Prof. Tibaijuka amjibu Jussa; adai Jussa amepotosha Wazanzibari

fikrapevu sungura

Senior Member
Oct 26, 2011
110
11
LEO tumechapisha habari zinazomnukuu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akishangazwa na kauli iliyotolewa katika Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Mji Mkongwe kwa tiketi ya CUF, Ismail Jussa kwamba andiko lililowakilishwa katika Umoja wa Mataifa (UN) na waziri huyo kuomba eneo la ziada nje ya maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi Baharini (EEZ) halikufanywa kwa niaba ya Serikali ya Muungano kwa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haikushirikishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri Tibaijuka alisema andiko hilo liliwasilishwa Januari 18 mwaka huu kama ombi la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuongeza kuwa, SMZ ilishirikishwa kikamilifu tangu mchakato wa kuandaa mradi huo ulipoanza mwaka 2007.

Waziri alitoa kauli hiyo baada ya mwakilishi huyo kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi mwanzoni mwa wiki, akilitaka Baraza kutolitambua andiko hilo lililowasilishwa UN na kuliomba liiagize SMZ kutojihusisha na mpango huo kwa namna yoyote kwa madai kwamba ni mpango wa kuhujumu eneo la bahari la Zanzibar. Mwakilishi huyo alikwenda mbele zaidi na kumtaka Waziri wa Ardhi, Ali Juma Shamhuna ajiuzulu, vinginevyo awajibishwe na Rais, huku akiungwa mkono na wajumbe waliosimama kuchangia hoja hiyo.

Tunampongeza Waziri Tibaijuka kwa uamuzi wake wa kukutana na waandishi wa habari jana na kuchukua muda mrefu kutoa ufafanuzi wa suala hilo ambalo tunadhani lingeweza kusababisha msuguano usiokuwa wa lazima kati ya pande mbili hizi za Muungano wetu. Tunasema hivyo kwa sababu tuhuma alizotoa mwakilishi huyo ni nzito mno pengine kuliko yeye anavyofahamu. Ndiyo maana tuhuma kama hizo zinapotolewa, serikali makini popote duniani hulazimika kuzijibu kwa ufasaha pasipo kuzibeza au kutoa majibu ya mkato kwa nia ya kuzificha chini ya zulia.

Hivyo ndivyo Waziri Tibaijuka alivyofanya na tunakubaliana naye kabisa aliposema alilazimika kutoa ufafanuzi wa kina kwa sababu pande hizo mbili za Muungano hazipaswi kugombea fito wakati nyumba inayojengwa ni ya wote. Moja ya sababu zinazotufanya turidhishwe na ufafanuzi wake ni pale alipotoa ushahidi wa namna Zanzibar ilivyohusishwa kikamilifu kupitia SMZ katika ngazi zote tangu 2007, kiasi cha kuibua mashaka kama kweli mwakilishi huyo wa Mji Mkongwe alipeleka hoja hiyo barazani kwa nia njema au alidhamiria kuwachafua viongozi wa pande hizo mbili za Muungano kwa kupeleka hoja iliyojengwa kwa misingi ya maneno ya mitaani?

Ufafanuzi wa Waziri Tibaijuka umetufumbua macho na sasa tumeelewa kwamba mchakato huo mkubwa na muhimu uliendeshwa na kamati mbalimbali zilizoundwa tangu mwaka 2007, ikiwamo kamati ya makatibu wakuu iliyoongozwa na Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, Nishati, Ujenzi na Makazi Zanzibar, Mwalimu Mwalimu na kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upimaji Ramani, Haji Adam Haji ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi. Sasa tumejua pia kwamba Pandu Makame kutoka katika Ofisi ya Makamu wa Rais ndiye aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Utekelezaji.

Tumefarijika kusikia kutoka kwa waziri huyo kuwa, zoezi la kupima alama za sehemu ya bahari inayoombwa lililofanyika Januari mwaka jana, masheha wa Kiuyu, Maziwa Ng'ombe, Kojani na Vitongoji walioko katika Kisiwa cha Pemba walishirikishwa, huku wenzao wa Makunduchi katika kisiwa cha Unguja pia wakishirikishwa. Hata wakati wa kuwakilisha andiko hilo huko UN ujumbe wa nchi yetu uliwahusisha viongozi wa pande mbili za Muungano, akiwamo Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ayoub Mohamed Mahamoud.

Sisi wa Mwananchi tunajivunia rekodi yetu ya muda mrefu ya kutetea haki za wananchi wa Zanzibar pale tunapoona zinakiukwa. Lakini tumefadhaishwa na tuhuma hizo zilizotolewa dhidi ya SMZ na Serikali ya Muungano na mwakilishi huyo wa Mji Mkongwe. Tunamshauri apate ujasiri na kuomba radhi kwa Baraza la Wawakilishi, SMZ na Serikali ya Muungano kwa upotoshaji mkubwa alioufanya.

Source: Mwananchi

Jussa ameupotosha Umma - Serikali

na Happiness Mnale

SERIKALI imesema taarifa iliyotolewa na mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu (CUF) kuwa Zanzibar haikushirikishwa kwenye mradi wa kuongeza eneo la ziada nje ya ukanda wa kiuchumi baharini si za kweli na inalenga kupandikiza chuki kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema mpango huo umewashirikisha wajumbe na viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Waziri Tibaijuka alisema jambo hilo ni la Muungano wa Tanzania wala si la wizara yake, ndiyo maana waliamua kuwashirikisha wenzao wa Zanzibar.
Alibainisha kuwa Jussa hakufanya utafiti wa kutosha kuhusu jambo hilo kabla ya kutoa taarifa yake kuwa Tanzania Bara inaiburuza Zanzibar katika jambo hilo.
"Ujumbe uliokwenda Marekani uliwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, si Tanzania Bara pekee kama alivyodai Jussa, hakuna haja ya kuvutana juu ya jambo hili.
"Tusigombee fito wakati tunajenga nyumba moja, wanaotaka kunikomoa mimi wanajidanganya, kwani watajikomoa wenyewe," amesema Tibaijuka.
Aliongeza kuwa hawezi kukurupuka katika kulishughulikia jambo hilo bila Rais Jakaya Kikwete na Dk. Mohamed Shein kulifahamu, kwani yeye hana mamlaka nalo na aliukuta mradi huo ukiwa na miaka miwili.
Waziri Tibaijuka alisema mchakato wa kuongeza eneo la ziada ulipitiwa na kushirikishwa kwa kamati mbalimbali, SMZ na Baraza la Mawaziri, ambapo wizara yake ilipewa baraka za kuendelea nalo.
Aliongeza kuwa wizara yake iliendelea na mchakato wa kudai eneo la nyongeza nje ya ukanda wa kiuchumi baharini ikiwa ni pamoja na kukusanya takwimu za jiolojia na taarifa ili kuthibitisha dai la Jamhuri ya Muungano katika kustahili kudai eneo hilo, hivyo haoni sababu ya kushambuliwa.
Juzi Jussa aliwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi akidai kuwa mchakato huo haukuishirikisha Zanzibar.

Kuomba radhi pekee haitoshì. Aueleze umma kapata wapi taarifa hizo na sababu ya yeye kuziamini. Ni matumaini mwakilishi hufanya tafiti kabla ya kuomba majibu kwa serikali. Kosa alilolifanya ni sawa na uhaini. Nawakilisha.
 
Umefanya la busara mama. Wakati mwingine bora tu kumjibu MPUMBAVU ili kusafisha hewa aliyochafua.
 
Source: Mwananchi

LEO tumechapisha habari zinazomnukuu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akishangazwa na kauli iliyotolewa katika Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Mji Mkongwe kwa tiketi ya CUF, Ismail Jussa kwamba andiko lililowakilishwa katika Umoja wa Mataifa (UN) na waziri huyo kuomba eneo la ziada nje ya maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi Baharini (EEZ) halikufanywa kwa niaba ya Serikali ya Muungano kwa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haikushirikishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri Tibaijuka alisema andiko hilo liliwasilishwa Januari 18 mwaka huu kama ombi la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuongeza kuwa, SMZ ilishirikishwa kikamilifu tangu mchakato wa kuandaa mradi huo ulipoanza mwaka 2007.

Waziri alitoa kauli hiyo baada ya mwakilishi huyo kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi mwanzoni mwa wiki, akilitaka Baraza kutolitambua andiko hilo lililowasilishwa UN na kuliomba liiagize SMZ kutojihusisha na mpango huo kwa namna yoyote kwa madai kwamba ni mpango wa kuhujumu eneo la bahari la Zanzibar. Mwakilishi huyo alikwenda mbele zaidi na kumtaka Waziri wa Ardhi, Ali Juma Shamhuna ajiuzulu, vinginevyo awajibishwe na Rais, huku akiungwa mkono na wajumbe waliosimama kuchangia hoja hiyo.

Tunampongeza Waziri Tibaijuka kwa uamuzi wake wa kukutana na waandishi wa habari jana na kuchukua muda mrefu kutoa ufafanuzi wa suala hilo ambalo tunadhani lingeweza kusababisha msuguano usiokuwa wa lazima kati ya pande mbili hizi za Muungano wetu. Tunasema hivyo kwa sababu tuhuma alizotoa mwakilishi huyo ni nzito mno pengine kuliko yeye anavyofahamu. Ndiyo maana tuhuma kama hizo zinapotolewa, serikali makini popote duniani hulazimika kuzijibu kwa ufasaha pasipo kuzibeza au kutoa majibu ya mkato kwa nia ya kuzificha chini ya zulia.

Hivyo ndivyo Waziri Tibaijuka alivyofanya na tunakubaliana naye kabisa aliposema alilazimika kutoa ufafanuzi wa kina kwa sababu pande hizo mbili za Muungano hazipaswi kugombea fito wakati nyumba inayojengwa ni ya wote. Moja ya sababu zinazotufanya turidhishwe na ufafanuzi wake ni pale alipotoa ushahidi wa namna Zanzibar ilivyohusishwa kikamilifu kupitia SMZ katika ngazi zote tangu 2007, kiasi cha kuibua mashaka kama kweli mwakilishi huyo wa Mji Mkongwe alipeleka hoja hiyo barazani kwa nia njema au alidhamiria kuwachafua viongozi wa pande hizo mbili za Muungano kwa kupeleka hoja iliyojengwa kwa misingi ya maneno ya mitaani?

Ufafanuzi wa Waziri Tibaijuka umetufumbua macho na sasa tumeelewa kwamba mchakato huo mkubwa na muhimu uliendeshwa na kamati mbalimbali zilizoundwa tangu mwaka 2007, ikiwamo kamati ya makatibu wakuu iliyoongozwa na Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, Nishati, Ujenzi na Makazi Zanzibar, Mwalimu Mwalimu na kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upimaji Ramani, Haji Adam Haji ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi. Sasa tumejua pia kwamba Pandu Makame kutoka katika Ofisi ya Makamu wa Rais ndiye aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Utekelezaji.

Tumefarijika kusikia kutoka kwa waziri huyo kuwa, zoezi la kupima alama za sehemu ya bahari inayoombwa lililofanyika Januari mwaka jana, masheha wa Kiuyu, Maziwa Ng’ombe, Kojani na Vitongoji walioko katika Kisiwa cha Pemba walishirikishwa, huku wenzao wa Makunduchi katika kisiwa cha Unguja pia wakishirikishwa. Hata wakati wa kuwakilisha andiko hilo huko UN ujumbe wa nchi yetu uliwahusisha viongozi wa pande mbili za Muungano, akiwamo Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ayoub Mohamed Mahamoud.

Sisi wa Mwananchi tunajivunia rekodi yetu ya muda mrefu ya kutetea haki za wananchi wa Zanzibar pale tunapoona zinakiukwa. Lakini tumefadhaishwa na tuhuma hizo zilizotolewa dhidi ya SMZ na Serikali ya Muungano na mwakilishi huyo wa Mji Mkongwe. Tunamshauri apate ujasiri na kuomba radhi kwa Baraza la Wawakilishi, SMZ na Serikali ya Muungano kwa upotoshaji mkubwa alioufanya.
Very good! I knew this Juha sorry Jussa was tempering with a straight shooter; the worlds' authority on these issues. Now my dear Jussa where will you hide your poor head? pretending to work on the interests of the islanders eh! very sorry. Can Barubaru come in please!?
 
ahaha,jussa,..mimi sijastuka kwa zle tuhumaa alizozitoa hyu bwan zidi ya serikali ya jamhri ya muungano wa tz,hnst jussa ni maradhi mapya ya siasa za kikanda anazo ubiri kila kukicha kuwaaminisha wa zenj kua wanaonewa kila kitu..?jamaa afanyi tafifti yoyte mara nying anaropoka tu..,sasa sijui chama chake hki ni cha kikanda ama?...labda as time goes on tutajua the hidden agenda ya cuf......may they are after kubomoa muungano,ukizingatia na kauli tetete za maarim seif...
 
Porojo za Jussa zitatupeleka pabaya anaonekana kuwa ni kiongozi asie na subira wala sio mfuatiliaji wa mambo.
 
Nahisi Jussa amezoea siasa za kishwari. Sasa baada ya serikali ya umoja wa kitaifa anatafuta namna ya ku-practice ushwari. Hivi ni kweli Jussa hakujua kama Zanzibar ilishirikishwa kwenye mchakato wa kudai hili eneo? Na kama hakujua hilo, alifanya nini kujiridhisha kuwa Zanzibar haikushirikishwa kabla ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye baraza la wawakishi? Inakuwaje mtu akurupuke na kuleta hoja kwenye chombo cha kutunga sheria bila ya kufanya research?
 
Jussa ni kipaza sauti tu. Kwa nini yule Mwigamba wa TD anaonekana ni mchochezi na sio Jussa?
 
Jussa ni Naibu katibu mkuu wa CUF zanzibar baada ya katibu Mkuu wa CUF na makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif lakini pia Jussa ni Mkurugenzi wa mambo ya nje wa CUF yuko jikoni karibu kabisa na mapishi. Muuza nyanya na raia wa kawaida wa zanzibar anasemaje kama kiongozi aliye karibu na taarifa, anayeweza kuzifikia taarifa kwa urahisi anakurupuka kiasi hicho. Ni aibu

Jussa alikuwa na fursa ya kumtumia Seif kupata ukweli wote kutoka serikalini.
 
Jussa kalidanganya baraza la wawakilishi na umma wa watanzania kupitia baraza hilo na mikutano ya hadhara. Anatakiwa kusimamishwa japo vikao 6
 
ukweli utabakia ukweli tu hata kama utaupotosha au kuuficha uvunguni lakini kuna siku utakuwa hadharani -- haya ni baadhi tu ya kero za muungano ambazo viongozi wetu hawataki kabisa vijadiliwe. hapa wenye akili zetu tunajua kabisa kwamba zanzibar si nchi na ndiyo maana haijulikana umoja wa mataifa, chochote wanachotaka kukiomba lazima waishirikishe Rep. of Tanzania.

Sasa unapozuia mambo kama haya yasijadiliwe kwenye mchakato huu wa katiba mpya sijui unaficha nini ambacho wananchi hawajui -- kazi ipo. Jusa ana haki ya kusema ni haki yake kikatiba.
 
mie niliwambia huyu Jamaa anatumika, Hivi inaingia akilini hoja ya mipaka isijadiliwe na Baraza la Mawaziri na kuwa na baraka za Rais, Kumbuka Mh.DR. Shein ni mjumbe ktk Baraza la Mawaziri hivyo ameridhia. Hao waliokataa kuwa SMZ haina habari ni wanafiki tu. Jussa sasa aseme tu anatumwa nannani kuchafuaq hali ya hewa? Angalieni isije ikawa ni kazi ya SEIF maana jamaa huyu sio wa kumwamini sn.

Tukumbuke kuwa ZENJ sio nchi jamani, hivyo haiwezi kuomba kuongeza kupanua mpaka wake na mataifa mengine kkwa kuwa sio Taifa. Na ninyi wazenj pimeni kauli za watu kwa kuziweka kwenye mizani sio kila jambo hawa wabara wanahujumun Zenj. mungu ibariki Tanzania yetu hata wale wanaotuonea kijicho nao uwatazame na uwakaripie kwa upole. Na watu wote mnaoitakia mema TANZANIA seme: AMINA
 
Agenda kubwa kwa akina Jussa ni moja tu. Ni Zanzibar ya hadi tarehe 11.01.1964 irudi. Haya mengine ni mapambio. Kikwazo kikubwa kabisa kwa hili ni MUUNGANO. Huu ukivunjwa kazi zingine huko mbele sawa na kumsukuma mlevi tu.
 
Kama kweli Jussa alipelekwa na Rostam 'king maker' kwa JK ili ampe ubunge wa kuteuliwa basi something bad or unusual is about to happen.Tusubiri tuone
 
Back
Top Bottom