Prof. Ndalichako Hujaambiwa Ukweli Kuhusu Usambazaji Vitabu Mashuleni..!

Midas Touch

Senior Member
Jan 23, 2008
186
198
  1. Kwanza nakupongeza sana Prof. wangu pale UDSM miaka ya 90s kwa kuteuliwa kati ya wengi kuiongoza Wizara ya Elimu. Pia nampongeza Dr. Magufuli kwa kukuteua.
  2. Nimesoma gazeti la Daily News la leo January 1, 2016 ukurasa wa kwanza na kuendelea uk. wa tatu kuhusu agizo lako ukiitaka TAASISI YA ELIMU TANZANIA vitabu VILIVYOIDHINISHWA vifikishwe mashuleni kabla ya tarehe 13/1/2016. Hili ni agizo zuri sana kuendana na kasi Mh. Rais Magufuli kuelekea ELIMU BORA na ya bure kwa maana hiyo. Peruzi kiambatanisho hapo chini,
  3. Kama Waziri wa Elimu, Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) hawajakupa habari kamili na za uhakika ili utoe maamuzi sahihi kuhusu hali ya vitabu na usambazaji wake.
  4. TIE hawana vitabu. Hata vile vya KKK darasa la I-II hawajakamilisha utayari wake ili vitumike mashuleni.
  5. Publishers/Wachapishaji ndio wenye vitabu vilivyoidhinishwa kuanzia chekechea hadi sekondari na vyuo vya elimu.
  6. Usambazaji vitabu mashuleni unafuata sheria ya manunuzi kupitia Government Procurement Services Agency (GPSA) kupitia wasambazaji walioidhinishwa (Authorized Booksellers/Distributors) na GPSA.
  7. Authorized Booksellers/Distributors wana mikataba hai na halali kati yao na GPSA (Hadi 2017) kuhusu usambazaji wa vitabu vilivyoidhinishwa vya Publishers/Wachapishaji katika shule na vyuo za/vya serikali. Kila mzabuni (Authorized Bookseller/Distributor) anayo orodha na bei ambatanishi kuhusu vitabu vilivyoidhinishwa vya Publishers/Wachapishaji vitakavyopelekwa mashuleni.
  8. TAMISEMI kitengo cha Elimu ndio kinachohusika na mpango mzima wa kusambaza vitabu mashuleni na vyuoni kwa mujibu wa sheria kupitia GPSA.
  9. TAMISEMI (Elimu) wanawasiliana na Publishers/Wachapishaji kupanga mkakati wa ununuzi wa vitabu na kisha usambazaji wake kupitia Authorized Booksellers/Distributors walioenea kila wilaya nchini. Unaweza kupata orodha ya Authorized Booksellers/Distributors kutoka GPSA. Mpangilio huu unaendana na sheria ya "Public Private Partnership (PPP) iliyopitishwa na Bunge letu hivi karibuni.
  10. Ni kweli kuwa TIE wanatakiwa kuandika vitabu vya shule, lakini itachukuwa muda mrefu sana kukamilisha shughuli hiyo kwa shule za chekechea, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu.
  11. Hata kama TIE itaandika vitabu vya shule na vyuo vya ualimu ili kuwa na mtizamo wa universal single textbook hapa Tanzania, kmantiki TIE itabaki kuwa Author tu kwani kazi iliyobaki itafanywa na Publishers (To publish), Printers (To print) na Distributors (To distribute). Ndivyo biashara ya vitabu inavyoendeshwa duniani kote. Hii inaendana na sheria ya PPP kawa nilivyoeleza hapo juu.
HITIMISHO
  1. Wahusika wanatakiwa wakupe mtiririko sahihi kuhusu hali ya vitabu nchini ili utoe uamuzi sahihi. Haiwezekani leo tarehe 1/1/2016 hadi 13/1/2016 vitabu viwe vimefika mashuleni. TIE hawana vitabu hivyo. Wakisema wanavyo, itakuwa miujiza..!
  2. Wewe ni Prof. tunakutakia kila la kheri katika Wizara ya Elimu na hatutasita kukupatia habari sahihi zaidi ili kufanikisha kazi yako kwa faida ya wote.
  3. Hadi leo sijaona ubaya wa MULTI TEXTBOOKS APPROACH TO SCHOOL TEXTBOOKS IN TANZANIA! Nimeisoma na kurudia tena, sijaona ubaya wake. Hii sera ilikuwa inalenga wanafunzi kusoma vitabu tofauti tofauti kwa somo lile lile ili kuongeza maarifa kutoka kwa waandishi tofauti. Silabasi ilisema kwamba, "Publisher to meet these minimum requirements" na kuorodhesha maelekezo ya uandishi wa kitabu cha somo husika na wizara ya elimu kukagua ubora na hatimaye kitabu kinapitishwa na Educational Materials Approval Committee (EMAC). EMAC ilikuwa ni kitengo cha wataalamu ndani ya wizara ya elimu wakishrikiana na stakeholders wengine nje ya wizara ya elimu. Mwanafunzi anaposoma kitabu kimoja tu kwa somo, hii inalenga kumpa mwanafunzi huyo ELIMU YA KASUKU, atakariri hadi kila ukurasa na kufaulu mtihani ingawa hatakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu somo husika. Baadhi ya watu WABAYA walidhalilisha sera ya MULTI TEXTBOOKS APPROACH kwa maslahi yao binafsi wakitumia MSEMO MBAYA kwamba, "Kila mwanafunzi anaamua kutumia kitabu chake tofauti wakati mtihani ni mmoja. Hii haikuwa kweli.
  4. Kuna taasisi kadhaa ndani ya wizara ya elimu zitakupatia wrong info. ili utoe maamuzi then you are misled.
  5. HAPPY NEW YEAR
 
Attachments

  • TIE TO DISTRIBUTE TEXTBOOKS BY JAN 13 2016.jpg
    TIE TO DISTRIBUTE TEXTBOOKS BY JAN 13 2016.jpg
    1.1 MB · Views: 24

SERIKALINI KUNAWANAFIKI WENGI WANACHUKI NA WASOMI WENGI WALIOTEULIWA NA MAGUFURI.WATAFANYA UWONGO NA ULAGHAI ILI KUHAKIKISHA WANACHEMSHA ILI WASEME.WASOMI WETU WAKUBWA HAWAJUI KAZI
 
Mbona sie tumesoma kwa kitabu kimoja na hatukuwa kama kasuku??Siungi mkono hoja yako kwa baadhi ya vipengele, mnatuchanganyia watoto wetu,vitabu vingine viwepo kwa kila somo ila viwe vya ziada tu. Kitabu cha kufundishia kiwe kimoja ili elimu iwe ni sawa kwa watoto wetu wote na watofautiane kwa juhudi binafsi na kujituma. Mengineyo unayajua zaidi lakini kwa hili sikuungi mkono. Jambo lingine ni utititri wa masomo ambao hanuna maana kabisa, yaani mtoto wa chekechea anasoma masomo matano??mie nilidhani KKK ndio size yake mpaka darasa la 2, lakn wa la pili ana masomo 10,hii sio sawa!Tunatesa watoto ndio maana hakuna wanachoelewa mwishowe mtoto anafika darasa la 7 hajui kusoma wala kuandika. Hapa naona kuna mchezo wa kibiashara tu, kutununulisha wazazi vitabu na madaftari kibao. Tusiipotoshe elimu yetu kwa maslahi binafsi
 
Nilipokuwa shule ya upili kwenye somo la fizikia nilikuwa na vitabu vya wachapishaji wawili tofauti..nelkon na Abbort kwenye kemia nilikuwa na lambert na Arthur A...wanafunzi wanatakiwa kusoma vitabu vingi tofauti ili kujiongezea maarifa
 
Kwa shule ya upili (secondary) ni sahihi kabisa kusoma vitabu vingi ili kupanua uelewa wa somo husika. Lakini nina mashaka kama mtoto wa darasa la kwanza au shule ya msingi kwa ujumla wake kuwa na vitabu vingi kutamsaidia. Kumbuka mtoto huyu akili yake haijakomaa sana kuweza kuunganisha na kuchambua vitu, ukizingatia kuna uandishi tofauti. Hapa kwa mtazamo wangu ni kuwachanganya watoto. Wakati sisi tunatoma darasa la kwanza Kulikuwa na kitabu kimoja tu kwa kila somo.. Kitabu cha kusoma kilikuwepo cha Juma na Roza, hesabu kimoja na kiingereza kitabu kimoja. Huu ulikuwa ni mfumo wa kitabu kimoja kila somo kwa shule za msingi. (kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba. Nadhani kiwango cha elimu kwa wakati huo kilikuwa juu kuliko ilivyo sasa. Shida tuliyo nayo kwa sasa, ni elimu kuwa sehemu ya biashara.
 
Back
Top Bottom