City Hunter 1922
Member
- May 5, 2017
- 94
- 32
HATIMAYE: UONGOZI WA ST JOSEPH UNIVERSITY COLLEGE OF ENGINEERING AND TECHNOLOGY DAR ES SALAAM, WAMSIMAMISHA MASOMO RASMI RAISI WA SERIKALI YA WANAFUNZI (SOSJCET) 2017/18 NDUGU BACHUBILA HARUNA.
Wakati wa sakata la raisi wa serikali ya wanafunzi ndugu BACHUBILA HARUNA akiendelea kusimamia utekelezaji wa madai ya wanafunzi yaliyoandikwa kwenye WARAKA na serikali ya wanafunzi mwaka 2016/17 chuoni hapo iliyopelekea kusababisha mgomo ambao msuluhishi alikua waziri wa elimu, awamu ya 5, prof JOYCE NDALICHAKO, sasa limevaa sura mpya baada ya raisi huyu kusimamishwa masomo siku moja baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu kumjibu barua yake ya msingi.
Kutokana na kukosekana, kukandamizwa pamoja na kutokuwa na uhuru wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo imepelekea ndugu BACHUBILA HARUNA, katika kutimiza majukumu yake ya kila siku ya kudai na kutetea wanafunzi KUBAMBIKIWA mashitaka yasiyokuwa sahihi kulingana na nafasi aliyokuwa nayo ili mradi tuu, chuo kilinde maslahi yao ya kiutawala na kibiashara.
Mnamo tarehe 27/03/2017 raisi aliandika barua ofisi ya waziri wa elimu , ambayo kichwa chake kilikua kikisomeka hivi “ WARAKA KUTOKA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA MTAKATIFU JOSEPH LUGURUNI( KIBAMBA) TANZANIA”.
Baada ya hapo raisi aliitwa kwenye kamati ya maulizo( equiry committee) ambayo ilijumuisha wajumbe 8, ambapo mmoja alikuwa mwakilishi wa wanafunzi( waziri mkuu).Kamati hiyo ilimtuhumu kwa kosa la kuvunja sheria ndogo ya chuo( by laws) kifungu cha 10 kifungu kidogo cha 3, kisemacho :- “all official correspondence by students, officials of student organization or officials of recognized student societies to government ministries, parastatals, non-governmental organization and correspondence addressed to the higher authorities in the management, the state house representative of foreign government, international non- organizations or any other such official bodies shall be routed through the dean of students, the dean of faculty the principal or the vice chancellor as required.”
Ambapo mara baada ya kupata taarifa hiyo wahindi hao,tarehe 10/03/2017 walimlima barua kuwa amevunja sheria zao ndogondogo na anastahili adhabu ya kuvunja kifungu hiki( PENALTY) inapatikana katika hiyo by-laws , inasema “suspension for 3 working days with an apology in writing from the student and cancellation of scholarship”, ukurasa wa 60, kifungu cha 20 kifungu kidogo cha 4.Lakini alitengenezewa kesi mpya na kupewa barua nyingine tena iliyomtaarifu kuwa amevunja Kipengele 4.17 na 4.13 vya sheria zao ndogondogo.
Kifungu 4.17 kiliwekwa bila kutumia akili na weledi na kudhihirisha hilo kifungu hicho kinahusu kosa la kutuma taarifa isiyo sahihi au kutuma taarifa feki kwa lengo la kusababisha hasara.Adhabu ya kifungu hicho ni kufukuzwa chuo kwa mwaka mzima.
Wadau,Bachubila hakutuma taarifa isiyo ya kweli maana alikuwa anakumbushia utekelezaji wa maagizo yalitolewa na mamlaka za JMT juu ya matatizo yaliyomo kwenye waraka ulioandaliwa na serikali iliyomtangulia.Kusema kuwa ameforge taarifa ni uongo kwa mantiki hiyo.
Ina maana hawa wahindi wanamaanisha IKULU, WAZIRI MKUU NA WIZARA YA ELIMU YA JMT zilikuwa zinafanyia kazi taarifa zisizo sahihi? Na walivyo jeuri wamekata rufaa TCU wakidai waraka huo uliwaonea! Kwa nini leo?(NIMEAMBATANISHA DOCS ZOTE KWA REJEA- barua ya Rais kwa mamlaka husika, barua ya kwanza ya wahindi yenye shtaka moja, barua ya pili ya wahindi yenye kumtengenezea makosa na adhabu ya kumfukuza,barua ya kuitwa enquiry,recommendations za enquiry,barua aliyojibiwa juzi na Ofisi ya Waziri Mkuu wa JMT na mwisho barua ya wahindi waliyompa jana kumfukuza rasmi).
Lakini ukiangalia vizuri,hicho kipengele katika by-laws hizo zenye mapungufu mengi ndicho kinachotumiwa kunyima uhuru wa serikali ya wanafunzi ndani ya chuo hicho na kupelekea kushindwa kudai madai yao nje ya chuo kwa kutumia hiki kipengele ambacho ni kinyume na sheria ya toleo namba 178 la vyuo vikuu jamuhuri ya muungano wa Tanzania, inaeleza wazi mlezi atakua mshauri wa serikali ya wanafunzi lakini mlezi wa wanafunzi wa chuo hiki MR JAISON JACOB ambaye ni muajiriwa, mzawa kutoka India ndiye anayetumika vibaya kunyima uhuru wa serikali ya wanafunzi kwa kulinda maslahi ya muajiri wake ambaye ni chuo cha st joseph.
Ni dhahiri uongozi wa chuo, hauwezi kukubali ukweli wowote kutoka kwa wanafunzi utakao hafifisha na kuchafua biashara ile wanayoifanya hata kama ni ukweli na hakika ni lazima walinde masilahi yao kwa gharama yoyote ile ikikumbukwa kwamba mwaka wa masomo 2016/17 serikali ilikinyima chuo udahili uliopelekea kukosa mabilioni ya fedha na kupata hasara kubwa, kitu walichoona barua ya kukumbusha yale matakwa yatawafanya kukosa udahili wa masomo mwaka huu 2017/18 wa masomo.