Uchaguzi 2020 Prof. Rwekaza Sympho Mukandala: Hatma ya CCM 2020 bado haijulikani

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,263
24,140
Siasa na Utawala
Profesa Rwekaza Sympho Mukandala anazungumzia kigezo muhimu na kikubwa cha siasa na uongozi na kubaki madarakani kwa muda muafaka, Ni je wananchi wanafuraha?

Prof. Mukandala anasema haitoshi baba wa nyumba kuleta nyama, samaki na chakula kila siku nyumbani lakini familia yake inaishi bila furaha. Prof. Mukandala anataka utoe tathmini katika maeneo yao chini baada ya muhadhara wake na kutoa alama/ maksi juu ya utawala wa CCM


  • Kiongozi kuongoza kwa hiyari, kushawishi na siyo kushurutisha
  • Wakati wa janga kubwa kwa nchi, kiongozi kuwa mbele pamoja na wananchi kukabiliana na changamoto hiyo
  • Kukithiri kwa Umasikini wa watu
  • Maendeleo ya Vitu kuleta Umasikini ktk Maendeleo ya Watu
  • Ajira na Viwanda
  • Kilimo Kwanza na Masoko ya Kilimo , Mifugo, Uvuvi
  • Wananchi kukosa kushirikishwa ktk kipi ni kipau-mbele kwao maana serikali haitoi nafasi wananchi kusema
  • Sera za kiuchumi za serikali kukazania Maendeleo ya Vitu na kusahau kabisa Maendeleo ya Watu.
  • Utawala wa sheria
  • Uhuru wa Kujumuika na Kufanya Siasa
  • Kupiga vita rushwa
  • Kushindwa siasa za Ushawishi kubaki Siasa za Kushurutisha
  • Tanzania kuelewa diplomasia ya kujinafasi ki Geopolitics ktk majukumu kikanda / Kimataifa : SADC , EAC , Africa Union , United Nations, WHO, Benki ya Dunia World Bank, Fuko la Fedha IMF
  • Uwezo wa Mwenyekiti wa CCM kuzuia chama kisiwe na mpasuko si tu CCM Tanganyika na hata CCM Zanzibar kuelekea 2020

Kipimo cha kufanya vizuri CCM hakiwezi kupimwa kwa vile serikali yake imeweza kutengeneza miundombinu lukuki na kulazimisha watu waridhike wakati wananchi hawana furaha kutokana na ukata mifukoni mwao. Kipimo halisi ni hayo madokezo hapo juu.


Source :
25 Nov 2018
African Intellectuals : Prof. Rwekaza Mukandala - Hali ya Uchumi na Siasa Nchini Tanzania Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano: "Tunatoka wapi, Tuko wapi na Tunakwenda wapi"
 
Alisema ikifika 2020 hakutakuwa na upinzani, cha ajabu ndiyo kwanza BFF ake amekuwa ‘mpinzani’ Mbatia, wamewekana hadi kwenye speed dial.

Mwingine amekuwa ‘Waziri asiye rasmi wa Fedha na Mipango’. Habari mbaya za uchumi ambazo hawawezi kuzitaja wenyewe, wanampa huyo aziseme.
 
Sasa ya toka mwaka 2018 ndo unaileta leo!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Prof. Mukandala muhadhara wake aliangalia mbele mpaka 2020 kuona kama utawala huu wa CCM utaweza kujirekebisha 2018, 2019 na ghafla tupo 2020.

Body language ya vigogo wateule ktk muhadhara huo ulionesha kuna mapungufu kibao lakini ndiyo hivyo Mwenyekiti CCM na Katibu wa CCM waliona 2020 ni mbali pamoja ya Prof. kuwapa angalizo hajui hatima ya CCM Mpya 2020 kutokana na mapungufu mengi ktk tathmini.

Muda ni mchache na Vitu vingi utawala wa CCM umeshindwa kuvirekebisha au kufanya vizuri.
 
Back
Top Bottom