Prof. Palamagamba Kabudi atangaza Tanzania kuwa M/Kiti na mwenyeji wa mkutano 39, wa SADC

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,179
Wanabodi,
Niko hapa ukumbi wa JNCC, kuhudhuria press conference ya Waziri Kabudi.

Karibuni

Paskali.

UPDATE
Press Conference imeanza kwa intro kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.

Kwenye utambulisho,
Waziri Kabudi, amemtambulisha, Emanuel Buhohela ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari, Wizara ya Mambo ya Nje.

Pia Prof Kabudi, amejitambulisha kama mwandishi wa habari, na akawashukuru waalimu wake 4, waliomfundisha uandishi wa habari, ambao tuko nao hapa, hawa ni Wallece Maugo, James Mpinga, Richard Mngazija na Henri Muhanika.

Pia akataja waandishi wenzake kina Dr. Harison Mwakyembe, Dr. Mlimuka, wote walikuwa waandishi wakatimkia kwenye sheria.
 
P
 
Bila shaka Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa mwenyeji, Waziri wetu anapaswa kujua hilo.

Tumejipangaje kutumia fursa yakuwa wanachama wa SADC ili kuinua uchumi wetu?

Malawi, Zambia, Mozambique, Namibia, Botswana, Swazirland, South Africa, Angola ni nchi ambazo zina fursa nyingi sana ambazo tukizitumia vizuri tunaweza kuingiza fedha nyingi sana na kuwatengenezea watu wetu mzunguko mkubwa sana wa kibiashara..
 
Pia Prof Kabudi, amejitambulisha kama mwandishi wa habari, na akawashukuru waalimu wake 4, waliomfundisha uandishi wa habari, ambao tuko nao hapa, hawa ni Wallece Maugo, James Mpinga, Richard Mngazija na Henri Muhanika.

Pia akataja waandishi wenzake kina Dr. Harison Mwakyembe, Dr. Mlimuka, wote walikuwa waandishi wakatimkia kwenye sheria.

P
 
Kabudi anaendelea, kueeza umuhimu wa mkutano huu, hivyo ameviomba vyombo vya habari, kushiriki kikamilifu, kuutangaza mkutano huu.

P.
 
”Mwenda tezi na homo, marejeo ngamani” ni maneno ya Prof. Kabudi, hivyo media ya Tanzania ifanye uzalendo kwa kuvutia nyumbani.
P
 
Ni vyema tujitahidi sasa kuishi kwa faida ya watu wetu kama USA, kuwepo kwetu kwenye hizi jumuiya kuwe kwa faida ya watu wetu na sio kuishia kwenye makongamano, warsha, vikao nk.

Malawi, Zambia, Botswana ni land locked, hebu tutumie fursa yetu yakuwepo SADC kuboresha reli ya Tazara na kujenga KONTENA TERMINAL kubwa pale Tunduma na KONTENA zao zote zifike pale kupitia reli. Wanapoagiza mizigo yao kutoka Nje kupitia shirika lolote la Meli kuwe na Connection ya moja kwa moja KONTENA zipokelewe Tunduma na kila kitu kifanyikie pale na Dar es salaam port iwe transit port na pale Tunduma iwe destination port. Mizigo ya DRC hasa Katanga province yote itaishia kwenye hiyo terminal..

Hicho pia kinaweza fanyika Kigoma na Bukoba, Unajenga Kontena terminal kubwa na zinakuwa destination port kwa mizigo ya DRC hasa Kivu, Bukavu nk, Wanyarwanda na Waburundi pia watachukulia Kontena zao straight kwenye hizi terminal.

Miji ya MBEYA, TUNDUMA, KIGOMA NA BUKOBA Itkauwa Centre of business na mzunguko wake utakuwa mkubwa, kipato cha wakazi kitakwenda juu, watu watapata ajira nyingi, mikoa hiyo itaendelea kwa kasi, Dar es salaam Msongamano utapungua lakini pia Bandari itakuwa busy na mapato kuongezeka.. VERY SIMPLE IDEA TUJARIBU KUWA WABINAFI WA TAIFA LETU.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom