Prof. Ndalichako amtumbua loan officer wa chuo kikuu cha ardhi na kutishia kumfuta kazi mkuu wa chuo hicho

Mm ninavyojua chuo cha ardhi kiko morogoro na tabora yaani
Ardhi institute lakini kama unazungumzia kwa DSM kinaitwa Ardhi University ( chuo kikuu ardhi) zamani UCLAS ilikuwa ni tawi la UDSM
Kwa maana kiliitwa University college of Lands and architectural studies
Wanafunzi wa digital mna shida sana yaani chuo unachosoma bado hujui kinaitwaje,shukuru kuwambo aliharibu sana elimu na ule mfumo wake Big results now (BRN) umetuletea wanafunzi wa mwendokasi mno
Uwezo wako mdogo wa kufkilia ndo chanzo cha majibu yako
 
Kama

Kama yuko innocent, basi atakuwa ana tatizo ambalo lilimkuta na akalikliaa kimya. Nakubaliana na wewe kuwa yaweza kuwa kuna watu walimkwamisha ili kumchafua, lakini kama ndivyo basi alitakiwa achukue hatua ya kuwaripoti wanaomkwamisha na si kuendelea kulumbana na wanafunzi ambao walikuwa wanaamini kuwa ufumbuzi wa matatizo yao uko kwake. Inaweza kuwa kweli yuko innocent. Nakumbuka kuna kipindi fulani juzi juzi mtu mmoja aliwahi kuchafuliwa kuwa ana wanafunzi hewa, wakati hakuwa nao, zilikuwa ni siasa za kwenye vyuo,..., na bahati nzuri that person was very smart. ali-punch na ukweli ukadhihirika baadaye kuwa hakuwa na wanafunzi hewa kama ilivyokuwa inadaiwa. Wabongo pia kwa kuchafuana usiwaache nyuma. Anaweza kuwa amewekewa vigingi ili aisome namaba!

Mkuu kwa tunaojua uchapaji kazi wa mshikaji madai ya wanafunzi ni baseless na kama ukifanyika uchunguzi huru hakuna kesi pale. Nakwambia toka mimi nasoma miaka hiyo huyo jamaa anafuata taratibu zote za kazi yake na haangalii makunyanzi. Kama umevurunda anakupa za uso na hapo chuki na wanafunzi ndipo zinapoanzia. Kwa mfano, kama Bodi wameleta hela na mwanafunzi hakusaini bila ya sababu za msingi na pesa ikarudi halafu Bodi wakazuia mkopo ukienda kwa jamaa kuomba msaada lazima akubane kwa maswali, akutie jambajamba na kukuchana sana kabla hajakusaidia. Sasa haya mambo ndiyo wanafunzi hawayataki. Wao wanataka hata wakivurunda waachwe tu.
 
Basi kama ndiyo hivyo naomba umkumbushe kuwa in essence wanafunzi ni wateja wa vyuo na serikali, japo mahusiano si ya kibiashara vile, ila ukweli ndiyo huo, na mteja ni mfalme! Pili anatakiwa awe na akiba ya uvumilivu na maneno pia, na akumbuke kuwa anaoshughulika nao ni watoto, wengi wao ni watoto. Tafadhali sana naomba abadilike ili aendelee kutumika Taifa bado linamhitaji, na hawa watoto wanaohitaji mkopo nao bado wanamhitaji pia!
 
Ushauri mzuri mkuu lakini hawa wanafunzi wa vyuo vikuu wa miaka hii wengi hamna kitu na hawajitambui. Wanajifanya ujuaji wa kila jambo wakati hawana lolote. Wanachotaka mtumishi afanye kazi kinyume na taratibu lakini mambo yakiharibika wao hawamo mtumishi ndiye anayewajibika. Katika suala la mikopo ya wanafunzi kama mtumishi hauko imara unaweza kujikuta matatani.
 
Wanafunzi wote wamefurahia kufukuzwa kazi kwa loan officer huyo aidha amemuagiza akabidhi ofisi ikiwa imekamilika taarifa zote muhimu na kama itatokea amefanya janja janja zozote za kuchanganya na kuharibu baadhi ya documents ili kumpa shida loan officer atakayeteuliwa adhabu kali juu yake itafuata

Pia Prof Ndalichako ametishia kumfuta kazi mkuu wa chuo hicho kwa sababu ya kumpa taarifa za uongo na kuonesha dalili zote za uzembe.
Nenda SUA kuna loan officer ana kiburi na majibu ya karaha
 
Huyo jamaa huwa wanafunzi wengi tu hapa ardhi wanalamika kuhusu dharau na nyodo zake na haiwezekani awe analaumiwa yeye tu, mpaka hata na hawa first year wa juzi. Kweli anastahili kutimuliwa.

Kwa taarifa yako huyo ndiye Loan Officer pekee aliyefanya kazi kwenye ofisi ile kwa muda mrefu tena kwa mafanikio kuliko waliomtangulia. Lini uliwahi kusikia ARU kuna migomo ya wanafunzi kwa kukosa mikopo? Ile ofisi ni ngumu na ugumu mwingi unasababishwa na ujuaji wa wanafunzi na kutofuata maelekezo na ndiyo maana Loan Officer aliyemtangulia mshikaji alikaa pale miezi mitatu tu akaacha kazi. Ili ufanye kazi ofisi ile unatakiwa uwe tough na mwenye msimamo. Mnatakiwa mseme hasa tatizo ni nini na siyo kumuangushia jumba bovu mshikaji. Au jamaa kawakazia mademu zenu nini?! Maana mmemuandama sana mshikaji kwa madai ya kijinga kabisa.
 
Ushauri mzuri mkuu lakini hawa wanafunzi wa vyuo vikuu wa miaka hii wengi hamna kitu na hawajitambui. Wanajifanya ujuaji wa kila jambo wakati hawana lolote. Wanachotaka mtumishi afanye kazi kinyume na taratibu lakini mambo yakiharibika wao hawamo mtumishi ndiye anayewajibika. Katika suala la mikopo ya wanafunzi kama mtumishi hauko imara unaweza kujikuta matatani.

Na ndiyo maana nikasema, anatakiwa awe na uvumilivu wa akiba, na maneno pia. Ni kutokana na haya unayoyasema hapa! Haya unayoyasema ndiyo inabidi yamu-tune awe kama ninavyotamani awe! Yupi mjinga kati ya mtoto anayeogopa giza na mkubwa anayeogopa nuru?
 
Mkuu kama ni uvumilivu pale ARU hakuna mvumilivu kama jamaa. Amekaa pale ofisini kwa miaka mitano akivumilia madhila ya hawa vijana, tena hatujawahi kusikia malalamiko wala migomo hapo ARU. Loan Officer aliyemtangulia alikaa ofisi ile kwa miezi mitatu tu akaacha kazi kutokana na mtiti wa hawa vijana. Ndiyo maana nikasema kuwa inawezekana kuna kitu nyuma ya pazia maana huwezi kujua labda jamaa amewakazia mademu zao na pengine ndio chanzo cha chuki yote hii.
 
Back
Top Bottom