Prof. Ndalichako kwa matokeo haya ya kidato cha nne tumekusoma

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
620
1,000
Kila taifa linajukumu la kusimamia elimu. Elimu ya nchi hutegemea kwanza public schools. Private ni kwa sababu maalum tu lakini nchi haiwezi kuinuka kuelimika kwa kutegemea private kwakua kwao focus ni commodification ya elimu.

Matokeo ya mtihani wa form 4 yanatupa sura ya nini kinaendelea kwenye shule zetu za serikali. Shule zetu zinafelisha sana. Vijana wetu kweli wanasoma bure lakini huenda ni bure iliyoghali sana. Nimefuatilia hata huo ufaulu unaosemwa kupanda umechangiwa na kupanda ufaulu shule za private. Huu mwendo si mzuri.

Nasikitika kwamba hata shule zile tunazoita maalum zinashuka kila mwaka. Ajabu ni kwamba hatujasema shida iko wapi? Waziri hajategua kitendawili mbali ya kupita anazunguka na kukemea wajenzi. Haipendezi watoto wa watanzania masikini wanapotezewa muda wao hivi.

Najua Prof. Ndalichako na makamishna wa elimu wote wanasomesha watoto wao private. Wapishi ambao hawakiamini wanachokipika, wanapika lakini hawali, wanakula mapochopocho kwa jirani. Asante sana mama. Mnawaza muendelee kututawala wanyonge kwakua mnajua watoto wenu ndio watapata elimu bora na watatutawala tena na tena.

Naomba upate siku utuambie tatizo nini shule za serikali? unakuta shule yote div 1-3 hakuna. Wote ni zero na four, hii ni society suicidal kabisa.

Kama huwezi mama wape wenye maono ya maana. Kama wizara ni kubwa, omba usaidiwe. Usiishie kuwachimbia mkwara walimu wakati huna mbinu mpya umewapa. Hujatoa dira mpya, unapita mulemule business as usual.

Nangu Mandokwa
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,639
2,000
Hayo matokeo huwa siyaamini tangu nilipopata div 2 wakati kuna masomo nilikuwa nayamudu kiasi kwamba ukiulizwa swali ni sawa na kuulizwa kuandika jina lako,lakini cha ajabu eti unawekewa "C"Ni jambo linaloumiza sana
 

mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
4,048
2,000
Hayo matokeo huwa siyaamini tangu nilipopata div 2 wakati kuna masomo nilikuwa nayamudu kiasi kwamba ukiulizwa swali ni sawa na kuulizwa kuandika jina lako,lakini cha ajabu eti unawekewa "C"Ni jambo linaloumiza sana
Wewe ulikariri au ulimeza maswali. Halafu unawalaumu Necta.
 

ArD67

JF-Expert Member
Nov 14, 2016
2,821
2,000
Wewe ulikariri au ulimeza maswali. Halafu unawalaumu Necta.
Halafu hoja yake inakinzana na ya mleta mada, hayaamini, anamanisha yanapikwa. Kama ndivyo Nani ambaye angejipikia chakula kibaya? Naamini huyu hata leo akiletewa answer papers zake, ajisahihishie na ajilinganishe na walichokijibu wenzake kitaifa, angejipunguzia hata hiyo 2 to 4 kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom