nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,029
- 2,902
Buseresere iko wilaya ya chato na Katoro iko wilaya ya Geita. Hapo umechanganya"Iwapo nia ni kuunda mkoa unaosogeza huduma jirani na wananchi ni busara mkoa huu kuundwa kwa kuweka makao makuu Biharamulo.
Hara hivyo sioni maana/mantiki ya wakazi wa wilaya za Ngara na Kakonko kuvuka wilaya ya Biharamulo wakienda Chato ambayo ni wilaya itakayokuwa pembeni mwa mkoa huu mpya.
Mkoa huu badala ya kunufaisha wakazi wake wengi, utawaumiza.
Pia sioni manufaa atakayoyapata mkazi wa Buseresere na Katoro kwa kuwa ataongeza umbali wa kwenda makao makuu ya mkoa.
Hata hivyo nashauri serikali badala ya kuwaza kuongeza mikoa, ijikite kupunguza ukubwa wa vijiji na kata.
Hili liende sambamba na kuwarahisishia utendaji wa kazi zao viongozi wa vijiji na kata kwa kuwapa usafiri, vifaa vya kazi kama kompyuta mpakato, simu zinazoweza kupata matukio [picha] vema.
Hapa Ngara kwenye kata ya Muganza, umbali kutoka Kitongoji cha Nyakafandi hadi makao makuu ya Kijiji chao cha Mukubu ni km.15.
Kutoka kitongoji hicho hadi makao makuu ya kata ni zaidi ya km.30.
Mtendaji wa kata na kijiji hawana usafiri wowote.
Huko hakuna umeme.
Wangeweza kusaidiwa kupewa umeme wa jua kwenye ofisi zao ili wachaji simu zao ambazo Kwa sehemu kubwa zinafanya kazi za ofisi.
Wananchi hatuna hitaji la mikoa na wilaya.
Tunahitaji zaidi huduma bora za vijiji na kata.
Ikumbukwe miaka michache iliyopita ukubwa wa vitongoji uliongezwa badala ya kupunguzwa.
Kuna sehemu mitaa/vitongoji vitatu viliungwa kuwa kimoja.
Mzigo uliongezeka."