Prof. Nyagori: Rais Magufuli yuko sahihi kulinda raia wake, barakoa zinaweza kutumiwa na magaidi kusambaza virusi vya corona

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,736
2,000
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na yale nyemelezi katika taasisi ya Jakaya Kikwete Prof Nyagori amesema magaidi au watu wenye nia ovu wanaweza kutumia barakoa kusambaza virusi vya Corona.

Akihojiwa na Salim Kikeke wa BBC Prof Nyagori amesema kiongozi yoyote duniani mwenye nia ya dhati ya kulinda raia wake lazima atakuwa makini sana kwenye vitu kama barakoa hivyo Rais Magufuli yuko sahihi kabisa.

Suala ni kwamba watu wavae barakoa zinazoaminika, amesema.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia

Maendeleo hayana vyama!
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,820
2,000
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na yale nyemelezi katika taasisi ya Jakaya Kikwete Prof Nyagori amesema magaidi au watu wenye nia ovu wanaweza kutumia barakoa kusambaza virusi vya Corona...
Nchi inayoletewa mpaka Michele wa plastic toka China leo wanaogopa Barakoa.... Hizi propaganda za kijinga sijiu watu wanapata faida gani...!!
 

mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,533
2,000
Huyu Professor hospitali yake pale Morogoro ilifungiwa na NHIF. Nilisikitika sana, though sina uhakika kama imeshafunguliwa au bado.
Wewe ndo umekuja na majibu mazuri kwa nini prof anatema mashudu kumbe anatafuta njia ya kurudisha ugali wake uliomwagwa siku nyingi.

Hivi hawa wazungu kweli nia yao ni kutua waafrica kupitia barakoa kwa kuweka corona? mbona hata wazungu pia wanakufa, wao wamewekewa corona wapi? na nani kawawekea?

Hawa wazungu hawawezi kuweka corona kwenye condom, au vyandarua au hata kutuwekea kitu kibaya kwenye ARV? wamesubiri corona ndo watuwekee? hii corona kwani ilianzia kwa wazungu au ni kule kwa marafiki zetu wachina mbona tunawakwepa wachina?

baadae wanasema hii ni vita ya kiuchumi kwani sisi TZ tuna procudt sokoni
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,902
2,000
Kwenye condom na ARV vipi? Mabeberu hawawezi kuweka virus? Huyu professor Hana tofauti gani na darasa la Sana?
Virus vya corona ili viweze kuleta madhara lazima vipitie kwenye njia ya hewa kuyafikia mapafu. Ukiviweka kwenye condom havitaweza kuyafikia mapafu yako kupitia kwenye urethra au rectum yako. Natumaini umeelewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom