Kinachonifanya niandike kwa uchungu ni shule hii kutumia mwavuli wa dini, mmiliki akitutangazia yeye AMEOKOKA huku matendo yake mimi na wazazi wengine wa hapa Dar na wa Dodoma nilikokuwa naishi, wengi tunaumia na tunaona tunaibiwa live. Dr Ngalichako nakuaminia najua utachukua hatua.
Ingekuwa shule ya Biashara haingeniuma hivyo ila hii inaniuma nikiwa kama Mluteri na shule kutumia jina la founder wa Kiluteri huku mmiliki amejenga kanisa kubwa na zuri kuliko yote Dodoma na Kuweka Msalaba mrefu kweli na kuwasha mwanga mwekunduu usiku ili kila anayeingia Dodoma toka Dar/Moro uushuhudie.
Ingekuwa shule ya Biashara haingeniuma hivyo ila hii inaniuma nikiwa kama Mluteri na shule kutumia jina la founder wa Kiluteri huku mmiliki amejenga kanisa kubwa na zuri kuliko yote Dodoma na Kuweka Msalaba mrefu kweli na kuwasha mwanga mwekunduu usiku ili kila anayeingia Dodoma toka Dar/Moro uushuhudie.
- Wanatudanganya wazazi na serikali, Shule hii inajulikana kama Martin Luther ipo Dodoma, ambayo kwa ndani kuna Martin Luther School na Martin Luther King, kwamba madarasa ya nyuma wanasoma kama Martin Luther na report zote mzazi utapokea kutoka Martin Luther School, wakati wa mitihani wa kitaifa, anachukua wanafunzi best 30, wanafanya kama Martin Luther na waliobaki wanafanya kama Martin Luther King. Ili wawe wa kwanza kiwilaya na mkoa, wakati king ni namba za mbali, ila references kwenye mikutano na matangazo tunaambiwa Martin Luther imekuwa ya Kwaaaanza. Halafu wazazi tunaambiwa Bw Yesu Asifiwe tunaitikia kwa sauti Ameeeeeeeeeeni. Mh waziri Mkuu Majaliwa, je unajua mwanao anasoma Martin Luther au Martin Luther King? Kama hatakuwa kati ya 30 Best, usije ukashangaa checti cha darasa la saba kimeandikwa Martin Luther King!
- Tunalazimishwa kununua vitu shuleni kwa bei ya ZAIDI sana ya bei ya kawaida, Soksi zinazouzwa Dodoma kwa 1,500 hadi 2,000, Dar tunapata hata kwa 1000, tumelazimishwa lazima zinunuliwe shuleni kwa 5,000/= eti kuna uiform ya soksi mwanzoni ilikuwa soksi nyupe tu ila wameona fulsa! Tracksuit inayouzwa 18,000 hadi 20,000 tunalazimishwa tununue kwa 30,000 Viatu vinavyopatikana kwa 20,000 tunalazimishwa kwa 30,000 Unapojiunga tu, unatakiwa utoe pesa ya usajili 230,000/= niulizieni hii ni ya nini???? Kujiunga watajitangaza weee, unachukua form kwa 20,000/= watoto say 500 tu watakusanya 10,000,000/=
Ada Martin Luther boarding 3M na Day ni 2.1M kuna watoto wa ndugu zangu Huko Dodoma St Fransis, Huruma Girls,Lwandai Ada zao hazizidi 1.8M na ni boarding, yaani chini ya ada ya day ya Martin Luther.
Shule ina Terms tatu, kila term hufungwa kwa AT LEAST WEEK 4, ya December kawaida week 6 (mwaka 2013 walifunga wiik 8) kwa maana hiyo wanafunga AT LEAST 3.5 MONTHS a Year. Kwa hivyo full saving pesa ya chakula. Kuna rafiki yupo Dodoma na anaumia sana, mtoto wake yupo Day na kanitumia ada zao
Michango ya mwanafunzi wa day
Ada ya Masomo 900,000
Usafiri 180,000 Ukiondoa weekend na 3 month on leave hii ni around 900/ kwa siku
Uji 90,000
Michezo ya Watoto 150,000 Sijawahi kuona enzi za Mwalimu na sitegemei kuona enzi za Magufuli
Chakula cha mchana 480,000 Kwa muda wa shule hii ni takriban 2500 kwa siku
Masomo ya jumamosi 300,000 (kwa idadi ya Jumamosi zisizozidi 36 ni Tsh 8,333/= kwa siku@Mtoto)
Jumla 2,100,000/= LIVE, (Hii ni day school, secondary nyingi boarding ni around 1.8
hapo hujalazimishwa kununua soksi 5000 kwao na Uniform zote ambako bei ni zaidi ya ile ya duka la Mangi halafu wazazi tunasalimiwa kwa Bwana Yesu Asifiwe!!! Wanafunzi zaidi ya 1400, chukulia wapo 1000X3000 faida ya soksi=3,000,000 kwa pair moja na pair zinatakiwa kadhaa!
Ada Kwa sisi wa Boarding ni 3M, yaani 2,100,000 kama ada ya Day, halafu unaongeza na ada ya masomo ambayo ni 900,000/=jumla 3M live, halafu unaongeza na Uniform kwa ujumla wake ni 400,000/=. Kama ni mgeni basi ongeza na 230,000 ya usajili (Zaidi wa wanafunzi 150 kwa mwaka wanajiunga, hivyo unaongelea kwa uchache sana 34,500,000/= za usajili tu.
Graduation iwe ya Kipaimara au ya Darasa la 7, mzazi lazima unalipishwa 220,000/= Hivi Mama Ndalichako niulizieni hizi pesa matumizi yake ni nini? Na unatakiwa ulipe January!
Mh Waziri, hii shule ni moja tu ya wanaogeuza huduma kuwa biashara tena ya kulazimisha, zipo nyingi za namna hii. Tunategemea sana serikali itasimamia tamko la kuweka ada/michango elekezi. Mtakuwa mmetutumbulia majipu toka kwenye nafsi zetu kwa kuwaelekeza wafanye huduma badala ya biashara
Ada na hasa Mihango elekezi inatakiwa isimamiwe kwa ukaribu sana.
Last edited by a moderator: