Prof. Ndalichako Hujaambiwa Ukweli Kuhusu Usambazaji Vitabu Mashuleni..!

Midas Touch

Senior Member
Jan 23, 2008
186
198
  1. Kwanza nakupongeza sana Prof. wangu pale UDSM miaka ya 90s kwa kuteuliwa kati ya wengi kuiongoza Wizara ya Elimu. Pia nampongeza Dr. Magufuli kwa kukuteua.
  2. Nimesoma gazeti la Daily News la leo January 1, 2016 ukurasa wa kwanza na kuendelea uk. wa tatu kuhusu agizo lako ukiitaka TAASISI YA ELIMU TANZANIA vitabu VILIVYOIDHINISHWA vifikishwe mashuleni kabla ya tarehe 13/1/2016. Hili ni agizo zuri sana kuendana na kasi Mh. Rais Magufuli kuelekea ELIMU BORA na ya bure kwa maana hiyo. Peruzi kiambatanisho hapo chini,
  3. Kama Waziri wa Elimu, Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) hawajakupa habari kamili na za uhakika ili utoe maamuzi sahihi kuhusu hali ya vitabu na usambazaji wake.
  4. TIE hawana vitabu. Hata vile vya KKK darasa la I-II hawajakamilisha utayari wake ili vitumike mashuleni.
  5. Publishers/Wachapishaji ndio wenye vitabu vilivyoidhinishwa kuanzia chekechea hadi sekondari na vyuo vya elimu.
  6. Usambazaji vitabu mashuleni unafuata sheria ya manunuzi kupitia Government Procurement Services Agency (GPSA) kupitia wasambazaji walioidhinishwa (Authorized Booksellers/Distributors) na GPSA.
  7. Authorized Booksellers/Distributors wana mikataba hai na halali kati yao na GPSA (Hadi 2017) kuhusu usambazaji wa vitabu vilivyoidhinishwa vya Publishers/Wachapishaji katika shule na vyuo za/vya serikali. Kila mzabuni (Authorized Bookseller/Distributor) anayo orodha na bei ambatanishi kuhusu vitabu vilivyoidhinishwa vya Publishers/Wachapishaji vitakavyopelekwa mashuleni.
  8. TAMISEMI kitengo cha Elimu ndio kinachohusika na mpango mzima wa kusambaza vitabu mashuleni na vyuoni kwa mujibu wa sheria kupitia GPSA.
  9. TAMISEMI (Elimu) wanawasiliana na Publishers/Wachapishaji kupanga mkakati wa ununuzi wa vitabu na kisha usambazaji wake kupitia Authorized Booksellers/Distributors walioenea kila wilaya nchini. Unaweza kupata orodha ya Authorized Booksellers/Distributors kutoka GPSA. Mpangilio huu unaendana na sheria ya "Public Private Partnership (PPP) iliyopitishwa na Bunge letu hivi karibuni.
  10. Ni kweli kuwa TIE wanatakiwa kuandika vitabu vya shule, lakini itachukuwa muda mrefu sana kukamilisha shughuli hiyo kwa shule za chekechea, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu.
  11. Hata kama TIE itaandika vitabu vya shule na vyuo vya ualimu ili kuwa na mtizamo wa universal single textbook hapa Tanzania, kmantiki TIE itabaki kuwa Author tu kwani kazi iliyobaki itafanywa na Publishers (To publish), Printers (To print) na Distributors (To distribute). Ndivyo biashara ya vitabu inavyoendeshwa duniani kote. Hii inaendana na sheria ya PPP kawa nilivyoeleza hapo juu.
HITIMISHO
  1. Wahusika wanatakiwa wakupe mtiririko sahihi kuhusu hali ya vitabu nchini ili utoe uamuzi sahihi. Haiwezekani leo tarehe 1/1/2016 hadi 13/1/2016 vitabu viwe vimefika mashuleni. TIE hawana vitabu hivyo. Wakisema wanavyo, itakuwa miujiza..!
  2. Wewe ni Prof. tunakutakia kila la kheri katika Wizara ya Elimu na hatutasita kukupatia habari sahihi zaidi ili kufanikisha kazi yako kwa faida ya wote.
  3. Hadi leo sijaona ubaya wa MULTI TEXTBOOKS APPROACH TO SCHOOL TEXTBOOKS IN TANZANIA! Nimeisoma na kurudia tena, sijaona ubaya wake. Hii sera ilikuwa inalenga wanafunzi kusoma vitabu tofauti tofauti kwa somo lile lile ili kuongeza maarifa kutoka kwa waandishi tofauti. Silabasi ilisema kwamba, "Publisher to meet these minimum requirements" na kuorodhesha maelekezo ya uandishi wa kitabu cha somo husika na wizara ya elimu kukagua ubora na hatimaye kitabu kinapitishwa na Educational Materials Approval Committee (EMAC). EMAC ilikuwa ni kitengo cha wataalamu ndani ya wizara ya elimu wakishrikiana na stakeholders wengine nje ya wizara ya elimu. Mwanafunzi anaposoma kitabu kimoja tu kwa somo, hii inalenga kumpa mwanafunzi huyo ELIMU YA KASUKU, atakariri hadi kila ukurasa na kufaulu mtihani ingawa hatakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu somo husika. Baadhi ya watu WABAYA walidhalilisha sera ya MULTI TEXTBOOKS APPROACH kwa maslahi yao binafsi wakitumia MSEMO MBAYA kwamba, "Kila mwanafunzi anaamua kutumia kitabu chake tofauti wakati mtihani ni mmoja. Hii haikuwa kweli.
  4. Kuna taasisi kadhaa ndani ya wizara ya elimu zitakupatia wrong info. ili utoe maamuzi then you are misled.
  5. HAPPY NEW YEAR
 
Attachments

  • TIE TO DISTRIBUTE TEXTBOOKS BY JAN 13 2016.jpg
    TIE TO DISTRIBUTE TEXTBOOKS BY JAN 13 2016.jpg
    1.1 MB · Views: 34

Wewe huyo Ndalichako siyo Prof ni Dr. Jitahidi kuwa up to date!
 
MULTI TEXTBOOKS APPROACH TO SCHOOL TEXTBOOKS IN TANZANIA! Nimeisoma na kurudia tena, sijaona ubaya wake. Hii sera ilikuwa inalenga wanafunzi kusoma vitabu tofauti tofauti kwa somo lile lile ili kuongeza maarifa kutoka kwa waandishi tofauti. Silabasi ilisema kwamba, "Publisher to meet these minimum requirements" na kuorodhesha maelekezo ya uandishi wa kitabu cha somo husika na wizara ya elimu kukagua ubora na hatimaye kitabu kinapitishwa na Educational Materials Approval Committee (EMAC).
I concur with you kwamba hii sera haina ubaya "theoretically". However, is it appropriate in our current circumstances? Is it practical in situations that almost all students have no access to books? Unaishia kurudi pale pale kwamba the most a student can get is only one book (Even the teacher may not ha that copy!). Kwa hali hii, ni more practical kuwa na kitabu kimoja ambacho serikali inaweza kuhakikisha kipo kila shule na kila mwanafunzi na mwalimu atakuwa nacho. Ina mapungufu, lakini kwa hali ilivyo ndiyo appropriate.

Multi-textbook approach ni nzuri kwenye mazingira ya wenzetu ambapo shule zina maktaba, local councils zina maktaba, access to online resources ni possible na wazazi wana uwezo wa kununua vitabu zaidi ya kimoja kwa somo. Kukumbatia sera hii hapa Tanzania kumedidimiza elimu kwa walio wengi na kuwezesha wachache. Gap ya walionacho na wasionacho kielimu imekuwa kubwa sana.
 
Back
Top Bottom