Prof. Shivji: "Katiba ya Tanzania inampa Rais nafasi ya kuwa Dictetor!" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Shivji: "Katiba ya Tanzania inampa Rais nafasi ya kuwa Dictetor!"

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by nsami, Jan 7, 2011.

 1. n

  nsami Senior Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhadhiri mwandamizi wa UDSM (msitaafu) na mwenyekiti wa Kigoda cha Mwl Nyerere amewaambia wanafunzi wa Udom kuwa Katiba ya Tanzania ya 1977 inampa Rais mwanya wa kuwa dictator.

  Amesema hayo jana katika mhadhara (public lecture) ulioandaliwa na serikali ya wanafunzi UDOSO chuo cha elimu kuhusu "Tafakuri Juu ya Mchakato wa Kutunga Katiba"

  Amesema katiba hii inampa rais mamlaka ya kuwa mkuu wa nchi, mkuu wa serikali, sehemu ya bunge na Amiri jeshi mkuu wa nchi. Jambo ambalo hata mwalimu alishawahi kukiri kuwa inampa mwanya wa kuwa dictator ingawa yeye hakutaka kuwa dictator.

  Kwa mujibu wa Prof. Suala la katiba mpya sio suala la muda au umri wa katiba iliyopo, kubwa na la msingi ni mchakato uliotumika kuipata katiba hiyo.

  Tanzania tangu ipate uhuru imeshaandika katiba mpya tano kwa michakato tofauti.

  Ya kwanza ni katiba ya uhuru (independence constitution) ya 1961, ilipitishwa na Bunge la waingereza.

  Ya pili ni katiba ya jamhuri (Republican constitution) ya 1962 iliyopitishwa na bunge maalumu la katiba (constitution assembly)

  Ya tatu ni ile ya muungano 1964 iliyotungwa na rais wa URT kwa mamlaka aliyopewa na article of union.

  Nne ni (entering constitution) ya 1965 ilipitishwa na bunge la kawaida. Iliundwa kwa mfumo wa chama kimoja ingawa vilikuwepo viwili TANU-Tanganyika na ASP-Zenji.

  Ya tano 1977 ya mfumo wa chama kimoja CCM ilipitishwa na bunge la katiba ingawa wajumbe wake ni walewale waliokuwa ktk kamati ya rais, na ktk tume.

  Naomba kutoa hoja.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,845
  Trophy Points: 280
  naaam na hatuitaki tushaichoka
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Namkubali shvji az a critical thinker,siku zote huwa mkwel na haogopi,ni miongoni mwa wasomi wachache waliobakia,mwingne aliyebakia ni DR AZAVELI LWAITAMA,PROFESA BAREGU,PROFESA OMARI,namkumbuka sana mwanaharakat PROF HAROUB OTHMAN,huyu nae alikua mwanaharakat wa kweli,RIP,but nina imani mwanaye anayesoma huko cuba atafuata nyayo,nae ni radical,wasomi wengne wamuige shvji,kuiga jambo jema si vibaya
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Na Proffessor Chachage Chachage jamani,Rest in peace.Shivji is an asset to this nation,he is never biased na always considers what benefits the majority.Live long Prof.We need a new constitution.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  yeah,chachage aliandika kitabu chake cha MAKUWADI WA SOKO HURIA,ukibahatika kisome ndugu-ni riwaya nzuri,dah cku zote watu wazuri ndio hufa mapema,maneno hayo aliwah kuyazungumza shvj pale NKRUMAH HALL UDSM
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Inafahamika. Na mkwere ndo anatumia ubovu wa katiba yetu kutu dictate waTZ! Jambo la msingi katika kuja na katiba mpya ni aina ya mchakato utakaotumika. Mi sioni umuhimu wa kua na tume,tume zilishakuwepo za jaji Nyalali na Kisanga. Na zilitoa mapendekezo mazuri sana. Kwa sasa,mi nataka elimu juu ya katiba itolewe,then wawakilishi wa makundi yote ya kijamii wakae na kuandaa rasimu,then wanasheria waliobobea ambao watachaguliwa na mkutano wa hayo makundi ya kijamii,wapewe jukumu la kuandika katiba mpya kwa kuzingatia rasimu ya hayo makundi.
   
 7. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nimekisoma Bababiri,nafikiri members wote wa Jamii Forums wangekisoma pengine tungekuwa na majibu mazuri sana ya matatizo mengi tunayopitia kama nchi maskini sijui na pengine kupata majibu ya maswali magumu tunayojiuliza kila siku ya maendeleo,siasa,uchumi na jamii kwa ujumla?
   
 8. R

  Robin Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Please jamani, kama kuna mwenye soft copy ya hiki kitabu atuwekeee jamvini. Mbarikiwe sana
   
 9. r

  ruz New Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Soft copy hiyo hapo
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,135
  Trophy Points: 280
  Yes, ni kitabu kizuri sana na nilibahatika kuhudhuria mhadhara wake kuhusu kitabu hicho, R.I.P Chachage, kumbukeni ndo huyu aliekataa uwekezaji feki wa MLIMANI CITY na kugawanywa kwa UDSM kuwa na Colleges with reasons
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160

  Alitaka soft copy ya kitabu cha late prof Chachage kinaitwa MAKUWADI WA SOKO HURIA na sio katiba ya Tanganyika na Zanzibar
   
Loading...