CCM imewatoa akili wasomi wetu kusema wasichokitenda.
Na hao watu wa kipato cha kati wanaolengwa ni wepi? Mimi nina mshahara wa kati ya 2 - 3 mil lakini nikipiga hesabu zangu za kimaisha naona kabisa siwezi kununua nyumba ya 169 mil. Je, hao walengwa ni wepi?
 

scramble

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
1,593
0
kauli za slaa awapo jukwani zimejaa uwongo na ubabaishaji. slaa simuoni kama kiongozi ane faa kuliongoza taifa hili! tuache ushabiki wa kisiasa za maji taka. utaifa kwanza. vua magamba, vua magwanda, VAA UZALENDO!
 

Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,527
2,000
Sio dhambi kufanyia kazi wazo zuri na si busara kujitapia eti lile wazo ni letu/langu cha msingi ni nini watanzania wanataka wapi,lini,kwa namna gani.hoja hapa si kufanyia kazi wazo la mtu fulani,bali ni kauli ya serikali kupitia waziri wake kwamba kitu fulani sasa ni wakati wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom