Prof. Safari awajibu wanazuoni wa kiislamu kuhusu DC

waliolaani chadema kumvua hijabu DC sioo Bakwata bali ni umoja wanazuoni ulioanzishwa mwaka jana,muhimu ni kuwa pande zote ziwe na subira
 
Well, Abdallah Safari, Kwanza ni msomi mkubwa wa ngazi ya Profesa, pili ni mwanasheria mzoefu, tatu ni mwanaharakati wa dini ya Kiislamu anayeipenda sana dini yake, nne ni mtu anayejiweza kiuchumi hasemi hivyo kwa sababu ya njaa kama wanavyofanya akina nani hii ambao ukimpa hela anasema cho chote. Kwa sababu hiyo, Waislamu wana kila sababu ya kumwani na kuzipuuza propaganda za ccm. Sisi sote ni watanzania kwanza, dini, makabila, kanda, rangi nk zije baadaye. Mungu ibariki na kuilinda Tanzania yetu.

sawa kabisa
 
namimi niungane nawengine kukupongeza prof! maanayake ule mjadala wa bakwata kunawatu wanaukomalia sana! safi kwakutoa elimu ya bure kwa bakwata! na wote wenye mawazo mgando kama hao!
 
kwa kweli sikufanya makosa kuichagua cdm, na kuipenda, kwani uwezo wa kuelewa na utendaji ni mkubwa mno.
thanx prof. sisi sote ni ndugu jamani, ndivyo tulivyozaliwa, tumesoma hivyo na tunafanya kazi hivyo, udini tusiuweke kati yetu.
 
well Prof. Safari kwani hili liko mahakamni ni bora tusubiri na tusikurupuke kuto hukumu kwa jambo ambalo limefanyika Igunga na wanaohukum wote wako Dar wamesoma/ kuona/kusikia tu kwenye vyanzo vya habari. hebu tuipe nafasi mahakama ifanye kazi maana hukumu zikitolewa sana zitzifanya kesi hii ifutwe maan itakuwa siyo halali
 
Waliomsikiliza Kibonde jana nasikia ametumia inshu hii kupakaza sana na kuifanya deal ya kisiasa akapigia sana debe ccm kupitia kipindi chake clouds pale. nimeona kwenye facebook wall ya mtu
 
Viongozi wa dini ya kiislamu kupitia taasisi mbili zilizotajwa hapo juu wameonyesha kukerwa na kitendo cha DC 'kuvuliwa sijui ni jalabibu ama ni mtandio katika kichwa cha mama wa kiislamu'. Hata mimi katika mazingira ya kawaida ningekerwa na tabia ya makamanda wale na naamini ingekuwa hivyo kwa kila mtu na viongozi wangu wa CDM ambao hujali sana mambo ya kijamii wangekuwa wa kwanza kuomba msamaha kwa niaba ya Chama.

Lakini katika hili naomba nitofautiane na viongozi wangu watukufu wa taasisi tajwa hapo juu. Kimsingi sasa hivi Igunga is political battle ground na mahala popote ambapo kuna mpambano waina yoyote sheria za kawaida huwa hazitawali bali kunakuwapo na sheria na taratibu ambazo zinaelekeza namna bora ya kutekeleza majukumu yetu.

Mkuu wa wilaya ya Igunga saa na wakati ule alikuwa ni mhalifu wa kijamii na alipaswa kushughulikiwa kwa namna ileile ya kiuhalifu. Bahati mbaya imetokea mama huyu aliyetakiwa kusimamia mpambano wa kisiasa wa vyama vya siasa, aliamua kuvaa daruga na kuingia uwanjani bila ya kibali na ruhusa ya refa na akaingilia upande wa goli la upinzani shughuli aliyopata anaijua mwenyewe na wapambe wake.

kujaribu kuingiza hoja ya uislamu kwa mama huyu ambaye alikuwa anavunja kanuni ya msingi ya kutoa haki haijarishi ni padri au sheik, au sista au mama wa kiislamu ni lazima ashughulikiwe kwa lugha ya kisiasa `ambayo ataielewa vizuri.

Kuvaa baibui, hijabu au kanzu, au nguo za usista na upadri ukaende kutenda ushetani utashughulikiwa kwa hasira za kishetani.Chadema walijitahidi kuzungumza lugha ambayo CCM na mama yule na mwajiri wake wangeielewa. Ni bahati mbaya kuwa tendo la muovu huyu limewafika vipofu wa maadili na sasa wamelivalia kanzu na kulibeba eti ni kukashifu uisilamu.

Ebu tumwogope Mungu, na tutende haki kwa kuzingatia imani zetu.CCM iliyopoteza dira inatupeleka pabaya inahubiri Tanzania isiyo na dini halafu inatugawa katika misingi ya imani zetu. Watanzania tumefika pahala pabaya ambapo mwizi anaulizwa dini yake kwanza na kama nikigundua ni mkrito mwenzangu nasema eti si mwizi, ukijua ni mwislamu unasema wanamuonea eti kwa sababu ya dini yake, jamani tunakwenda wapi? Jalabibu na uhalifu wa kisiasa vinahusiana nini? Uhalifu na imani vinahusiana namna gani?

Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padre aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusianao
Wenye masikio ya kusikia wamesikia.
 
hizi ni taasisi za ccm zilizoanzishwa baada ya uhuru.
1.uwt.
2.uvccm.
3.bakwata.
4jumuia ya wazazi.
5.sukita.
6.
7....................
baadhi ya taasisi hapo zimeshakufa zilizobaki ziko taaban kilichobaki ni mzazi ccm kufa kwani nayo iko icu.
taasisi zake zinatumika ki propaganda nyingfine hazina shida kwani matumizi mabaya yanaiathiri ccm yenyewe ila hii bakwata ni hatari sana kwani imeshikilia imani za watu wakati huohuo ikifanya shughuli za kisiasa.hatari iliyoje na waislamu wanaiona na wanakaa kimya.

katika makosa ya wazi bakwata iliyofanya ni hili.
ilitangaza wazi kuwa mwenye mamlaka ya kutangaza kuonekana kwa mwezi ni shehe mkuu.
haya mafundisho bakwata imeyapata wapi?
mtume alisema mtu yeyote akiuona mwezi kwa ushahidi wa watu wengine watatu basi ni halali kufungulia na kesho yake ni idd.
sasa bakwata wamepata wapi mamlaka ya kumteua shehe mkuu kuwa msemaji kwa jambo ambalo mtume ameliweka wazi?
ndugu waislam hawa watu ni wanafiki na hatari hata kwa uislam.
uganda hata kenya hatujawahi kusikia wakiwa na migongano kama hii ya kwetu,tuamke tuiambie ccm mambo ya waislamu yaendeshwa na kuamuliwa na waislamu kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu.
abdala safari ameeleweka vizuri naomba tuanzie hapo.
naomba tuelewe kwama wakristo ni watanzania ila watanzania si wakristo.
na waislamu ni watanzania ila watanzania si waislamu.
hii ni nyumba yetu sote tusiruhusu mmoja kati yetu aichome nyumba yetu kwa kisingizio cha kutetea kundi moja.
 
Haya wandugu naomba tujibu maswali yafuatayo:-

1.Katika purukushani za kumkamata muhalifu wa kike na ikatokea shanga,zikakatika,hijabu ikadondoka na saa ikapotea,kitendo hicho ni;
(a)shambulio la aibu
(b)utovu wa adabu wa mkamataji
(c)halali kwasababu bila hivyo vielelezo havitapatikana
(d)si halali kwasababu muhalifu mwanamke inabidi akamatwe na mwanamke na hayupo basi aachiwe'asepe'tu.

2.Polisi wa Tanzania ni wabovu kwa sababu;
(a)hawatumii akili bali hutii amri yoyote kutoka juu.
(b)wanapendelea chama tawala waziwazi.
(c)hawawapendi wapinzani.
(d)(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.



3.Kwa kuwahukumu chadema kuwa ni wahuni kabla ya kuwasikiliza Rajabu kiravu ni;
(a)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya uchaguzi.
(b)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya CCM.
(c)msimamizi mzuri wa maslahi ya chama tawala.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

4.DC asiye jua ratiba za kampeni zinazo fanyika wilayani kwake ni;

(a)mvivu anaye pokea mshahara asio ufanyia kazi.
(b)mbumbumbu tu wa kazi ya ukuu wa wilaya.
(c)mbabaishaji tu ambaye ni kielelezo cha ubaya wa kuteua watu kwasababu tu ya ukereketwa wao.
(d)mtu safi anaye fanikishwa matakwa ya chama tawala.

5.Waandishi na wachambuzi wanaoilaumu chadema kwa kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu;

(a)wanafanya kazi yao vizuri
(b)wanajipendekeza kwa ccm na watawala ili wapate safari na posho.
(c)hawajui walifanyaro kwasababu hawajasoma katiba ya nchi .
(d)mamluki wanao tumiwa na ccm kuvuruga upinzani.

6.Jukumu la kumkamata muhalifu ni la;
(a)polisi pekee.
(b)kila mwananchi.
(c)askari yoyote mwenye magwanda na silaha.
(d)vyama vya siasa.

7.Kama anaye paswa kumkamata muhalifu hataki yaani polisi wajibu wa mwananchi wa kawaida ni;

(a)kumwachia muhalifu aendelee kuvunja sheria.
(b)kumwachia muhalifu aende zake.
(c)kulalamika kwa polisi wale wale wasio taka kukamata.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

8.Wanao sababisha amani kuvurugika katika kampeni za uchaguzi hapa tanzania ni;

(a)polisi wasio taka kutenda haki.
(b)wasimamizi wa uchaguzi na wakuu wa wilaya.
(c)viongozi wa ngazi za juu wano amuru polisi kufanya wanavyo taka na siyo polisi walivyo ona inafaaa.
(d)waroho wa madaraka wanaopendelea ccm kwa makusudi kwa matarajio ya kupandishwa vyeo.


Toa hoja sio vihoja.
Mh. nimependa ulivyo dadavua hayo majukumu ya kila ahusikaye na kuisaidia government na CCM. Mwenye macho aambiwi tazama
...........................nadhani hata hao polisi wanajua makosa yao..but hakimu anayesikiliza kesi nina uhakika atakuwa mtu makini, bila kutumia siasa katika maamuzi yake. Tuzidi kuliombea taifa letu mema daima. Haiwezekani mvunja sheria akatetewa na dola na vyombo vyake, Jambo la aibu kabisa hili, au wanadhani waTZ wamelala. Imekula kwao. BAKWATA acheni unafiki, kuweni wakweli.............................................................................
.....................................................................................................................................................................
 
Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu bali kinasubiri uamuzi wa mahakama utakaoamua iwapo Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario alivuliwa hijabu kwa makusudi alipokamatwa na wafuasi wa chama hicho.

Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (HAY AT) kukitaka chama hicho kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitaha yake na hivyo kumdhalilisha.

Akizungumza na wandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA Prof. Abdallah Safari alisema kuwa chama hicho hakiko tayari kujibizana na wanazuoni hao.

"Si vizuri kuzungumzia mambo ambayo yako mahakamani lakini mahakama itaamua kama DC Fatma alivuliwa hijabu na kama alivuliwa ni kwa makusudi gani, ni uamuzi wa mahakama pekee ndio utaokaomua," alisema Prof Safari.

Alisema kuwa Chadema haina sera ya udini kwa hiyo hakiwezi kushabikia mtu kuvuliwa hijabu kwa makusudi huku akionya viongozi wa dini kuacha kutoa taarifa zinazopotosha ukweli na zinazolenga kuvuruga mshikamano wa Watanzania.

Prof. Safari ambaye ni mwanasheria na mwanazuoni wa kiisalamu, alisema kauli hizo zina lengo la kufarakanisha umma wa waislamu na chama hicho ambacho kinalengo la kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kunuka ufisadi wa CCM

Helkopta kukata anga

Wakati huo huo Chadema kinategemewa kuanza kutumia helkopta kurudia kampeni katika Kata zote 26, lengo likiwa ni kuwakumbusha wananchi na kuwahamasisha kukichagua chama hicho zikiwa zimebaki siku tisa kufika uchaguzi.

SOURCE:MAJIRA
Go on Proffessor!!Urais ndani ya Chadema unakutafuta!!!
 
Waliomsikiliza Kibonde jana nasikia ametumia inshu hii kupakaza sana na kuifanya deal ya kisiasa akapigia sana debe ccm kupitia kipindi chake clouds pale. nimeona kwenye facebook wall ya mtu

Huyu Kibonde ni wa kupuuzwa tu kwani inaelekea ule ugonjwa umeshagonga utosini sasa hana tofauti na chizi mwingine yoyote, siku si nyingi akiona jalala ataanza kuchekelea kujipatia mlo.Halafu mtu mwenyewe ni punga.
 
Chadema ni wadini sana and ni chama cha kikristo,thats why hakikubaliki mikoa ya pwani and zenji! Chadema wanawadharau sana waislamu,sijui kwanini?? Waislamu msikubali,komaeni hadi hawa WANAFIKI CHADEMA UNAFIKI UWAISHE!! Me nawashauri mfanye maandamano nchi nzima ya kuipinga chadema! Hawa cdm hawana adabu kabisa
 
Ndugu wanaJF anachosema Prof. Safari ni kweli kabisa, hawa wanazuoni wa kiislamu wanashabikia mambo wasoyajua au basi kama wakijitetea wakadai wanajua walifanyalo basi watuthibitishie kuwa wameungana na wenzao wa CCM na wako kwenye kampeni. Vinginevyo wanajiingiza kwenye mambo machafu yaani, kutumia udini kama kinga dhidi ya siasa, watanzania wengi tumeshajua kuwa CCM maji yakifika shingoni mbinu yao ni kutumia kinga za udini (ukiristu na uislamu)
Kinacho onekana hawa wana zuoni wanatumiwa kwa malengo fulani, lakini tukichunguza kwa makini si wanazuoni wote wenye mwelekeo wa hiyo BAKWATA!!!!!!!! Sioni kama kuna sababu ya kuwalaumu ua kulaumiana isiwe kama issue ya UDOM, kuwaingiza wailomo na wasiokuwemo!!!!!!!!
 
Mh. nimependa ulivyo dadavua hayo majukumu ya kila ahusikaye na kuisaidia government na CCM. Mwenye macho aambiwi tazama
...........................nadhani hata hao polisi wanajua makosa yao..but hakimu anayesikiliza kesi nina uhakika atakuwa mtu makini, bila kutumia siasa katika maamuzi yake. Tuzidi kuliombea taifa letu mema daima. Haiwezekani mvunja sheria akatetewa na dola na vyombo vyake, Jambo la aibu kabisa hili, au wanadhani waTZ wamelala. Imekula kwao. BAKWATA acheni unafiki, kuweni wakweli.............................................................................
.....................................................................................................................................................................

Tatizo bado kuna watanzania wachache ambao hali zao ni mbaya kupindukia wanaendelea kuing'ang'ania CCM,hii kitu ndio inaleta ugumu,chakufanya hapa ni kutoa elimu kwa watu kama hao na kuwaeleza hali halisi ya maisha.
 
Hawa Bakwata nafikiri uongozi wote unastahili kwenda motoni....Mbona hoja za msingi kama Umeme wa shida wamekaa kimya? Wameona Hijab ni issue.......Waislamu kazi mnayo tena kubwa na hii kitu inayoitwa Bakwata.
 
Chadema ni wadini sana and ni chama cha kikristo,thats why hakikubaliki mikoa ya pwani and zenji! Chadema wanawadharau sana waislamu,sijui kwanini?? Waislamu msikubali,komaeni hadi hawa WANAFIKI CHADEMA UNAFIKI UWAISHE!! Me nawashauri mfanye maandamano nchi nzima ya kuipinga chadema! Hawa cdm hawana adabu kabisa
Umekurupuka wapi wewe, umelalia mataputapu nini??????? Mada hapa si Uislamu wala Ukristo bali ni kumdharirisha Mkuu wa Wilaya wa Igunga Fatma Kimario!!!!!!!!!!!Wacha ushambenga!!!!
 
Chadema ni wadini sana and ni chama cha kikristo,thats why hakikubaliki mikoa ya pwani and zenji! Chadema wanawadharau sana waislamu,sijui kwanini?? Waislamu msikubali,komaeni hadi hawa WANAFIKI CHADEMA UNAFIKI UWAISHE!! Me nawashauri mfanye maandamano nchi nzima ya kuipinga chadema! Hawa cdm hawana adabu kabisa

Mwisho wa ubaya ni aibu.
 
Mzee hata kiswahili kinakusumbua,kweli we ni chadema!! Sio kudharirisha ni kudhalilisha!! Ndo mnataka kuongoza nchi nyinyi na umbumbumbu huu
Umekurupuka wapi wewe, umelalia mataputapu nini??????? Mada hapa si Uislamu wala Ukristo bali ni kumdharirisha Mkuu wa Wilaya wa Igunga Fatma Kimario!!!!!!!!!!!Wacha ushambenga!!!!
 
viongozi wa dini ya kiislamu kupitia taasisi mbili zilizotajwa hapo juu wameonyesha kukerwa na kitendo cha dc 'kuvuliwa sijui ni jalabibu ama ni mtandio katika kichwa cha mama wa kiislamu'. Hata mimi katika mazingira ya kawaida ningekerwa na tabia ya makamanda wale na naamini ingekuwa hivyo kwa kila mtu na viongozi wangu wa cdm ambao hujali sana mambo ya kijamii wangekuwa wa kwanza kuomba msamaha kwa niaba ya chama. Lakini katika hili naomba nitofautiane na viongozi wangu watukufu wa taasisi tajwa hapo juu. Kimsingi sasa hivi igunga is political battle ground na mahala popote ambapo kuna mpambano waina yoyote sheria za kawaida huwa hazitawali bali kunakuwapo na sheria na taratibu ambazo zinaelekeza namna bora ya kutekeleza majukumu yetu. Mkuu wa wilaya ya igunga saa na wakati ule alikuwa ni mhalifu wa kijamii na alipaswa kushughulikiwa kwa namna ileile ya kiuhalifu. Bahati mbaya imetokea mama huyu aliyetakiwa kusimamia mpambano wa kisiasa wa vyama vya siasa, aliamua kuvaa daruga na kuingia uwanjani bila ya kibali na ruhusa ya refa na akaingilia upande wa goli la upinzani shughuli aliyopata anaijua mwenyewe na wapambe wake. Kujaribu kuingiza hoja ya uislamu kwa mama huyu ambaye alikuwa anavunja kanuni ya msingi ya kutoa haki haijarishi ni padri au sheik, au sista au mama wa kiislamu ni lazima ashughulikiwe kwa lugha ya kisiasa `ambayo ataielewa vizuri. Kuvaa baibui, hijabu au kanzu, au nguo za usista na upadri ukaende kutenda ushetani utashughulikiwa kwa hasira za kishetani.chadema walijitahidi kuzungumza lugha ambayo ccm na mama yule na mwajiri wake wangeielewa. Ni bahati mbaya kuwa tendo la muovu huyu limewafika vipofu wa maadili na sasa wamelivalia kanzu na kulibeba eti ni kukashifu uisilamu. Ebu tumwogope mungu, na tutende haki kwa kuzingatia imani zetu.ccm iliyopoteza dira inatupeleka pabaya inahubiri tanzania isiyo na dini halafu inatugawa katika misingi ya imani zetu. Watanzania tumefika pahala pabaya ambapo mwizi anaulizwa dini yake kwanza na kama nikigundua ni mkrito mwenzangu nasema eti si mwizi, ukijua ni mwislamu unasema wanamuonea eti kwa sababu ya dini yake, jamani tunakwenda wapi? Jalabibu na uhalifu wa kisiasa vinahusiana nini? Uhalifu na imani vinahusiana namna gani?ndugu zangu waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padre aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo dc yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa bakwata na basuta tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusianao
wewe kwa akili yako hiyo unaweza kumvua chupi hata mama yako mzazi
 
Back
Top Bottom