Prof. Safari ajiunga CHADEMA; akabidhiwa kadi rasmi leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Safari ajiunga CHADEMA; akabidhiwa kadi rasmi leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Apr 1, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Prof. Safari kajiunga RASMI na CHADEMA na hivi sasa yupo Live anajaribu kutoa ufafanuzi wa kwanini kajiunga CHADEMA.

  Tutaendelea kujuzana kinachoendelea, fuatilia updates hapa chini:

  =============
  UPDATES:

  1) Kuna mvua sana jijini Dar, vyombo vya habari kadhaa vimeomba kupewa muda walau ili waandishi waweze kuwasili. Ieleweke kuwa HABARI HII bado itakuwa TETESI, jina na nani anahamia CHADEMA tutafahamu baadae.

  2) We are now LIVE. Mvua nafahamishwa imepungua jijini Dar

  3) Sasa anaongea Dr. Slaa, anamkaribisha rasmi Prof. Safari na anamkabidhi katiba ya CHADEMA

  4) Baada ya kutoka CUF nilitafakari kwa kina, nilishauriwa kuandika vitabu. Mke wangu na wanangu tumetafakari na tukafikia muafaka! - Prof. Safari

  5) Kuna masuala matatu muhimu ambayo si ya kufumbia macho; suala la ununuzi wa nyumba za serikali, analitolea ufafanuzi. Kuna suala la UKANDA, nalo analitolea ufafanuzi. Na kuna suala la UDINI ambalo pia anajaribu kulitolea ufafanuzi kwa mapana kwa kuangalia historia tangu uhuru wa Tanganyika na ule wa Zanzibar - Prof. Safari

  6) Anawashangaa waislam wanaoburuzwa na wadini kuendekeza udini na anadai kinachosisitizwa katika uislam ni uadilifu. Anasema CCM wametumia fursa hii kujaribu kuuvuruga upinzani hasa wanapoona chama cha upinzani wanapoona kinakuwa na nguvu. Walianzia CUF kwa kudai ni chama cha waislam na sasa wanadai CHADEMA ni chama cha wakatoliki - Prof. Safari

  7) Tumepewa vitu tulivyo navyo Tanzania ili vitunufaishe sote si wachache tu- Prof. Safari

  8) Saa ya Ukombozi imefika sasa! Tujiunge na CHADEMA kuleta ukombozi huo - Prof. Safari

  MUDA WA MASWALI NA MAJIBU:

  Bahati mbaya sisikii vema maswali, majibu nitayaweka hapa.

  Kwanini anayaongelea yanayohusu ufisadi baada ya kujiunga CHADEMA? Ni propaganda za kisiasa au aelewekeje?

  - Nyumba za serikali anapendekeza twende mahakamani lakini anasikitika majaji wengi wameshanunuliwa! Anasema njia nyingine itumike falsafa ya People's Power. Hoja ya kuuzwa nyumba za serikali haikupita bungeni na ni haramu
  - Slaa anaongezea kuwa kati ya vitu ambavyo CHADEMA ingefanya within 100 days ingepewa madaraka ingerejesha nyumba hizo kwakuwa ilikuwa ni batili.

  - Anasema kitu kibaya ni kibaya, haijalishi upo CHADEMA ama CUF si propaganda.
  - Mbowe anaongelea kuwa kazi ya uamsho imefanyika Kanda ya Ziwa tu, si kama Zanzibar haijafikiriwa na wala Prof hajaja kwa ajili ya hili, suala si kujenga ukanda bali kujenga taifa. Rukwa bado, Kilimanjaro wala Arusha bado hivyo Lindi watafika na hata Zanzibar
  - Mbowe anasema kwanza wanamkaribisha Prof. ndani ya chama na wanaamini ni mtu muhimu na ana historia safi. Masuala mengine ya kiuongozi yatafuatia baada ya vikao vya chama vya kimaamuzi kufanyika

  - Anaulizwa kadi ya CUF ataiweka wapi? Kasema technically ndani ya CUF kama hutoi michango maanake umeshajiondoa rasmi na alishatoa taarifa CUF kuwa kaachana nao. Kasema wakiihitaji atawapelekea.

  - Anafafanua juu ya CCM kutumia UDINI kuwagawa watanzania, anasema hawana utofauti na wakoloni walivyotumia mbinu za kuwagawa waafrika ili kuwatawala

  - Dr. Slaa anasema yeye binafsi anayo kadi ya CCM kwakuwa aliinunua na wala si mali ya Makamba, hajairudisha na wala hawapi kamwe!

  - Prof. Safari anahitimisha kwa kuwakaribisha wanasiasa wengine MAKINI kuhamia CHADEMA kwani ndicho chama makini na anasisitiza wale MAKINI TU.

  MWISHO

  ====================

  WASIFU WA PROF. SAFARI:


  KUZALIWA (UMRI):

  Profesa Safari alizaliwa June 3, 1951.

  ELIMU YAKE:

  1972- Secondari,
  1979- University of Dar es salaam shahada ya sheria (LLB),
  1985- Masters (LLM),
  1995- (PhD) University of Sussex England. Baada ya kupata shahada hiyo alibaki England akawa anafundisha,
  2000- Alitunukiwa u Profesa.

  UZOEFU WA KAZI

  1972-1974 Matafiti msaidizi katika taasisi ya Institutes of Kiswahili Research
  1974-1976 Mhariri katika kampuni ya Tanzania Publishing House
  1979-1986 Wakili wa serikali katika wizara ya sheria
  1988-1991 Afisa Mtafiti na uchapishaji katika kituo cha Uhisiano wa nje kisha Mhadhiri mwandamizi wa sheria katika kituo hicho Nyadhifa (Vyeo) alivyowahi kushika;
  1978-1986 Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  1982-1984 Mhadhiri wa sheria university of Dar es Salaam
  1983-1986 Mkuu wa Kitengo cha sheria, wizara ya sheria
  1984-1986 Mwakilishi wa wizara ya sheria katika baraza la elimu ya sheria Afrika Mashariki
  1990-1991 Kaimu Mkurugenzi wa masomo na program katika kituo cha mahusiano ya kimataifa
  1996-Hadi sasa, Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA), pia Mkurugenzi wa Masomo na programu wa kituo cha uhusiano wa Kimataifa
  1999-Hadi sasa, Katibu Mkuu wa Tanzania Center for Conflict Resolution, pia Mkurugenzi wa bodi ya hakimiliki (COSOTA)

  Makongamano:
  1978-Alihudhuria mikutano kadhaa ya Kimataifa kuhusiana na mambo ya sheria barani Afrika huko Nairobi (All African Law Students Association) Aidha,amewahi kuhudhuria makongamano mbalimbali yaliyohusu mambo ya sheria katika sehemu zifuatazo, Afrika Kusini, Sweden, Geneva, Botswana, Uganda na Marekani.

  Tuzo alizowahi kupata:
  1991-alitunukiwa tuzo iitwayo Ford Foundation Scholarship for Doctor of Philosophy programme
  1999-2001, Shaaban Robert Literary

  Maisha yake:
  Ameoa na ana watoto wawili.
   
 2. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Tunasubiri
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkutano na waandishi wa habari unakaribia kuanza. Sijui kuna nini, lakini tutawajulisha kila hatua.
   
 4. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  haya matangazo yanayo angukia APRIL fool's day yanatia mashaka, sijui tuyaamini au?
  MAANA hatuchelewi kusikia TAMKO kutoka kwa RAIS kwamba TUNAWALIPA DOWANS leo, mkipiga kelele wanasema ni APRIL FOOL's day mkikaa kimya wanalipa FASTA
   
 5. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kiroho kinanidunda! Lakini nawaamini makamanda wangu hapo...
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Safi, nafuatilia kwa karibu.

  Tetesi ni kuwa kuna mtu anajiunga rasmi CHADEMA leo
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Dakika nne bado tu hazijaisha?? Tunasubiri kwa hamu!!
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mod Umefuta Post Yangu

  Haya leta mambo
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Fools' day inaisha saa 4 mkuu. Dakika 5 zimeshapita, nafahamishwa waandishi kadhaa wapo eneo la tukio. Angalia last post hapo huu nilichodokeza
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  SItta??
   
 11. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Six au ?
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hii inanikumbusha sana siku hii:

  [​IMG]
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Invisible heshima zako hapa JF siku zote zimesimama sana hivyo chonde mambo ya fools day tuwaachie Michuzi Blog kuleeee!!!!
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Sidhani,

  Hajawa na ujasiri huo!
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Vipi mambo Bado?
   
 16. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cheche!!

  hamna kitu humu.

  ngoja nisubiri, maana siku hii unaweza kuambiwa Obama yuko Kwa-Mtogole
   
 17. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  No!! Riz 1.
   
 18. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nadhani dk 8 tayari...nimeshakaa mkao wa kula!
   
 19. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  mimi nimeshindwa kufanya kazi hadi nipate hii kitu. nasubiri hapa hapa na refresh page kila sekunde
   
 20. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #20
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Sasa mkuu ikiitishwa Press si kwanza zinaanza porojo kabla ya jambo lenyewe?

  Hint yangu ilikuwa clear, kuna mtu anahamia CHADEMA leo; muda si mrefu atatajwa na kukabidhiwa kadi yake ya CHADEMA. Najua waandishi humo ndani hawajui, I can bet that
   
Loading...