Yo Yo
JF-Expert Member
- May 31, 2008
- 11,217
- 1,702
Nyani Ngabu ina maana huoni alichokiandika Kuhani
BTW Kumbe kijana ni mshika pembe wengine wanakamua maziwa.....cupcake wako leo.......
First Lady,
Hata mimi ningefurahi kama angekuwa amefungua hiyo branch ya ICSU Tanzania badala ya ugenini. (By the way, ukisema "...was the first and founding Director of ..." maana yake nini?)
Na anaweza kutokea opponent wa Kiafrika huko anaejua yanayoendelea Tanzania akam corner ajieleze:
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa STAMICO kwa miaka kumi sasa, kwa hiyo madudu yoooote ya ufanisi mbovu, ufisadi lukuki, vifo vya wachimbaji, unyuma wa jamii zilizo karibu na migodi, hasara kwa Taifa ziletwazo na misamaha ya kodi, na ufukara wa wachimbaji wadogo wadodo, yooooote haya yametokea chini ya usimamizi wa bodi ya Wakurugenzi wako, au?
Utakwendaje wewe mkurugenzi wa bodi ya Wakurugenzi wa STAMICO kuchunguza vifo vya migodini wakati ajali zenyewe inawezekana zinatokea kutokana na uzembe fulani wa STAMICO?
Na hiyo tume yako ya uchunguzi iligundua nini, na nini kimebadilika?
Wakati ukiishi nje ya nchi, kwa nini hujiuzulu majukumu yako yanayohusiana na STAMICO, idara ya nyanja muhimu ya uchumi, iliyofeli kazi kwa kila aina ya vipimo?
Mkeo anaitwa Bertha, ana shahada tatu. Bertha who? Kuliko kuweka shahada za mkeo weka jina lake kamili. Unaionyesha dunia kwamba bado una mfumo dume! Na kijana wako mwenye shahada mbili huyu, info nzuri zaidi hapa ni majina ya hao yatima uwaleao, sio shahada za non-candidate family members!
La mwisho, kwa sehemu nyingine, mfano USA (na hawa ndo vinara wenye influence ya nani anakuwa nani na nini kinafanyika United Nations na matawi yake), unapo ji-introduce kama professor unajulikana kama ni mwalimu. Hiyo inakushushia executive profile yako kwa sababu unaonekana unajiuza kama mtu wa academia ambae hana executive credentials. Ondoa hiyo professor weka title ya Doctor!
BTW Kumbe kijana ni mshika pembe wengine wanakamua maziwa.....cupcake wako leo.......