Prof. Ndulu: Maneno ya kiingereza ndio ya kitaalamu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Ndulu: Maneno ya kiingereza ndio ya kitaalamu?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kintiku, Feb 5, 2011.

 1. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwasikia watu wengi anapoongea kiswahili au lugha ya asili basi huweza kusema jambo hili kwa kitaalamu hujulikana kama..................hapo atataja neno hilo kwa kiingereza. Mimi nadhani sio sahihi kabisa zaidi ya ulimbukeni wa kasumba ya lugha ya kiingereza.

  Utasikia waandishi na watangazaji wakisema'' kitaalamu mipira kama hiyo huitwa ''dead balls'' au ''deflection'' au kitaaluma sehemu hiyo inajulikana kama '' impossible angle''

  Nimeamua kuandika baaada ya kuwaona hata watu wenye weledi wakitumbukia katika kadhia hiyo. Mfano, hivi karibuni Prof. Ndulu alikaririwa akisema hivi kuhusu noti mpya:''noti hizo mpya ni bora zaidi kuliko zile za zamani kwa kuwa zimewekewa dawa inayojulikana kitaalamu kama ‘Anti Soiling Treatment’ inayozuia zisichafuke au kuchanika kwa haraka''

  Hayo maneno siyo ya kitaalamu bali ni maneno ya kawaida kabisa ya kiingereza. Kwa mtazamo wangu tunatakiwa kusema '' kwa kitaalamu'' katika maneno ambayo ni istilahi; yaani hujulikana kwa watu wenye fani hiyo husika yaani mtu wa ''kawaida'' hawezi kuyaelewa: Mfano wataalamu wa kemia wana maneno yao, kadhalika fani ya utabibu ina maneno na procedures zake ambazo zinatumia maneno ambayo sio ya kawaida au watu wa Bailojia.
   
 2. P

  Paul S.S Verified User

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  u got point there
   
 3. b

  bulunga JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  yale yale, shule za kata zifundishwe kiswahili
   
 4. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unachosema ni sahihi mkuu, kitaalamu hiyo inaitwa ''good observation''
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hah hah hah.
   
 6. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Bongo ukiongea bila kuweka maneno ya kingereza unaonekana hujasoma.
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo una point ila kuwekana sawa naomba uelezee hayo maneno kwenye Bold ungependa waseme nini..., kuna wakati badala ya kutumia neno moja utajikuta unatumia sentensi nne lakini kwa watu wanaojua mpira ukisema "dead ball" wanaelewa moja kwa moja..

  Lakini "you have got a point mkuu" au kwa lugha ya kitaalamu "Hapo umenena"
   
 8. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,027
  Likes Received: 3,220
  Trophy Points: 280
  Huu uzi uliouanzisha kitaalam unaitwa thread ,loh
   
 9. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Voice of Reason,
  Nakubaliana kuna maneno ni ngumu kusema kwa ufupi kwa kiswahili, alipaswa kuondoa neno '' kwa kitaalamu inaitwa''......................... angesema noti hizo zimetengenezwa katika mfumo/njia inayojulikana kwa lugha ya kiingereza kama '' Anti Soil Treatment''
   
 10. N

  Nyafi Member

  #10
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko sawa kabisa mhe.:clap2:
   
Loading...