Prof. Shivji adhalilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bungeni

Hata mimi nilimsikia Nahodha akisema hupaswi kusema ukweli kwa kilakitu, kunawakati ukisema ukweli unaweza kuvuruga usalama (amani ) ya nchi. Wanajaribu kukwepa hoja zilizo wazi za Tundu Lisu. Na leo amewakamata kweli.
Werema ni ziro kweli Kikwete ni kipofu kama mpaka sasa hajaona kuwa ana mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ndiye mshauri na kiongozi mkuu wa sheria serikalini na hajui sheria au anatafsiri vibaya sheria za nchi, basi na kikwete mwenyewe ni zero.

werema kuonyesha ni sifuri, atajichanganyaje kuhusu sual la chenji ya rada!!!!, rada , mawasiliano ya anga, hali ya hewa ni masuala ya muuungano.Kama kuna fedha ilichukuliwa kununua rada ni wazi ilikuwa ni fedha ya muungano, iweje akubali rada ni suala la muungano, lakini fedha haikuwa ya muungano, huyu anajua sheria mpka amdharu prof shij ati ni mwadishi wa katiba na si mtaalamu wa sheria.werema mtupu sana.
 
Tatizo la Warema ni kuacha taaluma na kuchanganya siasa na taaluma, ni ukweli ulio wazi kuwa uwezi tegemea Dr Mwakyembe azungumze jambo lolote kuupinga Muungano, Haya na huyu Profesa Paragamanda Kabudi ndio magamba zuri kabisa, uwezi tegemea aseme jambo lolote v/s Muungano. Anachofanya Warema ni kumdhalilisha Prof Shivji kwa kuwa uwa anaongea ukweli kuhusu ubaya wa serikali hii dhaifu ya CCM na ubovu wa katiba ya sasa na zaidi ubovu wa MUUNGANO wetu. Namshauri sana Warema, kuhusu shule hawezi kumfikia TUNDU LISSU na mbaya zaidi hawezi kufikia hata 1/4 ya uwezo wa Prof Shivji. Warema ana njaa na anazeeka vibaya. Hawa ndio wakushughulikia baada ya kuchukua nchi 2015...kuna watu wengi sana wataikimbia hii nchi mwaka 2015.
 
Nahodha ni mmoja wa watu wasioutaka muungano. mmeona alivyosita kutoa ushauri. eti ''ukweli usemwe lakini siyo sana unaweza kuleta vurugu na machafuko''

Hapo ni sawa kabisa. Nahodha anaonekana wazi anajikakamua kuutetea muungano lakini moyoni mwake nafsi inamsuta.
 
Huyu jamaa, ana hasira bada ya Prof. Shivji, kuiponda ponda rasimu ya katiba aliyoiwasilisha,
 
katika jambo lisilotarajiwa, hatimaye mwanasheria wa serikali mh. werema amejikuta akimkashfu prof. shivji ambaye ni mhadhimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam na mwenyekiti wa kigoda cha mwal. JK nyerere kwa kumwambia yeye (Prof. shivji) anajua sheria za katiba kwa kusoma (NADHARIA) wakati maprof. wengine (aliwataja) wanaijua katiba kwa vitendo, Hayo yametukia pale ambapo werema alitakiwa kuisemea serikali juu ya hoja ya Mungano iliyosomwa na mh. Tindu lisu (CHADEMA) kwa kunukuu mistari kadhaa katika kitabu cha legal union of Tanzania kilichoandikwa na prof. Shivji ambacho kinaonyesha kukiukwa kwa sheria za muungano. my take: Serikali ismkashfu prof. Shivji kisa tu anatetea haki ya mtanganyika!
 
hakuna kiongozi ndani ya magamba anayeweza jenga hoja za kweli kuhusu katiba kwani itawamaliza hivyo watabakikujiumauma tu.sawa na demu aliyetongozwa amekubali lkn ameshindwa kusema ndiyo amebaki kujiumauma tu .
 
Katika hali ya kushangaza leo jioni hii baada ya Mwanasheria Mkuu kushindwa kujibu hoja juu ya Muungano zilizotolewa na hotuba ya Kambi ya Upinzani (Lissu) amejikuta akisema kuwa Lissu amenukuu mwanasheria ambaye hakusoma katiba , nanukuu " kwa bahati mbaya umemnukuu Prof.Shivji, huyu alikuwa academic advisor wangu" lakini mbona hukunukuu wengine kama Prof.Kabudi, Dr.Mwakyembe kuhusu Muungano?.......huyu uliyemnukuu (Shivji) hakusomea sheria ya katiba ila ni mwandishi wa mambo ya katiba........."

Kauli hii nimeiona ni kama tusi kwa Prof.Shivji ambaye ndio huyo huyo aliyewafundisha wakina Mwakyembe , Kabudi ,Werema ..kuhusu sheria na alikuwa mkuu wa kitivo kwa miaka nenda rudi.Kitendo cha leo kusemwa kuwa yeye ni mwandishi tuu na hapaswi kunukuliwa naona ni udhalilishaji mkubwa kwa huyu gwiji wa sheria na anayeheshimika ndani na nje ya nchi yetu.

Nafikiri kuna haja ya kumpima huyu AG wetu ,


Pili, kuhusu suala la Nahodha , leo kasema kuwa Lissu kasema ukweli lakini sio mara zote ukweli unapaswa kusemwa kwani unaweza ukaleta mitafaruku hivyo ukweli usiwe unasema sana .

Nikagundua kuwa kumbe CCM uongo ni jadi yao na wanataka watanzania wote wasiuseme?

Naomba kuwasilisha.

Mkuu cha kusikitisha ni kuwa AG kajifanya kutokuona kuwa Lissu amemnukuu Shivji kwenye kitabu/chapisho linalohusu Muungano (The foundations of the Union, sina uhakika kama nimepatia title hii), na wala sio masuala ya katiba kama AG anavyotaka kutuaminisha.

Amenisikitisha sana, lakini nadhani kuna kitu au dhana anataka kutuaminisha kuhusu machapisho au mafundisho ya Shivji.
 
Kwanza napenda kuweka rekodi sawa. Prof. Issa Ghullamhussein Shivji(PhD) hakuwahi kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria-UDSM. Kuhusu Werema,huyu amekosa staha. Mwanasheria yeyote anaweza kufanya chochote kihusianacho na sheria. Hata kama Prof. Shivji hakusoma Sheria za Katiba,anabaki kuwa Mwalimu bora wa Katiba na mbobezi kuliko hata waliosomea sheria hizo. Hata iweje,Werema na aliowataja hawamfikii Prof. Shivji...
 
Sikupenda alivokuwa akijibu hoja za Lisu. Aliweka mikono mfukoni kama ishara yeye ni zaidi na naliiona kama jeuri.
imekuwa tabia ya baadhi ya mawaziriri kuwaponda wapinzani ili waonekane si lolote. Werema ni kitu gani hasa kwa profesa Shivji. labada hayo madaraka
 
werema kuonyesha ni sifuri, atajichanganyaje kuhusu sual la chenji ya rada!!!!, rada , mawasiliano ya anga, hali ya hewa ni masuala ya muuungano.Kama kuna fedha ilichukuliwa kununua rada ni wazi ilikuwa ni fedha ya muungano, iweje akubali rada ni suala la muungano, lakini fedha haikuwa ya muungano, huyu anajua sheria mpka amdharu prof shij ati ni mwadishi wa katiba na si mtaalamu wa sheria.werema mtupu sana.

Sasa Werema atuambie wakati wizara ya ulinzi inaomba kupitishiwa bajeti ikiwemo na hiyo hela ya rada kuna sehemu waziri mhusika alisema sehemu ya hela ni ya ulinzi zanzibar na nyingine Tanganyika? Au aliomba kwa ujumla wake wakiwemo na wazanzibar?
 
Huyo werema hamuwezi Shivji shimvi ,prfsor na mwanasheriawa kuchaguliwa vitu viwili tofauti yule Shivji ameandila vitabu vingi huyo werema hajawahi andika kitabu hata cha wanafunzi wa certificate wajifunze sheria bado ni mwanafunzi wa Shivji awe na heshima
 
Mimi sijui mambo ya sheria sana lakini huwezi kulinganisha werema na shivji kwani shivji yupo juu mno hata Kama werema atasoma tena sheria miaka 100 kuanzia sasa hamfikii
 
Huyo werema hamuwezi Shivji shimvi ,prfsor na mwanasheriawa kuchaguliwa vitu viwili tofauti yule Shivji ameandila vitabu vingi huyo werema hajawahi andika kitabu hata cha wanafunzi wa certificate wajifunze sheria bado ni mwanafunzi wa Shivji awe na heshima

leo werema amefanya siasa za shombo ya samaki
 
Huyo werema hamuwezi Shivji shimvi ,prfsor na mwanasheriawa kuchaguliwa vitu viwili tofauti yule Shivji ameandila vitabu vingi huyo werema hajawahi andika kitabu hata cha wanafunzi wa certificate wajifunze sheria bado ni mwanafunzi wa Shivji awe na heshima

leo werema amefanya siasa za shombo ya samaki,yeye yupo pale as lawyer tena A.G,jamaniiiiiiii
 
Back
Top Bottom