Prof. Safari: Nyumba za Serikali zitarudi

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Gazeti la RAI, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Profesa Abdallah Safari, alisema iwapo Chadema itakamata madaraka ya uongozi nchini, basi nyumba hizo zitarejeshwa kwa umma.
 
Hapo ndo utata ulipo. Siasa tu naona zinaendelea. Unarudishaje nyumba ambayo mtu ameshapitia milolongo yote ya kuimiliki kisheria? As much as I like politics, its too good to be real the way I see it. Mwisho wake ni kuwa disappoint wananchi kwa kushindwa kutimiza hiyo ilani pindi watakopopewa kura. Aidha kuliingiza taifa katika gharama zisizo za msingi za kuendesha kesi na kuburuzana mahakamani na wanaposhindwa kesi hawasemagi wanameza aibu yao.
 
Mikataba ya kisheria kutoka serikali halali, watu wamemaliza kulipa, hati wanazo, tunamsubiri kama ataweza
 
Kwani sheria huwa hazibadiliki? Wangapiwana hati kumbe feki? Ishu ni mchakato wa kuziuza ulikuwaje maana nyingizimeuzwa kimaghumashi ndio maana hawa sisiem hawataki kuondoka madarakani maanauozo walioufanya ni mkubwa hata kwenye hizo nyumba za serikali! Wanaogaopakibao kisije kikawageuka! Kwanza hao wenyewe walioziuza nanatakiwa kushitakiwa!

Maana huwezikuuza nyumba za serikali bila sababu zinazoeweleka. Niambie ni sababu zipi zamsingi walizowambia wananchi kwamba zinaifanya serikali ya Chama Cha Mafisadi(CCM)kuuza nyumba za serikali wakati hata hizo zilizokuwepo hazitoshi kwawatumishi wa serikali? Ni ufisadi tu wa kutaka kujimilkisha mali za umma wakatiwenye hizo mali ambao ni mimi na wewe na watanzania wengine wote hasa watumishiwa serilai tunaabika! Wamelewa madaraka maana huko ni kuopora nchi!
 
Magufuri hapa alichemka, manake unakuta Nyumba ipo kati kati ya kambi ya jeshi/magereza/polisi nayo iliuzwa, teh teh teh teh!
 
Hapo ndo utata ulipo. Siasa tu naona zinaendelea. Unarudishaje nyumba ambayo mtu ameshapitia milolongo yote ya kuimiliki kisheria? As much as I like politics, its too good to be real the way I see it. Mwisho wake ni kuwa disappoint wananchi kwa kushindwa kutimiza hiyo ilani pindi watakopopewa kura. Aidha kuliingiza taifa katika gharama zisizo za msingi za kuendesha kesi na kuburuzana mahakamani na wanaposhindwa kesi hawasemagi wanameza aibu yao.

sheria siyo msaafu, nawe unamiliki mojawapo?
 
Magufuri hapa alichemka, manake unakuta Nyumba ipo kati kati ya kambi ya jeshi/magereza/polisi nayo iliuzwa, teh teh teh teh!

kwenye Halmashauri za wilaya ndiyo vituko, unakuta nyumba zote ni za watu binafsi waliouziwa mpaka mkurugenzi anapanga nje ya eneo la halmashauri.
 
Hili linawezekana ngoja tusubiri muda ufike wote mliochukua nyumba hizo jipangaeni kuzirudisha
 
Magufuri hapa alichemka, manake unakuta Nyumba ipo kati kati ya kambi ya jeshi/magereza/polisi nayo iliuzwa, teh teh teh teh!
Magufuli chini ya Che Nkapa alichemka sana. Ni aibu watumishi wanakaa hotelini kwa sababu ya ujinga kama huu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
natamani sana hilo litokee..... kinachoniumiza kichwa ni HOW?
watawatimua wamiliki kama mbwa mwizi? au watawalipa hela waliyonunulia/watakayokuwa tayari kulipwa?
 
Walipouziwa waliuziwa na masharti mazito sana. Ndiyo maana wengine wakaziuza haraka haraka.

Ilikuwa inatakiwa wasiuze wala kufanya ujenzi hadi miaka kama 30 hivi (hapa sina uhakika) na sana sana wafanye matengenezo tu. Ila wengi walipuuza na kufanya tofauti kabisa. Hilo linajulikana sana na wengi watakuja kulia siku moja.
Hapo ndo utata ulipo. Siasa tu naona zinaendelea. Unarudishaje nyumba ambayo mtu ameshapitia milolongo yote ya kuimiliki kisheria? As much as I like politics, its too good to be real the way I see it. Mwisho wake ni kuwa disappoint wananchi kwa kushindwa kutimiza hiyo ilani pindi watakopopewa kura. Aidha kuliingiza taifa katika gharama zisizo za msingi za kuendesha kesi na kuburuzana mahakamani na wanaposhindwa kesi hawasemagi wanameza aibu yao.
 
nyumba za serikali lazima zirudishwe, nyumba ziliuzwa kwa bei ya kutupwa hivyo basi watarudishiwa hizo pesa walizonunulia kwa wakati huo, poleni sana, anzeni kujiandaa!
 
Nyumba ya mamilioni ya pesa inauzwa bei ya kutupa inauzwa bei chee wapi na wapi? mfano nyumba masaki iliuzwa milioni 30 wakati kiwanja tu kinauzwa zaidi ya milioni 500
 
Mkuu hekimatele
Usijipe imani ya kujidanganya, serikali ni ya wananchi, na ikiwa jambo lolote limetekelezwa bila ridhaa ya wananchi ni haki na rahisi sana kurudiwa utekelezaji kama ilivyokuwa awali, mifano IPO, hapa nchini na nchi za nje.
 
Alhamisi, Juni 06, 2013 06:44 Na Joe Beda

VIONGOZI na wananchi wanaoishi kwenye nyumba za Serikali zilizouzwa miaka kadhaa iliyopita wametahadharishwa kuwa, zitarejea mikononi mwa umma wakati wowote ule. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na RAI jijini Dar es Salaam wiki hii, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Profesa Abdallah Safari, alisema sula hilo kwa sasa linasubiri muda tu.

“Kwanza ieleweke kwamba viongozi hao hawakununua nyumba zile, bali waligawana tu. Hilo haliwezi kudumu miaka yote kwani halikufanyika kihalali,” alisema Profesa huyo msomi wa Sheria na na Lugha ya Kiswahili.

Alisema ugawanaji wa nyumba hizo kisheria unajulikana kama “inconsolable transaction” (ununuzi wa kidhalimu), kwani haukuzingatia thamani ya ardhi wala ya majengo yenyewe kwa sasa.

Profesa Safari alisema nyumba hizo zingeweza kurejeshwa mikononi mwa umma hata leo hii kwa kufuata taratibu za kisheria, lakini bahati mbaya waliopewa dhamana ya kutafsiri na kusimamia utekelezwaji wa sheria (majaji) nao baadhi yao waligawiwa nyumba hizo.

“Ni wazi iwapo Chadema tutakamata madaraka ya uongozi nchini, basi nyumba hizo zitarejeshwa kwa umma. Hilo ni moja kati ya mambo matatu niliyowaambia Chadema waliponiomba nijiunge na chama chao kuwa ningependa yasimamiwe kikamilifu,” alisema.

Sera ya uuzaji wa nyumba za Serikali ilifanyika wakati wa Awamu ya Tatu ya uongozi chini ya Rais Benjamin Mkapa na kusimamiwa kikamilifu na Waziri wa Miundombinu wa wakati huo, John Magufuli, ingawa ilipingwa na kulalamikiwa na watu wengi.

Nyumba hizo nyingi zilikuwa maeneo maarufu kama ‘uzunguni’ na zilijengwa wakati wa ukoloni na Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere maalumu kwa viongozi wa kiserikali.

Lakini kwa mshangao wa wengi, kwa sasa idadi kubwa ya nyumba hizo zipo mikononi mwa viongozi wengi wastaafu wa Awamu ya Tatu na wengine wa Awamu ya Nne wanaoelekea kustaafu huku, Magufuli akidai kuwa zitajengwa nyumba nyingine maeneo muafaka kama yale ya zamani.

Katika mahojiano, Profesa Safari pia alizungumzia tatizo la udini lililopo nchini kwa sasa, akisema nalo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

“Kwenye kikao changu na marehemu Bob Makani pomoja na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa) tulilizungumzia hili na nikawaomba waliweke kwenye sera za utekelezaji wa chama chetu.

“Suala la udini ni ‘hyper sensitive’ na lazima tukubali kuwa udini Tanzania upo! Upo na wala si kwetu tu, hili ni suala la kimataifa na tumelirithi kutoka kwa Wakoloni. Ni lazima tulitafutie ufumbuzi na nina amini Chadema italitatua hili,” alisema.

Profesa Safari ambaye pia ni mwanazuoni wa Kiisalamu, alivitaja vitabu kadhaa vinavyothibitisha udini nchini na kushauri Tanzania ijifunze kutoka Senegal namna walivyolitatua tatizo hilo na kuiepusha nchi yao kwenda mwelekeo wa Nigeria na nchi nyingine kadhaa.

Kweli tupu.
Alhamisi, Juni 06, 2013 06:44 Na Joe Beda

VIONGOZI na wananchi wanaoishi kwenye nyumba za Serikali zilizouzwa miaka kadhaa iliyopita wametahadharishwa kuwa, zitarejea mikononi mwa umma wakati wowote ule. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na RAI jijini Dar es Salaam wiki hii, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Profesa Abdallah Safari, alisema sula hilo kwa sasa linasubiri muda tu.

"Kwanza ieleweke kwamba viongozi hao hawakununua nyumba zile, bali waligawana tu. Hilo haliwezi kudumu miaka yote kwani halikufanyika kihalali," alisema Profesa huyo msomi wa Sheria na na Lugha ya Kiswahili.

Alisema ugawanaji wa nyumba hizo kisheria unajulikana kama "inconsolable transaction" (ununuzi wa kidhalimu), kwani haukuzingatia thamani ya ardhi wala ya majengo yenyewe kwa sasa.

Profesa Safari alisema nyumba hizo zingeweza kurejeshwa mikononi mwa umma hata leo hii kwa kufuata taratibu za kisheria, lakini bahati mbaya waliopewa dhamana ya kutafsiri na kusimamia utekelezwaji wa sheria (majaji) nao baadhi yao waligawiwa nyumba hizo.

"Ni wazi iwapo Chadema tutakamata madaraka ya uongozi nchini, basi nyumba hizo zitarejeshwa kwa umma. Hilo ni moja kati ya mambo matatu niliyowaambia Chadema waliponiomba nijiunge na chama chao kuwa ningependa yasimamiwe kikamilifu," alisema.

Sera ya uuzaji wa nyumba za Serikali ilifanyika wakati wa Awamu ya Tatu ya uongozi chini ya Rais Benjamin Mkapa na kusimamiwa kikamilifu na Waziri wa Miundombinu wa wakati huo, John Magufuli, ingawa ilipingwa na kulalamikiwa na watu wengi.

Nyumba hizo nyingi zilikuwa maeneo maarufu kama ‘uzunguni' na zilijengwa wakati wa ukoloni na Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere maalumu kwa viongozi wa kiserikali.

Lakini kwa mshangao wa wengi, kwa sasa idadi kubwa ya nyumba hizo zipo mikononi mwa viongozi wengi wastaafu wa Awamu ya Tatu na wengine wa Awamu ya Nne wanaoelekea kustaafu huku, Magufuli akidai kuwa zitajengwa nyumba nyingine maeneo muafaka kama yale ya zamani.

Katika mahojiano, Profesa Safari pia alizungumzia tatizo la udini lililopo nchini kwa sasa, akisema nalo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

"Kwenye kikao changu na marehemu Bob Makani pomoja na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa) tulilizungumzia hili na nikawaomba waliweke kwenye sera za utekelezaji wa chama chetu.

"Suala la udini ni ‘hyper sensitive' na lazima tukubali kuwa udini Tanzania upo! Upo na wala si kwetu tu, hili ni suala la kimataifa na tumelirithi kutoka kwa Wakoloni. Ni lazima tulitafutie ufumbuzi na nina amini Chadema italitatua hili," alisema.

Back
Top Bottom