JERUSALEM 2006
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 526
- 583
Natumai hamjambo wana_jamiiforum.
Juma lililopita nilitembelea wilaya ya Muleba mkoani Kagera katika jimbo la uchaguzi la Waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi, Prof Anna Tibaijuka. Katika uchaguzi mkuu wa 2010 huyu mama alipita bila kupingwa, hivyo basi kuwafanya wananchi wa muleba Kaskazini kumchagua hata kama walikua hawamtaki. CHADEMA na CUF walimpa heshima ya pekee kwa kutomuwekea mpinzani kwani alikua na uhusiano mzuri na hivi vyama vya siasa na pia alikua anakubalika kwa wananchi.
Wanajamvi sikuamini macho yangu wala masikio yangu kwa yale niliyo yaona na kuyasikia huko vijijini. Wananchi wanasema liwalo na liwe kwani huyu mama amewasahau kabisa tangu apewe uwaziri. Kwa ufupi hajawahi kufanya mkutano wowote wa hadhara unao tathimini shughuli zote za maendeleo ya jimbo lake. Ameshindwa kufanikisha na kutekeleza ahadi zake na kuonekana kuwa ni mzushi.
Wana_muleba wanawaomba CHADEMA kutofanya makosa waliyoyafanya uchaguzi uliopita, na wanaombwa kumsimamisha mgombea katika jimbo hilo la uchaguzi linaloonekana kuwa wazi.