Uchaguzi 2020 Prof. Rwekaza Sympho Mukandala: Hatma ya CCM 2020 bado haijulikani

3 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Toka Mlimani City : mkutano wa Baraza Kuu wa Chadema:

Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA wamepiga kura kupendekeza nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapigia kura ifuatavyo :
Wajumbe 442 wa Baraza Kuu wapiga kura :
Matokeo: Tundu Lissu 405 , Lazaro Samuel Nyalandu 36 na Dr. Mayrose Kavura Majinge 1.
 
3 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Mkutano Wa Baraza Kuu - Chadema (Peter Msigwa, John Heche, Esther Bulaya, Halima Mdee)


Source : Jenerali online
 
Prof. Rwekaza S. Mukandala amehitimisha kuwa hajui hatima ya Magufuli na CCM Mpya itakuwaje 2020 wananchi wakiamua.
Hayo ni maneno yamkosaji,CCM inashinda sbh tu na mkandala akiangalia kwa macho yake yote mawili kama anayo!!!!!!
 
04 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

# LIVE : MKUTANO MKUU MAALUM WA CHADEMA KUELEKEA 2020


Kutoka ukumbi wa Mlimani City mkutano maalum wa CHADEMA umeketi na kutoa Ilani yake ya uchaguzi, kuthibitisha majina ya wagombea wa nafasi za uongozi wa kisiasa katika dola watakaoiwakilisha CHADEMA katika chaguzi za Jamhuri ya Muungano na zile za Serikali ya Zanzibar.
Source : JamiiForums
 
WAJUMBE WAHUSUDU BANGO LA TUNDU LISSU 2020, LIKIWEKWA KATIKA MKUTANO MKUU WA CHADEMA
Wajitokeza kwa wingi kupiga picha za ukumbusho

SOURCE : Swahili Villa
 
5 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Live : ACT-Wazalendo Ukumbi wa Diamond Jubilee


Magwiji Maalim Seif , Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Membe wakutana katika mkutano mkuu wa ACT Wazalendo
Kikosi Kazi hiki cha upinzani chenye mkakati kabambe kuelekea 2020, CCM Mpya kwisha habari yake
 
5 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Tundu Lissu - "Tanzania imepoteza ushawishi na marafiki, siyo tu wa EAC , bali SADC, AU-African Union , UN-United Nations".



Hayo yamesemwa katika hotuba ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee unapofanyika mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo.
 
05 August 2020
Nairobi , Kenya

Chadema na Lissu: Tundu Lissu kugombea Urais Tanzania dhidi ya Magufuli kwenye uchaguzi mwaka huu 2020



Source : KTN News Kenya
 
6 August 2020
Dodoma, Tanzania

RAIS MAGUFULI AMJIBU TUNDU LISSU "HATUWATAKI MABEBERU"



Magufuli akizungumza mbele ya wana CCM Mpya amekumbusha masuala mbalimbali aliyoyasimamia kwa ajili ya nchi na kusema ni bora kufa kwa kuitetea nchi yako maana tumechezea sana na mabeberu. Mfano madini yanachimbwa halafu yanatoroshwa, wanaenda kufaidi wengine ..

Magufuli akamsimamisha na kumshukuru Spika wa Bunge Spika Ndugai kwa kuunda Tume ya Madini na ripoti yake akaileta kwa serikali ..imetengenezwa sheria bora zaidi ya madini na sasa nchi inafaidika.

Magufuli ameonesha wasiwasi kuwa CCM Mpya ikiondoka wakaja wale wasio na rangi ya kijani nchi kweli itafaidika na Maendeleo haya tunayoyaona? Mh. Mafuguli anawahoji wanaCCM Mpya na kusema ndiyo maana potelea mbali nimeomba kugombea Urais kwa miaka mingine mitano.

Kutokana na kuiinua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye uchumi wa kati, CCM Mpya tumeleta Maendeleo ya Vitu kama maFlyover, ndege za cash 11 .....vitu tulivyokuwa tuona ona ulaya, mgombea wa CCM Urais Mh. Magufuli anawakumbusha wanaCCM Mpya.

Magufuli anawaambia WanaCCM Mpya tujiulize kwanini zamani Maendeleo haya ya Vitu hayakufanyika? Ni kwa sababu tumedhibiti vyanzo vya mapato zamani hawakuweza. Mwenyekiti na mgombea wa CCM anatia kibwagizo CCM Oyee! CCM Oyee, wapo watu ...


Tuna changamoto kwenye kilimo, mifugo na uvuvi amesema John Pombe Magufuli akiwaeleza sababu zake za kujitosa tena kugombea Urais.. wanaohoji Maendeleo ya Vitu kama yatawapatia kula (mlo) nina wasiwasi..mkiwapatia hao upinzani kura wakaongoza nchi basi Maendeleo ya Vitu kama ndege, meli watavipiga mnada...
Source : DarMpya TV
 
6 August 2020
Dodoma, Tanzania

LIVE : MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM MHE. RAIS DKT JOHN MAGUFULI AKICHUKUA FOMU OFISI ZA NEC DODOMA



Source : Wasafi media
 
21 Jun 2018
MSIGWA: "Simpongezi MAGUFULI, Serikali Imeleta maumivu makubwa kiuchumi, Pesa Hakuna" Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, akichangia hoja katika mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango.


MSIGWA: "Simpongezi MAGUFULI, Serikali Haina Adabu, Pesa Hakuna"
Hotuba ya Mch. Peter Msigwa iliyo bado imara hata baada ya miaka kupita ikihoji utendaji wa serikali zote za CCM ya awamu ya 4 na hii ya CCM Mpya awamu ya tano, kuwa haina sera madhubuti zenye muendelezo na hata mawaziri maprofesa hawana misimamo tukitazama walipokuwa wanatumikia awamu ya 4 na hii ya CCM Mpya ushauri wao huyumba hauna manufaa kwa nchi.

Source : Global TV online
 
7 August 2020
SALAMU KUTOKA CHADEMA KANDA YA KATI KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU 2020


Mikoa 3 : Dodoma, Singida, Morogoro, majimbo 29 ya ubunge, kata zaidi ya 500 za udiwani. Maandalizi 2020 ya kanda ya Kati wagombea majimbo yote 29 yana wagombea. Katika kata 559 wagombea udiwani wamejitokeza ktk kata zote 559. Kanda ya Kati pia imepata heshima ya kutoa mtia nia Urais 2020 kupitia tiketi ya CHADEMA.
Source : CHADEMA MEDIA TV
 
7 August 2020

SALAMU KUTOKA CHADEMA KANDA YA MAGHARIBI KATIKA MKUTANO MKUU 2020
Mikoa 3; Tabora, Katavi, Kigoma. Majimbo 23, Kata 403. Idadi ya wapiga kura kanda ya Magharibi kwa mujibu wa daftari la wapiga kura 2,105,000. Maandalizi uchaguzi 100% tayari.

Source : CHADEMA MEDIA TV
 
7 August 2020
SALAMU KUTOKA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI KATIKA MKUTANO MKUU
Mambo mwaka huu 2020 kutakuwa na makubwa angani na ardhini magari 125, cyber crew 200. Jeshi kubwa la wanawake jasiri wamejitokeza kuwania kuchaguliwa kupitia CHADEMA.


Source : CHADEMA MEDIA TV
 
CHADEMA KANDA YA NYASA WATOA UJUMBE MZITO KWA CCM MPYA



Majimbo 31 kanda ya Nyasa yasubiriwa kunyakuliwa na CHADEMA. Nguvu yetu ni ndani ya chama. Samaki akiwa nje ya maji si chochote ni sawa na David Silinde aliyejidanganya akiwa nje ya CHADEMA anatakuwa na nguvu.

Source: MbeyaYetuOnlineTV
 
Yohana : Mlango 10
38 lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.
 
Prof. Mukandala anasema haitoshi baba wa nyumba kuleta nyama, samaki na chakula kila siku nyumbani lakini familia yake inaishi bila furaha.


Nyama yenyewe ni nyama basi! mifupa tu, samaki- mapanki

Kurekebisha hataki kwani pambio nyingi zinaimbwa "uhimidiwe"
 
9 August 2020
Manyoni, Tanzania

Lissu asalimia waTanzania akielekea Singida
Amelazimika kufanya hivyo baada ya kuzuiliwa na wananchi ili angalau awasalimie

Source : CHADEMA MEDIA TV
 
Back
Top Bottom