Prof. Tibaijuka: Rais aache kutumbua nyama akayaita majipu!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Akiongea na Count Down ya Clouds Fm Prof Tibaijuka amesema yeye ni muhanga wa ufisadi. Amesema kuna mtandao wa mafisadi unaotoa watu kafara na wenyewe hauguswi.

"Naafiki kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi, labda itasaidia kukamatwa na kushitakiwa mafisadi wenyewe. Maana wengine tunatolewa kafara na mtandao hauguswi, labda zitaachwa kukamuliwa nyama na kuziita majipu". Alisema Prof Tibaijuka.

My take:
Mtandao huu ni upi? Unalindwa na nani? Hivi Prof ni msafi au anajitetea?
 
Hata mimi naanza kuafiki.maneno ya Tibaijuka. huu ndio ukweli wenyewe. Ukiona mwana CCM ana insinuate jambo kama hili ujue. Si Bure. Angesema mwana ukawa. Matusi wangesemwa wanaona wivu na wamekalia upinzani.
Sasa kasema msisiemu Nguli na profesa tibaijuka.
Magu anatumbua NYAMA.
Binafsi Sijaona usaha mpaka sasa
 
Tibaijuka anatakiwa atuambie huo mtandao ni upi na una kina nani na si kuendelea kutuweka kwenye mabano. Kwa jinsi alivyoongea inaonesha yeye anaujua mtandao hivyo wao kujiita nyama tafsiri yake ni kwamba jipu huota kwenye nyama, sasa wao nyama watueleze hayo majipu yaliyoota juu yao ni yapi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom