Prof. Safari: Magufuli shujaa wa Afrika

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,485
54,855
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari amemfananisha Rais John Magufuli na Rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Congo (DRC), Patrice Lumumba kutokana na juhudi binafsi anazofanya kutetea rasilimali za nchi.

Wakati Profesa Safari akisema hayo, Mbunge wa Chambani, Yusuf Salim Hussein (CUF) amesema anamuunga mkono Rais Magufuli, kwani amejitoa mhanga kwa maslahi ya taifa. Aliwaambia wabunge vita hiyo ni ngumu na wanapaswa kumshukuru Rais bila ya kujali kama ni wa CCM, Chadema au CUF.

“Sisi si maadui, tuungane tuwe pamoja kwa maslahi ya taifa, tujiulize tunataka kwenda wapi, tusameheane na twende mbele kwani tukipasuka hatutafika,” alisema. Kwa upande wake, Profesa Safari alisema hayo ofisini kwake Dar es Salaam jana, alipotoa maoni yake juu ya agizo la Rais kutaka iundwe timu ya wataalamu kupitia upya sheria za madini nchini na kupelekwa bungeni ili zifanyiwe marekebisho.

“Ninampongeza Rais John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kutetea rasilimali za nchi. Anafanya kazi kama walivyokuwa wanafanya baadhi ya viongozi wazalendo barani Afrika ya kupigania haki za wananchi wao kufaidika na rasilimali za nchi,” alisema Profesa.

Alitoa mfano wa Patrice Lumumba, Kwame Nkrumah na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama viongozi waliojitolea kwa ajili ya wananchi wao. Alisema maamuzi anayoyafanya Rais yanasimama katika Kifungu cha Tisa (Kifungu Kidogo C) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho ya mwaka 2000, ambacho kinasisitiza kwamba utajiri wa Taifa uendelezwe, uhifadhiwe na kutumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine.

Profesa Safari aliwaomba Watanzania na wataalamu wa sheria za mikataba, kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais katika kutetea maslahi ya Taifa. “Nchi hii ina wanasheria wengi wazuri katika masuala ya madini na mikataba. Ninashauri watafutwe wataalamu hawa watakaokuwa sio wala rushwa ili wamsaidie Rais katika vita hii ya rasilimali,” aliongeza Profesa Safari.

Akizungumza kwa niaba ya wazee waliofika Ikulu kusikiliza ripoti ya Kamati ya pili ya kuchunguza mchanga wenye madini, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alielezea ujasiri unaofanywa na Rais Magufuli kuwa ni mfano wa kuigwa na Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais kutetea rasilimali.

Juzi Rais Magufuli alipokea ripoti ya Kamati ya Pili ya Madini ya kuangalia masuala ya kisheria na kiuchumi, ambapo ilionesha Serikali imekuwa ikipoteza mapato ya Sh trilioni 108.46 kutokana na udanganyifu, unaofanywa katika usafirishaji wa mchanga wa dhahabu ‘makinikia’ nje ya nchi katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi mwezi Machi 2017.

Wakati huo huo, Bunge linatarajiwa kutoa Azimio la kumuunga mkono Rais Magufuli kutokana na kazi nzuri, zilizofanywa na kamati mbili alizoziteua kuchunguza mchanga wa dhahabu (makinikia) zilizobaini wizi mkubwa, anaripoti Mgaya Kingoba kutoka Dodoma.

Wabunge wengi wakiwamo wa Kambi ya Upinzani, walisema jana kuwa wameikubali kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli katika suala la madini, ingawa wao walinyoosha kidole kwa Serikali ya CCM kuwa ilishindwa kuzuia wizi huo.

Wabunge wote waliochangia jana walitoa pongezi kwa Rais Magufuli kutokana na kazi nzuri ya kamati zake mbili; ya kwanza ya wataalamu wa jiolojia na kemia na ya pili ya wachumi na wanasheria, ambazo zimeibua wizi mkubwa uliofanywa na kampuni za uchimbaji madini.

Hata kabla ya kuanza kwa mjadala huo asubuhi, Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM), aliomba mwongozo wa Spika, kwa nini Bunge lisitoe Azimio la kumpongeza Dk Magufuli kwa kazi nzuri kuhusu makinikia.

Akijibu mwongozo huo, Spika Job Ndugai aliagiza Kamati ya Uongozi ikutane mara moja na baadaye kabla ya kusitisha shughuli za Bunge mchana, angetoa majibu ya kikao hicho alichoagiza kiongozwe na Mwenyekiti wa Bunge, Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM).

Kabla ya kusitisha kikao hicho saa saba mchana, Spika Ndugai alitangaza kuwa kikao kimeamua kuwa ni busara kutoa Azimio ili kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kulinda rasilimali za Taifa.

Alisema kwa maana hiyo azimio hilo litaandaliwa kwa kufuata Taratibu na Kanuni za Bunge na kuwasilishwa bungeni, lakini akaagiza, “Kwa mamlaka yangu ya Spika, liwasilishwe kesho (leo) bila kuchelewa.”

Katika mjadala wa bajeti, Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajab (CCM) alisema Bunge lichukue hatua kuhakikisha kiwanda cha kuchenjua dhahabu kinaanzishwa nchini ili kumuunga mkono Rais Magufuli, ikiwamo kuifumua bajeti ili kutenga fedha za kiwanda hicho.

Akaongeza, “Tumeibiwa sana, never, never, never again (kamwe isijirudie). Tuhakikishe fedha zetu zinarudi, wakikataa tuwashitaki,” alieleza Balozi Adadi. Kwa upande wake, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) alisema wananchi wa jimbo lake wanafahamu madhira yaliyosababishwa na kampuni za madini, ikiwamo vifo vya binadamu na mifugo.

Alisema zipo pia rasilimali nyingine zinazoibwa hata katika maeneo ya utalii kama Loliondo. Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko (CCM), alisema Taifa limeibiwa sana na sasa basi,

Chanzo: Habari leo
 
Tatizo liko kwenye tabia.

Kwani mpinzani pekee nchi hii ni Mbowe tu?

Hata Mzee wetu marehemu Ndesamburo alikuwa muasisi wa upinzani nchi hii lakini hayakutokea haya mbona, Jibu ni kwamba aliheshimu SHERIA na taratibu za nchi yake maana upinzani siyo kuacha kuheshimu serikali iliyopo madarakani.


Mbowe aangalie alipokosea na siyo kusema anaonewa chuki, huko ni kutafuta huruma kwa watu wasiojielewa

Sheria gani amekiuka? Iweke hapa precisely siyo kkupiga ramli za kipumbavue kwa sababu tu umekaririshwa.

Hawa manyang'au wamefuata sheria? Sheria ipi inayowapa mamlaka ya kuharibu mali? Jibu bila hadhithi za kipumbavue!
 
FB_IMG_1497369581414.jpg
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom