Prof. Ndalichako akagua miradi ya Elimu Kasulu, Kigoma

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1593591920806.png

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekagua miradi ya elimu inayotekelezwa katika Halmashauri ya Kasulu mkoani Kigoma yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 13. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kasulu, Chuo cha Ualimu Kabanga na jengo la Utawala la shule ya Sekondari Grand.

Akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga mara baada ya kukagua, Waziri Ndalichako amesema chuo hicho kinajengewa upya miundombinu yote baada ya ile ya awali kuchakaa sana na kushindwa kukarabatiwa. Ameongeza kuwa ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho unagharimu zaidi ya bilioni 10, na kuwa utakapokamilika utabadili taswira ya mji huo kwa kuwa majengo yanayojengwa ni ya kisasa na imara ambayo yatadumu kwa muda mrefu.

Akizungumzia mradi wa ujenzi wa jengo jipya la utawala na utengenezaji wa mfumo wa maji katika shule ya sekondari ya Grand, Profesa Ndalichako amesema umegharimu zaidi ya Shilingi milioni 534 na kwamba utakapokamilika utaongeza morali ya walimu kufundisha na kusaidia wanafunzi waliopo katika shule hiyo. Mradi mwingine uliotembelewa na Waziri wa Elimu ni ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha wilaya ya Kasulu ambao upo katika hatua za mwisho ambao umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 2.97.

Jumla ya majengo 15 yatajengwa na kitachukua wanafunzi 320 watakaokuwa wakilala chuoni hapo. Waziri Ndalichako amewataka wananchi wa wilaya ya Kasulu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutumia fursa ya kuwepo kwa vyuo mbalimbali katika Halmashauri hiyo kujipatia maarifa na ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa ama kujiajiri ili kujiletea maendeleo binafsi na ya mkoa wa Kigoma.
 
Anatafuta kura tu Hana lolote. Kwa Nini asimuachie Waziri wa ujenzi ndo aje kukagua maendeleo ya ujenzi.
 
We already know that she will run for parliamentary elections in Kigoma, so this is like his first part of the campaign.
 
Anahangaika tu, kukagua majengo sio kazi yake kama Waziri wa Elimu.

Aongee basi Kingereza tena
 
Anatafuta kura tu Hana lolote. Kwa Nini asimuachie Waziri wa ujenzi ndo aje kukagua maendeleo ya ujenzi.

Hilo la kura linaweza likawa lakini kumbuka ni Waziri wa Elimu na maeneo yote aliyotembelea yanahusiana moja kwa moja na wizara anayoiongoza Mkuu
 
Huyo maza anapokua anaongea hua naona kama fuse kidogo zime.......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom