Prof. Tibaijuka, huwezi kufikiriwa kuwa Rais ajaye kwa sasabu kuu mbili...

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,846
2,000
Wanajamvi Umofia kwenu,

Kwanza ulifanikiwa kufanya vizuri UN HABITAT kwa kuwa wenzetu wanamfumo mzuri wa kubana watendaji utendaji kazi wao wasidanganyike WALA KUDANGANYA.

Kwa Tanzania hii na kama ingekuwa tanzania tuitakayo iliyoasisiwa na mhe. Jaji warioba kwa kusikiliza kilio cha wananchi mkaizika Dodoma Tanzania hii ni hatari wewe kupewa nafasi hiyo hata kwa hoja huu ni wakati wa wanawake.

Kwasabu kuu zifuatazo.
1.Nafasi uliyopewa ya waziri wa ardhi uliwaacha Watanzania mdomo wazi na hata wenye uwezo mdogo kupeleka bungeni mpango wa kuwapa Wazungu Kigamboni na Watanzania kupewa karatasi (hisa). Biashara ya ardhi kubadilishana na karatasi ni hatari na haina tofauti na ile ya wakoloni kuwapa wenzetu pipi wakachukua dhahabu. Prof mzima kudanganywa na wazungu watanzania watoe ardhi wapewe karatasi we ukaona ni sawa tu ni ulijitoa sana ufahamu. Ningekuwa kiongozi wako kabla sijakuchukulia hatua ningechukuza umepewa nini mpaka ukajiondoa ufahamu singekutoa hivi hivi kwani moyoni ningebakiwa na swali huyu prof wamempa nini?

Kwanini? hao waliokuambia uende bungeni kutafuta ridhaa ya kubadilisha karatasi na ardhi usingewambia hizo hisa zina sebule ngapi au vyumba vingapi?

Baada ya kukusikia ukiuwasilisha nilikutoa moyoni na akilini kwani mama sikukutegemea ungesaliti Taifa lako Mama makinda nilikuwa simwamini na kumtegemea nafasi aliyopewa angepwaya hivyo hata akipwaya huwa sishangai nashangaa siku akipatia wewe nilikuwa sikutegemei ungetuuuza kwa vikaratasi?

Hao wanaokudanganya uwape ardhi wawape Watanzania karatasi na Ikulu wakakuacha bila kukukanya ukitaka kujua wanaweza kukuchukulia hatua kali na kutokuwa na imani kwao hebu nenda kapime kina cha maji kwa kuwambia waheshimiwa wabunge wizara tunataka tupime maeneo ya Masaki, Oysterbay, Upanga kujenga mji wa kisasa hivyo maeneo hayo ni eneo la mradi wanoishi huko watapewa karatasi (hisa) waachie hayo maeneo.


Kwanza wewe mwenyewe kwa ufahamu wako hutadhubutu kuwaza hivyo na wanaotaka kuwekeza kwa style hiyo uliyotaka kuwafanyia watu wa kigamboni utawachukulia hatua.

Kigamboni ni sehemu ya bahari, masaki, oysterbay nayo ni sehemu ya bahari kuna makazi ya watu kama kingamboni kwanini mpango wa hisa msiupeleke huko nako au Asiyekuwa nacho atanyanganywa hata kile kidogo anadhaniwa anacho na aliyenacho ataongezewa?

Mama mwalimu alikusomesha kwa kodi zetu uje kutusaidia ambao hawakupata nafasi hiyo au waliopata hawakufikia ngazi uliyofikia na kama wamefikia nafasi hiyo umepewa kwa ajili ya kuwatumikia. Kusema kweli katika hilo umewaangusha watanzania uliotaka kuwachukulia ardhi yao kwa kipande cha karatasi na umewaangusha wakina mama.

Hivyo kufikiriwa kwa ajili ya Urais Ujao ni hatari we wakitunyonya unaweza kwenda ngambo ulikokuwa ukalala hata kwa jirani sisi wengine tukipanda ndege ikavuka mipaka ya Tanzania kabla hatujafa ni bahati na kuna familia nyingine hazina hata aliyefika uwanja wa ndege tutakimbilia wapi?

