Prof. Tibaijuka: Nilitolewa mbuzi wa kafara Escrow

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
99,336
2,000
PROF. TIBAIJUKA: NILITOLEWA MBUZI WA KAFARA ESCROW
WAZIRI wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

WAZIRI wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amefunguka na kusema alitolewa mbuzi wa kafara katika kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Amesema wabaya wake walijikita kuhoji matumizi ya Sh milioni 10, badala ya Sh bilioni 1.6 alizopokea.


Profesa Tibaijuka ameyasema hayo ikiwa ni miaka miwili na nusu tangu avuliwe uwaziri kwa sababu ya kashfa hiyo.

Katika kashfa hiyo, Profesa Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, ni mmoja wa watu waliopata mgao wa fedha hizo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira.

Rugemalira alikuwa mbia wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.

Akizungumza na gazeti hili Dodoma jana, alisema baadhi ya mambo kuhusu suala hilo kama atayaweka wazi yanaweza kuingilia kitabu anachotaka kuandika.

Alisema wakati wabaya wake wakimsakama kwa kauli yake aliyosema kuna Sh milioni 10 alitoa kwenye akaunti yake akisema zilikuwa ni za mboga, vita hiyo ilimsaidia kumuinua badala ya kumuangusha kama walivyotarajia.

“Hili ni swali zuri na kweli sijawahi kufafanua maana yangu ilikuwa nini kusema Sh milioni 10 ni hela ya mboga. Niliona kwamba nilishatolewa mbuzi wa kafara kwa hiyo niachie Mungu.

“Kama akipenda na kunivusha nitapata nafasi ya kueleza jinsi nilivyokumbwa na kadhia hiyo .

“Kumbuka hivi sasa watu wanatumbuliwa kila siku lakini mimi nadhani naingia katika historia ya Tanzania kama mtu pekee aliyetumbuliwa katika Serikali ya Awamu ya Nne, wengine walijiuzulu,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alisema pamoja na hali hiyo kwa sasa wana CCM katika jimbo lake hawataki ujinga kwa sababu waliweza kumsimamia na kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kura nyingi.

“Bahati nzuri pia tukampata Rais mkweli ambaye naye hataki ujinga na utani usio na maana kuingoza Serikali ya Awamu ya Tano.
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
4,961
2,000
I wish I could be president...
Angekuwa anaongelea gerezani sasa hivi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,608
2,000
Alikuwa wapi kuyasema haya akiwa bado Mr dhaifu yupo ikulu??? Na kwanni asimuombe mwenyekiti wake amsake mhusika mkuu wa kupiga pesa za TEGETA ESCROW!!! kama yye ni mbzui wa kafara je mhusika ni nani ssa aliyekuwa analindwa hapa??? Ifike muda hizi tuhuma ziwekwe wazi na wahusika watolewa kinga maana hizi kafara mpaka lini
 

alibaaliyo

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
385
500
Mh Pro Tibaijuka hongera sana. You are my hero. Natambua uwezo wako uliotukuka kitaaluma pia mwanaharakati wa maendeleo. Dunia imetambua hilo na wananchi wapenda maendeleo wa Muleba.
JF inatumika kukuchafua lakini wewe ni mwanamke jasiri umeonyesha kuwa ukiwa na dhamira safi Mungu yuko upande wako.
Mod wa JF tafadhali mwache Prof Tibaijuka afanye kazi zake za ubunge.

Sentensi aliyotamka bungeni ya "unavyopanua....." kwani ina shida gani. Shida iko kwa wanaotafisri kinyume na alichomaanisha. Go Go Professor tuko mashabiki wako wanaotambua uwezo wako hata kabla ya kuwa mbunge. WEWE NI MFANO KWA MWANAMKE ANAYEPIGANIA HAKI NA MAENDELEO. VITABU VITAANDIKWA KWA KUENZI MCHANGO WAKO.
 

alibaaliyo

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
385
500
Mod JF tafadhali acha kuweka hizi habari za kumchafua Prof Anna Tibaijuka. JF ISITUMIKE KUMCHAFUA PROF.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom