MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Prof. Anna Tibaijuka ameyasema hayo wakati akichangia mjadala bungeni kuhusu wananchi waliokumbwa na zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa Umma huku akitoa mfano wa Mbunge wa Mtera (CCM) Livingston Lusinde kwamba licha ya elimu yake ya darasa la saba lakini uwezo wake ni zaidi ya mtu mwenye shahada mbili.
‘’Tukiangalia humu bungeni, Lusinde huwa anapenda kujiita darasa la saba lakini mimi ninamjua huyu ana masters (Shahada ya Uzamili) ni kwamba hana cheti tu. Sasa unaona kwamba ni perspective, Lusinde hawezi kusema ni darasa la saba, sio darasa la saba, elimu yake huyu mtu ana masters tena zaidi lakini sasa sababu ya certification, sisi tumekwama kwenye certification kwa hiyo tunashindwa kwenda mbele kama taifa. Kwa hiyo hilo naomba tuliweke kuwa ni muhimu sana’’.
Prof. Tibaijuka amesema kuna wafanyakazi wengi ambao walikuwa na uwezo mkubwa katika maeneo yao lakini wamejikuta wakifukuzwa kazi kutokana na ukosefu wa vyeti.
Amesema ni vizuri serikali ikaangalia pia uwezo wa mtu kuliko kuangalia vyeti peke yake kwa sababu kutokuwa na cheti hakumfanyi mtu kutokuwa na uwezo katika eneo lake la kazi.
Chanzo: Gazeti la Mwanachi,
Angalizo:
Kwa kiwango kikubwa ninakubaliana na hoja ya Prof. Tibaijuka kwa sababu pia kuna watu wengine kama Mbunge John Mnyika ambaye elimu yake ni kidato cha sita lakini uwezo wake ni zaidi ya mtu mwenye cheti cha Uzamili.
Ninakumbuka tuliwahi kujadili sana uwezo wa Lusinde baada ya mdau mmoja hapa Jamiiforums ( Pascal Mayalla ) kuleta mada (Thread) kuhusu uwezo wa Mbunge Lusinde kwenye Mada hii;

Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.
Wanabodi, Kama ambavyo huwa ninajinasibu humu kuwa, japo mimi nina chama, ila sina mtu, kwenye mazuri napongeza, na kwenye mabaya nakosoa, hili ni Bandiko la Pongezi Kwa Mbunge wa Mtera, Mhe. Livingstone Lusinde. Naangalia hapa Clouds TV, Mbunge wa Mtera, Mh. Livingstone Lusinde anahojiwa...
www.jamiiforums.com