Kumbuka pia hata kwenye ardhi kwa mara ya kwanza mlionyesha weledi kuunga mkono mliunga kama serikali hoja ya ardhi ya mhe.Halima mdee kutatua migogoro ya ardhi mpaka sasa matatizo ya adhi hatua zilizotakiwa zichukuliwe sidhani kama 25% umesaidia serikali na bunge kuwahudumia wananchi.
Vile vile, Kushindwa kujibu hoja za mhe. Halima mdee na kumnanga na kujitoa ufahamu wa hali ya juu huku ukijua wasomi wanapenda hoja ijibiwe kwa hoja yaani mama siku hiyo ulilipuka sana ukidhani unamlipua mtu kumbe unalipua Taaluma yako iliyobeba wakina mama na kuwaweka mstari wa mbele wanaweza.

Sababu ya PILI, Mhe. Mama Prof umetoka wapi ESCROW na wewe ni wa ardhi na makazi au ESCROW ni makazi mie namtafuta mstari wa mbele waziri mhusika Prof. Muhongo simwoni kwenye account za ki ESCROW wewe Mama mbona uko mstari wa mbele sio kwa maslahi mapana ya Wananchi kama mhe. tumbili bali uko katika kundi dogo lililonufaika na Overpayment na kutokulipa kodi. Na umekuwa mstari wa mbele kujitetea, "Nilipewa kwa good faith" baada ya muda Ruge ni ndugu yangu kanisaidia bilioni.
Wakati wengine wamechotewa wakawa kimya wewe uliona ukinyamaza sio maslahi kwa nchi je kuchukua pesa zote hizo mbona hukutafakari ukasema jamani usalama wa Taifa kuna mtu ananipa kibilioni vipi huyu mtu au Usalama kuna ndugu ananipa bilion hebu mchunguzeni kwa kuwa anafanya kitu ambacho ni adimu.
Mama kwa kuwa umeamua kulikupa kwanini usiwambie watnzania nyuma ya pazia ilikuwaje mpaka wakakumegea au kwanini usingewambia watanzania kaombeni hela za wenzetu wamepiga dili la ESCROW mtatue changamoto zenu. Kizuri kula na nduguyo unaweza kututajia ndugu wengine waliopata zali la bilioni au ni wewe tu kwenye familia kulikoni?

Mwisho wadau wanaomuunga mkono Prof. na watakaomwomba kwasababu ya karata ni wakati wa wanawake achukue form mtanisamehe siku ya kura nikalala asubihi mpaka jioni.

Hoja ijibiwe kwa hoja

Nisamehewe kwa wale wanaonufaika kwa kuona Prof akijitoa ufahamu wananufaika na arhi ya kingamboni,nk
Waelewe hisia zangu au hoja zangu sio amri ya 11 ziwafurahishe

Wanaomkataa karibuni kwa hoja zaidi

Wanaomkubali karibuni tena kwa moyo mweupe kwa hoja.
 

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,846
2,000
NAJIULIZA waziri wa ardhi kashfa ya nishati na madini wapi na wapi?
Ukiangalia mhe. Muhongo humuoni akichotewa ingawa ni wizara yake au katibu mkuu alimchukulia?
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,361
2,000
NAJIULIZA waziri wa ardhi kashfa ya nishati na madini wapi na wapi?
Ukiangalia mhe. Muhongo humuoni akichotewa ingawa ni wizara yake au katibu mkuu alimchukulia?
jamani mama alipewa vijisenti tu na kaka yake kwa ajili ya kuendeleza kashule kake. Hata hivyo huyo kaka yake hakuwa na hela nyingi kwani alikuwa na kama vishilingi billioni mia mbili tu ambavyo kwake ni pesa ya kununulia ugoro.

Wengine aliwachangia hela ya harusi kiasi kidogo tu cha zaidi ya tushilingi milioni mia nne.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom