Elections 2015 Prof. Mwandosya: Richmond na Escrow wakatwe urais CCM

Lakini kumbu kumbu zake za wanaohusika na scandals za Richmond na Escrow ziko intact.

Mkuu masopakyindi nina uhakika katika ulingo huu wa siasa haujaanza kufuatilia leo.Mwandyosa hapaswi hata kumnyooshea kidole kada yeyote yule kwa kumuita fisadi.Yeye ndie miongoni mwa waanzilishi wa ufisadi serikalini.Sakata la Alliance Air gazeti la RAI (miaka ya 90 -2000) lilianika kila kitu juu ya Mwandyosa na hakuwahi kukanusha.
 
Last edited by a moderator:
Sisi watanzania tunakata CCMyote ikatwe kwa mana wao ndio wahusika wa masakata yoote yaliyowahi kutokea Tanzania
We bawacha nyamaza bana usituharibie siku ccm ndiyo chama ambacho tunaona kinamsaada kwa watanzania siyo hiyo michagadema yenu.
 
Mkuu masopakyindi nina uhakika katika ulingo huu wa siasa haujaanza kufuatilia leo.Mwandyosa hapaswi hata kumnyooshea kidole kada yeyote yule kwa kumuita fisadi.Yeye ndie miongoni mwa waanzilishi wa ufisadi serikalini.Sakata la Alliance Air gazeti la RAI (miaka ya 90 -2000) lilianika kila kitu juu ya Mwandyosa na hakuwahi kukanusha.
Mkuu hizo scandals zilikuwa za kupikwa na kundi ka mtandao, Lowassa alikwemo.
Hiyo inaitwa di-information ya kurusha mchanga kwenye macho ya watu kwa nia ya kuwachafua.
Scandals za Richmond na Escrow are for real.
 
Mtia nia wa urais CCM Prof.Mark Mwandosya amesisitiza kuwa watia nia wote wa urais wanaosakamwa na masakata hatari ya Richmond na Escrow ni lazima wakatwe kugombea urais.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa kati ya wagombea Mh. Lowassa amewahi kukumbwa na sakata la Richmond hadi kupelekea kujiuzuru u-PM.Vilevile Prof. Muhongo alilazimika kujiuzuru kwa kashfa ya ESCROW.

Wakatwe tu!!!
 
huyu mzee nilizani amepona.wsshindane kwa hoja nasio kutafuta sababu za kumshambulia lowasa.CCM yote ni mafisadi.wanapotumbua mamilioni huku watoto wanakaa chini hili mwandosya halioni.lowasa ndie kiongozi aliyedhubutu kuonyesha anaweza

Lowasa anaweza kwalipi!? Mbona mnajitia upofu? Alidhubutu kuonyesha anaweza nini? Jamani watanzania tunajitia upofu, Lowasa amekudhu sehemu ya serilaki since 1977, mpaka leo hakuna alichofanya ambacho ni cha kukumbukwa zaidi ya kashfa ya richmond na nyingine. Huyu mtu anauzuri gani! Au ndo mahaba niue
 
Huyu mzee atakuwa ameshasahau tarehe yake ya kurudi kwenye matibabu India.

Mimi kutoka kwenye nafsi yangu huyu babu re -proffesa hata hanivutii kumpa kura yangu , mara mia hata nimpigie babu Mkaidi wa NLD kuliko Mwandosya. Huwa wana msifia sana ila sijawahi kuona makeke yake kisiasa zaid ya kumuona yupo yupo tu kama fungu la kukosa.
 
huyuhuyu mwandosya alisema ccm walimtusi warioba ili wapitishe katiba ya ccm.la huyu hafai uraisi.warioba aliofanya kosa gani mpake mtia nia huyu amtusi ili katiba ipite hafai uraisi huyu.na huyu mebe kila kukicha anaenda kusali kwenye kaburu la nyerere huyu anaabudu mizimu atatuletea imani za mizimu hafai
 
Yeye Mwandosya alilipwa na Rwanda aitulize Tanzania kuhusu Bunge la EA kuhamia Kigali, pia Makao Makuu ya EA Business teyari wamehama na yeye atalipiwa matibabu ya Gonjwa lake India hadi anafariki, mfadhili ni Kagame.
Ununuzi wa Radar, yeye kachukuwa USD 200,000. Abishe vyote ili tufunguke zaidi.

Ulikuwa wapi siku zote? Acheni uzushi na upuuzi wachumia tumbo ninyi!
 
Lowassa ni Mwizi akatwe! Anataka tumpe nchi ili watuchezee na akina Rostam Aziz na hata waliomzukunguka tu wooote wezi watupu!
 
Yeye Mwandosya alilipwa na Rwanda aitulize Tanzania kuhusu Bunge la EA kuhamia Kigali, pia Makao Makuu ya EA Business teyari wamehama na yeye atalipiwa matibabu ya Gonjwa lake India hadi anafariki, mfadhili ni Kagame.
Ununuzi wa Radar, yeye kachukuwa USD 200,000. Abishe vyote ili tufunguke zaidi.
Ccm imeoza by Makongoro Nyerere.
 
Mtia nia wa urais CCM Prof.Mark Mwandosya amesisitiza kuwa watia nia wote wa urais wanaosakamwa na masakata hatari ya Richmond na Escrow ni lazima wakatwe kugombea urais.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa kati ya wagombea Mh. Lowassa amewahi kukumbwa na sakata la Richmond hadi kupelekea kujiuzuru u-PM.Vilevile Prof. Muhongo alilazimika kujiuzuru kwa kashfa ya ESCROW.

HANA JUKUMU LA KUTAMKA HAYO,
WIVU UNAMSUMBUA!/
WATANZANIA WANAIJUA KWA UNDANI RICHMOND/ KUJIUDHULU KWAKE NI UADILIFU ULIOTUKUKA,
KWANI ALISHINDWA KUKOMAA KAMA PINDA???
SUALA LILIKUWA NI HEKIMA TU KUTUMIKA,.eu/
 
huyuhuyu mwandosya alisema ccm walimtusi warioba ili wapitishe katiba ya ccm.la huyu hafai uraisi.warioba aliofanya kosa gani mpake mtia nia huyu amtusi ili katiba ipite hafai uraisi huyu.na huyu mebe kila kukicha anaenda kusali kwenye kaburu la nyerere huyu anaabudu mizimu atatuletea imani za mizimu hafai

CCM hawafai
 
Inasikitisha sana viongozi wanajua kuwa Vodacom inawaibia wananchi lakini wanasubiri kuulizwa. Kauli kama hizi zinasikitisha sana.

"Watatuuliza kuhusu EPA, wataendelea kutuuliza kuhusu Richmond, watatuuliza kuhusu Escrow, kubwa zaidi watatuuliza kuhusu Vodacom ingawa hili halizungumzwi lakini linakuja, lazima tujitayarishe", Prof. Mwandosya

Monday, June 22, 2015

Mwandosya: Lowassa Asisite Kuniunga Mkono

Mpekuzi blog

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu, Profesa Mark Mwandosya amemuomba mgombea mwenzake katika kinyang'anyiro cha kutafuta ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea kupitia CCM, Edward Lowassa asisite kumuunga mkono kama walivyofanya watangaza nia wengine ili mambo yaishe mapema.

Aidha, amewaonya wanaotishia kukihama chama endapo hawatapitishwa, akisema huo ni upuuzi na pia vitisho kwa Mwenyekiti wa Chama na wanaCCM kwa ujumla, hivyo wanaojiona wao ni maarufu kuliko chama wanajidanganya.

Mwandosya alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wilayani Mbozi alipokuwa akizungumza na wanaCCM waliomdhamini katika mbio zake za urais, pamoja na wanachama wengine waliojitokeza katika Ofisi za CCM Wilaya.

Mgombea huyo alisema amefarijika kusikia anaungwa mkono na wagombea wenzake, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe pamoja na kupata taarifa za Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira naye kusema anamuunga mkono.

Alisema pamoja na kuungwa mkono na wenzake hao watatu, anamuomba pia Lowassa naye kumuunga mkono ili kuipunguzia kazi Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM).

"Nimesikia Membe amesema hapa Mbeya asipopitishwa yeye basi atamuunga mkono Profesa Mwandosya, nikasikia tena na Waziri Mkuu akisema hata kama asipopitishwa yeye atafarijika kama Profesa Mwandosya atakuwa mgombea, nikasikia tena na Wassira naye kupitia kwa mtu wake wa karibu ataniunga mkono, sasa namuomba mwenzangu naye Edward au maarufu kama Edo naye aseme Profesa ndiyo wangu, ili kazi iishe na tuipunguzie kazi Halmashauri Kuu,"alisema Profesa na kushangiliwa.

Awali Profesa Mwandosya aliwaeleza wanachama hao kuwa mwaka huu wa uchaguzi ni mwaka mgumu sana kwa CCM na kuwataka wanachama kutofanya mchezo katika kujibu mapigo ya wapinzani.

"Watatuuliza kuhusu EPA, wataendelea kutuuliza kuhusu Richmond, watatuuliza kuhusu Escrow, kubwa zaidi watatuuliza kuhusu Vodacom ingawa hili halizungumzwi lakini linakuja, lazima tujitayarishe.

"Sasa nani huyo ataweza kutusafisha, wananchi wakimtazama watasema huyu atatusaidia na atajibu, kila ninakopita naambiwa na wananchi kuhusu ufisadi na rushwa vinatuumiza."

"Kama chama lazima tukabiliane na hilo na hapa hatumzungumzii mtu lazima kama chama tuyaeleze kwa wananchi. Nani atafanya hivyo wakubwa wanajua," alisema Profesa.

Akizungumzia wanaotishia kuhama chama, alisema wanajidanganya kwani CCM ni maarufu zaidi ya mtu mmoja mmoja, akisema mtu pekee aliyewahi kuhama na kukitikisa chama alikuwa Augustine Mrema, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani.

Mpekuzi blog

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom