Prof. Safari: Huu ndio wakati muafaka wa kuendeleza maazimio ya oparesheni UKUTA

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,376
24,928
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa huu ni wakati muafaka wa kuendeleza maazimio ya UKUTA kwasababu waliyoyatabiri ndiyo yanayotokea sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari amesema lengo la UKUTA lilikuwa endelevu na lenye lengo la kukemea udikteta nyemelezi.

Alisema yale yaliyokuwa yakipingwa ndiyo yanajitokeza sasa, hivyo ni wakati wa kuuamsha kwa nguvu moja.

full_size_20170216160442.jpeg

Chanzo: Mwananchi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa huu ni wakati muafaka wa kuendeleza maazimio ya Ukuta kwa sababu waliyoyatabiri ndiyo yanayotokea sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari amesema lengo la ukuta lilikuwa endelevu nz lenye lengo la kukemea udikteta nyemelezi.

Alisema yale yaliyokuwa yakipingwa ndiyo yanajitokeza sasa, hivyo ni wakati wa kuuamsha kwa nguvu moja.

View attachment 471131 Chanzo : Mwananchi Online
Mwanzoni nilikuwa bado sijaamini kama kweli kuna udikteta, sasa nimeamini asilimia mia, kauli za kibabe juu ya wananchi ambao kimsingi ndiyo waajiri wake, kutopenda matajiri, kukandamiza watu, kukiuka katiba na sheria kuanzia yeye hadi wateule wake yani kiufupi nchi inaendeshwa kama familia ya mtu
 
Ngoja tuone kama itakuwa kweli au ndo uswahili wenu..........................
 
Tena sasahivi wala msijaribu vyombo vimeagizwa kuhangaika na wahuni kama hawa
 
Ukuta tena? Angalau mwanzo tulikuwa na balance ya kuacha getto lakini siku hizi hata msosi wa kesho hautabiriki, nitaweza kweli kushiriki?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa huu ni wakati muafaka wa kuendeleza maazimio ya Ukuta kwa sababu waliyoyatabiri ndiyo yanayotokea sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari amesema lengo la ukuta lilikuwa endelevu nz lenye lengo la kukemea udikteta nyemelezi.

Alisema yale yaliyokuwa yakipingwa ndiyo yanajitokeza sasa, hivyo ni wakati wa kuuamsha kwa nguvu moja.

View attachment 471131 Chanzo : Mwananchi Online
Sory mkuu hivi huyu prf safari ana undugu na mhogo mchungu yule muigizajj??
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa huu ni wakati muafaka wa kuendeleza maazimio ya Ukuta kwa sababu waliyoyatabiri ndiyo yanayotokea sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari amesema lengo la ukuta lilikuwa endelevu nz lenye lengo la kukemea udikteta nyemelezi.

Alisema yale yaliyokuwa yakipingwa ndiyo yanajitokeza sasa, hivyo ni wakati wa kuuamsha kwa nguvu moja.

View attachment 471131 Chanzo : Mwananchi Online

Na nilikuwa mmoja kati ya watu tuliopambana kutafuta kula za magufuli tukiwa pamoja na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa mwanza bwana magessa mlongo huyu jamaa basi tu alifanya kazi kubwa sana hadi majimbo yote ya ilemela na nyamagana kwenda ccm na kushawishi watu wampigie magufuli kula, tulikuwa tunamwandalia vikao katika maeneo mbalimbali kama buhongwa nyakato n.k

then anakuja kushawishi watu na wanabadilika hapohapo, mlongo ni kichwa hasa, lkn aliambulia kufukuzwa, juhudi zote hizo ilikuwa kuleta mtu ambae hatukutegemea kama atakuwa hivi ubabe, kupenda sifa, kutumia wateule wake kukandamiza watu, kuingilia mihimili mingine ya dola, bunge kudharauliwa, na mengine mengi tu, anasahau kwamba kulikuwa nautofauti wa kula 2800000 tu kati yake na upinzani,

kama hata mm mfia magufuli siyo ccm nimebadilika je ni wangapi watakuwa wamebadilika kwa sababu ya mwenendo mbaya wa huyu rais, manake hata vijijini watu wamechoka ukiunganisha na tatizo la fedha lililopo kwa wananchi hao hawataki kusikia jina magufuli kabisa ngoja tuone 2020 na kama patakuwa na uchaguzi huru na wa haki basi magufuli hawezi kushinda labda upinzani wakose mtu mwenye sifa na ambae hajazungukwa na wapiga dili wanaotegemea apite ili waje madili, imefika wakati watu tunaona lowassa alionewa kwa kashfa lukuki, lkn kama lowassa akiachana na watu wasioeleweka na ambao hawana sifa nzuri ktk jamii basi atashinda asubui tu,

ushauri wangu kwa cdm wahakikishe watu wote wanaomfuata lowassa wabaki wanachama wa kawaida tu ndani ya chama ili kuondoa taswira ya kwamba wanamfuata ili akipita wapige dili so watu wote wa aina hiyo wawekwe pembeni kabisa
 
Lazima tuungane kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vya siasa kupinga mfumo udikteta kwenye nchi yetu kwa nguvu zote.
Leo mmiliki wa JF Maxence Melo ana kesi mahakamani, Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe Lijuakali yupo gerezani, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema yupo mahabusu zaidi ya miezi mitatu kwa kesi ya maono. Yote yamesababishwa sheria kandamizi pamoja udikteta kwenye nchi yetu. Mtu mmoja kujiona yeye ana mamlaka yote.
kuendeleza maazimio ya Ukuta kwa sababu waliyoyatabiri ndiyo yanayotokea sasa.
 
Hivi yupo huyu prof, mwambie aanzie udikteta wa chama chake mwenyekiti kukaa miaka mingi na wao kupitisha jina la mgombea urais kwa maamuzi ya wakubwa
 
Lazima tuungane kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vya siasa kupinga mfumo udikteta kwenye nchi yetu kwa nguvu zote.
Leo mmiliki wa JF Maxence Melo ana kesi mahakamani, Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe Lijuakali yupo gerezani, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema yupo mahabusu zaidi ya miezi mitatu kwa kesi ya maono. Yote yamesababishwa sheria kandamizi pamoja udikteta kwenye nchi yetu. Mtu mmoja kujiona yeye ana mamlaka yote.
kuendeleza maazimio ya Ukuta kwa sababu waliyoyatabiri ndiyo yanayotokea sasa.
Jimbo la Kyela tuko tayari kwa UKUTA iwe mchana au usiku .
 
Back
Top Bottom