prof. shivj, dr. lwaitama, prof.balegu kuandaliwa mihadhara chuo cha uhasibu arusha


M

Moses James

Senior Member
Joined
Dec 13, 2012
Messages
132
Likes
0
Points
0
M

Moses James

Senior Member
Joined Dec 13, 2012
132 0 0
Wanajf tumekuwa tukisikia uwepo wa midahalo na mihadhala ya kitaaluma inayolenga uchumi na siasa na muungano ikifanyika ktk vyuo hasa chuo kikuu cha mlimani kiasi cha kukifanya chuo hicho na Mwanafunzi wake kuonekana bora na maarufu kuliko mahali pengine. Nataka kukubali kwamba ni sahihi kusema chuo hicho ni bora kwa ndicho pekee kimekuwa kikiorodheshwa kuwa miongoni mwa vyuo 50 bora vilivyopo Africa. Umaarufu huu hautokani tu na kuwa ndicho chuo kikuu cha kwanza kuwahi kuwepo nchini kwetu bali pia ni michango ya uendeshaji wa midahalo ya muhimu ktk chuo hicho tofauti na vyuo vingine. Kilichotokea uhasibu siku ya ijumaa ni mpango wa mungu, wagombea waliokuwa wanapewa sapoti na serikali inayomaliza mda wake walibwagwa kwa aibu ya karne kwa kuzidiwa kura takribani 400 kati ya wapiga kura 1500.wakati wale waliokuwa wanapewa sapoti na baadhi ya viongozi wa chuo wakiachwa nyuma kwa zaidi ya kura 200. Ushindi huu ni mwanzo mzuri kwa mapinduzi ya fikra kwa wanauhasibu wengi, kwani watakuwa na uwezo wa kuandaa midahalo na mihadhara mbalimbali ya siasa,uchumi na kijamii kiujumla kama ambavyo vyuo vingine hufanya na kuvifanya vyuo na Mwanafunzi wake kuonekana wenye dhamani miongoni mwa jamii ya kitanzania.
 

Forum statistics

Threads 1,274,147
Members 490,601
Posts 30,502,622