comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Waziri wa elimu , sayansi na teknolojia Prof Joyce Ndalichako amesema wataalamu wote walioshiriki kuchapisha vitabu vyenye makosa kimaudhui na kutumika katika taasisi za elimu kuwajibishwa, Prof Ndalichako alikua akijibu maswali bungeni baada ya wabunge kupigia kelele vitabu vvyenye makosa na kuendelea kutumika mashuleni, Aidha msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu elimu Mh Suzan Lyimo amemuomba Waziri Ndalichako kufanya uhakiki wa sifa kwa watendaji wote katika wizara ya elimu ili kujiridhisha sifa zao kama ni stahiki hasa baada ya kuendeleza makosa katika mitaala na vitabu hivyo kuzorotesha mfumo wa elimu, nae Mbunge Hussein Bashe ameomba kuwe na mitaala inayofanana nchini ili kuweka uwiano katika ubora wa elimu nchini.