Prof. Safari awajibu wanazuoni wa kiislamu kuhusu DC

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu bali kinasubiri uamuzi wa mahakama utakaoamua iwapo Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario alivuliwa hijabu kwa makusudi alipokamatwa na wafuasi wa chama hicho.

Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (HAY AT) kukitaka chama hicho kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitaha yake na hivyo kumdhalilisha.

Akizungumza na wandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA Prof. Abdallah Safari alisema kuwa chama hicho hakiko tayari kujibizana na wanazuoni hao.

"Si vizuri kuzungumzia mambo ambayo yako mahakamani lakini mahakama itaamua kama DC Fatma alivuliwa hijabu na kama alivuliwa ni kwa makusudi gani, ni uamuzi wa mahakama pekee ndio utaokaomua," alisema Prof Safari.

Alisema kuwa Chadema haina sera ya udini kwa hiyo hakiwezi kushabikia mtu kuvuliwa hijabu kwa makusudi huku akionya viongozi wa dini kuacha kutoa taarifa zinazopotosha ukweli na zinazolenga kuvuruga mshikamano wa Watanzania.

Prof. Safari ambaye ni mwanasheria na mwanazuoni wa kiisalamu, alisema kauli hizo zina lengo la kufarakanisha umma wa waislamu na chama hicho ambacho kinalengo la kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kunuka ufisadi wa CCM

Helkopta kukata anga

Wakati huo huo Chadema kinategemewa kuanza kutumia helkopta kurudia kampeni katika Kata zote 26, lengo likiwa ni kuwakumbusha wananchi na kuwahamasisha kukichagua chama hicho zikiwa zimebaki siku tisa kufika uchaguzi.

SOURCE:MAJIRA
 
Saf sana,mm ni mwislam lakin kwa hil la DC kuvuliwa hijab cwez kulijadil ktk mising ya uislam na kuihusisha na chadema,huyu mama alikuwa mhalif,hata kama angevuliwa nguo zote alistahili..Bakwata siku zote hawapo kwajil ya waislam wapo kwajil ya maslah binafs ya serikal ya ccm,tena siwapend kupita kias,tena wanatumiwa na ccm kuvuruga waislam..chadema ipo kwajil ya watanzania wote na si kwajil ya wakristo.. Kwa hilo bakwata mmetokota
 
there you are prof.
 
Ni heri kuwa na Msomi mmoja mwenye uelewa kama Profesa Safari kuliko kuwa na Watu Elfu kumi Vibaraka kama Ephrahim Kibonde. Hata kama ingekuwa kweli DC alikwenda pale kama Kiongozi wa Dini, the way wanavyoshabikia issue hiyo na kuiweka kwenye hali ya udini ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa. Inapofika mahali, kutokana na Ukibaraka wake na kujipendekeza kwa CCM Kibonde eti anadai hata Waislam wataanza kuwavua nguo Masista(kana kwamba DC ambaye ni mvunja sheria ni kiongozi wa dini), hii inaonyesha upeo wake mdogo ambao unaweza kuwashawishi wenye upeo mdogo kama yeye kuanza kutekeleza hayo ambapo sidhani kama wenzetu Wakristo nao watakubali na mwisho wake kila mtu anaujua utakuwaje.

Zamani ndio nilikuwa najua kwamba Waathirika huwa wanaweza kuzungumza mambo ambayo hawakuyatarajia lakini si baada ya kupatikana kwa ARV's.
 
Ni kweli BAKWATA hawapo kwa ajili ya waislam,nakuunga mkono BAKWATA(BARAZA KUU LA WALAFI TANGANYIKA)
Saf sana,mm ni mwislam lakin kwa hil la DC kuvuliwa hijab cwez kulijadil ktk mising ya uislam na kuihusisha na chadema,huyu mama alikuwa mhalif,hata kama angevuliwa nguo zote alistahili..Bakwata siku zote hawapo kwajil ya waislam wapo kwajil ya maslah binafs ya serikal ya ccm,tena siwapend kupita kias,tena wanatumiwa na ccm kuvuruga waislam..chadema ipo kwajil ya watanzania wote na si kwajil ya wakristo.. Kwa hilo bakwata mmetokota
 
Saf sana,mm ni mwislam lakin kwa hil la DC kuvuliwa hijab cwez kulijadil ktk mising ya uislam na kuihusisha na chadema,huyu mama alikuwa mhalif,hata kama angevuliwa nguo zote alistahili..Bakwata siku zote hawapo kwajil ya waislam wapo kwajil ya maslah binafs ya serikal ya ccm,tena siwapend kupita kias,tena wanatumiwa na ccm kuvuruga waislam..chadema ipo kwajil ya watanzania wote na si kwajil ya wakristo.. Kwa hilo bakwata mmetokota

Tuko pamoja mkuu.
 
Ndugu wanaJF anachosema Prof. Safari ni kweli kabisa, hawa wanazuoni wa kiislamu wanashabikia mambo wasoyajua au basi kama wakijitetea wakadai wanajua walifanyalo basi watuthibitishie kuwa wameungana na wenzao wa CCM na wako kwenye kampeni. Vinginevyo wanajiingiza kwenye mambo machafu yaani, kutumia udini kama kinga dhidi ya siasa, watanzania wengi tumeshajua kuwa CCM maji yakifika shingoni mbinu yao ni kutumia kinga za udini (ukiristu na uislamu)
 
Viongozi wa dini ya kiislamu kupitia taasisi mbili zilizotajwa hapo juu wameonyesha kukerwa na kitendo cha DC 'kuvuliwa sijui ni jalabibu ama ni mtandio katika kichwa cha mama wa kiislamu'. Hata mimi katika mazingira ya kawaida ningekerwa na tabia ya makamanda wale na naamini ingekuwa hivyo kwa kila mtu na viongozi wangu wa CDM ambao hujali sana mambo ya kijamii wangekuwa wa kwanza kuomba msamaha kwa niaba ya Chama.

Lakini katika hili naomba nitofautiane na viongozi wangu watukufu wa taasisi tajwa hapo juu. Kimsingi sasa hivi Igunga is political battle ground na mahala popote ambapo kuna mpambano waina yoyote sheria za kawaida huwa hazitawali bali kunakuwapo na sheria na taratibu ambazo zinaelekeza namna bora ya kutekeleza majukumu yetu.

Mkuu wa wilaya ya Igunga saa na wakati ule alikuwa ni mhalifu wa kijamii na alipaswa kushughulikiwa kwa namna ileile ya kiuhalifu. Bahati mbaya imetokea mama huyu aliyetakiwa kusimamia mpambano wa kisiasa wa vyama vya siasa, aliamua kuvaa daruga na kuingia uwanjani bila ya kibali na ruhusa ya refa na akaingilia upande wa goli la upinzani shughuli aliyopata anaijua mwenyewe na wapambe wake.

kujaribu kuingiza hoja ya uislamu kwa mama huyu ambaye alikuwa anavunja kanuni ya msingi ya kutoa haki haijarishi ni padri au sheik, au sista au mama wa kiislamu ni lazima ashughulikiwe kwa lugha ya kisiasa `ambayo ataielewa vizuri.

Kuvaa baibui, hijabu au kanzu, au nguo za usista na upadri ukaende kutenda ushetani utashughulikiwa kwa hasira za kishetani.Chadema walijitahidi kuzungumza lugha ambayo CCM na mama yule na mwajiri wake wangeielewa. Ni bahati mbaya kuwa tendo la muovu huyu limewafika vipofu wa maadili na sasa wamelivalia kanzu na kulibeba eti ni kukashifu uisilamu.

Ebu tumwogope Mungu, na tutende haki kwa kuzingatia imani zetu.CCM iliyopoteza dira inatupeleka pabaya inahubiri Tanzania isiyo na dini halafu inatugawa katika misingi ya imani zetu. Watanzania tumefika pahala pabaya ambapo mwizi anaulizwa dini yake kwanza na kama nikigundua ni mkrito mwenzangu nasema eti si mwizi, ukijua ni mwislamu unasema wanamuonea eti kwa sababu ya dini yake, jamani tunakwenda wapi? Jalabibu na uhalifu wa kisiasa vinahusiana nini? Uhalifu na imani vinahusiana namna gani?

Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padre aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusianao
 
Well, Abdallah Safari, Kwanza ni msomi mkubwa wa ngazi ya Profesa, pili ni mwanasheria mzoefu, tatu ni mwanaharakati wa dini ya Kiislamu anayeipenda sana dini yake, nne ni mtu anayejiweza kiuchumi hasemi hivyo kwa sababu ya njaa kama wanavyofanya akina nani hii ambao ukimpa hela anasema cho chote. Kwa sababu hiyo, Waislamu wana kila sababu ya kumwani na kuzipuuza propaganda za ccm. Sisi sote ni watanzania kwanza, dini, makabila, kanda, rangi nk zije baadaye. Mungu ibariki na kuilinda Tanzania yetu.
 
Haya wandugu naomba tujibu maswali yafuatayo:-

1.Katika purukushani za kumkamata muhalifu wa kike na ikatokea shanga,zikakatika,hijabu ikadondoka na saa ikapotea,kitendo hicho ni;
(a)shambulio la aibu
(b)utovu wa adabu wa mkamataji
(c)halali kwasababu bila hivyo vielelezo havitapatikana
(d)si halali kwasababu muhalifu mwanamke inabidi akamatwe na mwanamke na hayupo basi aachiwe'asepe'tu.

2.Polisi wa Tanzania ni wabovu kwa sababu;
(a)hawatumii akili bali hutii amri yoyote kutoka juu.
(b)wanapendelea chama tawala waziwazi.
(c)hawawapendi wapinzani.
(d)(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

3.Kwa kuwahukumu chadema kuwa ni wahuni kabla ya kuwasikiliza Rajabu kiravu ni;
(a)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya uchaguzi.
(b)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya CCM.
(c)msimamizi mzuri wa maslahi ya chama tawala.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

4.DC asiye jua ratiba za kampeni zinazo fanyika wilayani kwake ni;

(a)mvivu anaye pokea mshahara asio ufanyia kazi.
(b)mbumbumbu tu wa kazi ya ukuu wa wilaya.
(c)mbabaishaji tu ambaye ni kielelezo cha ubaya wa kuteua watu kwasababu tu ya ukereketwa wao.
(d)mtu safi anaye fanikishwa matakwa ya chama tawala.

5.Waandishi na wachambuzi wanaoilaumu chadema kwa kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu;

(a)wanafanya kazi yao vizuri
(b)wanajipendekeza kwa ccm na watawala ili wapate safari na posho.
(c)hawajui walifanyaro kwasababu hawajasoma katiba ya nchi .
(d)mamluki wanao tumiwa na ccm kuvuruga upinzani.

6.Jukumu la kumkamata muhalifu ni la;
(a)polisi pekee.
(b)kila mwananchi.
(c)askari yoyote mwenye magwanda na silaha.
(d)vyama vya siasa.

7.Kama anaye paswa kumkamata muhalifu hataki yaani polisi wajibu wa mwananchi wa kawaida ni;

(a)kumwachia muhalifu aendelee kuvunja sheria.
(b)kumwachia muhalifu aende zake.
(c)kulalamika kwa polisi wale wale wasio taka kukamata.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

8.Wanao sababisha amani kuvurugika katika kampeni za uchaguzi hapa tanzania ni;

(a)polisi wasio taka kutenda haki.
(b)wasimamizi wa uchaguzi na wakuu wa wilaya.
(c)viongozi wa ngazi za juu wano amuru polisi kufanya wanavyo taka na siyo polisi walivyo ona inafaaa.
(d)waroho wa madaraka wanaopendelea ccm kwa makusudi kwa matarajio ya kupandishwa vyeo.

Toa hoja sio vihoja.
 
Prof Safari wakati uko huko Igunga Jaribu kuomba utoe daawa kwa viongozi wa Misikiti na Waislaam wote uhatari wa kufanywa Makasuku kwa Waislam na wanasiasa
 
Ndio Prof. Umenena vema. Watanzania tunatakiwa kuwa makini sana na watu/viongozi wanaotaka kutumia dini kugawa watanzania. Tunatakiwa kuwakataa kwa nguvu wachozezi wote.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom