Prof. Safari: Kuna haja ya kufungua kesi kuhoji uhalali wa Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari ameishauri CHADEMA kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya uhalali wa ubunge wa makada 19 wa chama hicho walioadhibiwa baada ya kwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum na kutotokea mbele ya Kamati Kuu kujieleza.

Wanachama hao, ambao ni pamoja na mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Halima Mdee waliapishwa Novemba 24 wakati kukiwa na utata wa barua iliyopelekwa Tume ya Uchaguzi (NEC) kuhusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum, baada ya katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika kusema hakuiandika wala Kamati Kuu haikukutana kupitisha orodha.

Kitendo hicho kiliifanya Chadema iwate mbele ya Kamati Kuu kujielezas, lakini wote hawakutokea na hivyo chombo hicho kufikia hatua ya kuwavua uanachama, lakini Spika Job Ndugai alisema hatatambua uamuzi huo aliodai wa kuonea wanawake baada ya kuhukumiwa bila ya kusikilizwa.

Nafasi za viti maalum ni za vyama ambavyo hupata zaidi ya asilimia tano ya kura za wabunge, tofauti na za ubunge wa jimbo ambazo hupatikana kutokana na vyama humdhamini mgombea.

“Kama wataenda bungeni, njia pekee ni kuomba tafsiri ya mahakama ili chombo hiki kiseme katika mazingira haya ibara ya 71 (1) f hawa ni wanachama halali,” alisema Profesa Safari, ambaye amebobea katika sheria.

Ibara hiyo ya katiba inasema mtu atapoteza ubunge iwapo “ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge”.

Profesa Safari, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema kuanzia 2014 hadi 2019, alisema kuna haja ya kufungua kesi kupata tafsiri kama Mdee na wenzake bado ni wabunge halali baada ya Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama.

“Mahakama ndiyo ina haki ya kutafsiri,” alisema.

Profesa Safari alisema suala la Mdee na wenzake kufukuzwa Chadema lipo wazi kwa mujibu wa ibara ya 71 (1) (f) ya Katiba ya jamhuri ya Muungano inayoeleza kuhusu mbunge kufukuzwa uanachama na pia sifa za kugombea zinazoelezwa katika ibara 67 (1)b, inayotaka mgombea ubunge apendekezwe na chama chake.

“Dhana ya kuwa na chama ni muhimu. Ukishatimuliwa huwezi ukakingikiwa kifua na mtu yeyote. Bahati nzuri matukio yametokea mara nyingi sana. Wakati wa Tanu walifukuzwa kina Anangisye, halafu wabunge wa CUF walitimuliwa. Mara nyingi tu (haya yanatokea),” alisema Safari.

Pia alielezwa kushangazwa na kitendo cha Spika kuwatetea makada hao akihoji wameanza urafiki lini.
 
Unafunguaje kesi katika mazingira kama haya? Prof. amechanganyikiwa?

87659087.jpg
5678901.jpg
 
Walivyokuwa wanafutwa wale wa CUF alishangilia Sana speaker. Wale walihitajika kulindwa zaidi kuliko Hawa wa safari hii. Sema kwakuwa tunaangalia matakwa yetu kwa wakati husika, basi speaker awe consistent kwenye maamuzi.

Aheshimu maamuzi ya vyama pia.
 
CDM tabu yote hii ya nini?? Maamuzi yenu ni kwamba mmeshawavua uanachama, kwanini mnateseka ?
Wananchi wameshawashitukia kwa taarifa yenu.

Ni heri mkubali tu mapema raia waanze kuzoea kulikoni mje mkubali mwishoni na vidonda havitapona (muwaruhusu hao covid19 sababu mlikubaliana wenyewe,msicheze na akili zetu)
 
Wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari ameishauri CHADEMA kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya uhalali wa ubunge wa makada 19 wa chama hicho walioadhibiwa baada ya kwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum na kutotokea mbele ya Kamati Kuu kujieleza...
Mahakama gani?

Suala la uchaguzi + covid-19 ni uhalifu wa Kidola ukiwa engineered na Jiwe.

Ni kama tukio la Lissu kupigwa risasi mchana kweupee.

Mnapoteza muda na raslimali.
 
Wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari ameishauri CHADEMA kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya uhalali wa ubunge wa makada 19 wa chama hicho walioadhibiwa baada ya kwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum na kutotokea mbele ya Kamati Kuu kujieleza...
Naunga mkono hoja ya Pr. Safari
Hii imekaa ki profesional zidi kuliko kelel za kisiasa majukwani na kwenye vyombo vya habari.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom