Mimi nimeamini maneno ya Kub Mbowe wakati wakimkabidhi ripoti Waziri Mkuu, kwamba anaishukuru serikali kwa kuliamini bunge na kuwa mambo yote yameenda vizuri. Labda wewe mkuu unazijua kanuni za bunge kumpita Mbowe, Silinde na wakili msomi Ole Milya!!!!!Acha porojo bwana mdogo rudi kwenye kanuni za utendaji wa mihimili yetu inavyoelekeza. Usipende kuamini anayoyaongea rais wetu mpendwa, ayaongeayo mengi yana matatizo ya kiufundi na kiafya..
Kuhusu kumuangalia Lipumba ni bora niangalie nzi walivyo kizunguka kinyesi.
Ripoti ilikua kwenye flash mzee. Ile ya dom ilikua funika kombe tu, rimoti iko ferryView attachment 584627
Mwanasiasa mkongwe na waziri mwandamizi wa zamani,Prof Mark Mwandosya ameandika katika "tweet" akihoji kuwa,huu utaratibu wa kamati ya Bunge kuundwa na Spika kuchunguza jambo fulani,na baadae badala ya kuliwasilisha bungeni na wabunge kupata muda wa kujadili,safari hii kamati zimewasilisha taarifa zao nje ya bunge lakini katika viwanja vya bunge,na baadae taarifa hiyo kukabidhiwa kwa Rais.
Prof Mwandosya anahoji anasema "Je Kanuni za Bunge zimabadilika?"...Maana ilivyozoeleka na kwa mujibu wa kanuni,kamati kama hizi huwasilisha taarifa zao ndani ya bunge,bunge hujadili na baadae kutoa maazimio ambayo Serikali hupaswa kuyafuata na kuyatekeleza.
Hivi ndivyo ilivyofanya kamati ya Mwakyembe juu ya suala la Richmond,Kamati ile ya Operesheni Tokomeza na hata kamati hizi mbili za kuchunguza Tanzanite na Almasi zilipaswa kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge.
Nami niungane na Prof Mwandosya kuuliza "JE KANUNI ZA BUNGE ZIMEBADILIKA"
barafu wa JF
Mnajitahidi sana kutetea maovu, na actually nyie ni sehemu ya maangamizi yanayoelekezwa kwa taifa hili. Baada ya awamu hii utawala utakaoingia madarakani(kama waliopo hawatajigeuza akina Kagame, M7 na Mugabe) kazi kubwa ya kwanza itakuwa kuanza upya kuirejesha nchi katika kuheshimu mihimili (mgawanyo wa madaraka).Kanuni hazijabadilika na wala hazijavunjwa. Tofauti na kamati hizo nyingine alizotaja prof Mwandosya ambazo ziliundwa kwa utashi wa bunge lenyewe, hizi za juzi ziliundwa kwa ombi la Rais. Kama ulimsikia Spika Ndugai wakati anawasilisha alisema wazi aliunda kamati zile kutokana na ombi la Rais kwamba bunge limsaidie kuchunguza. Kimsingi kamati ya bunge ndio bunge lenyewe na taarifa hii ilikuwa ni hitaji la serikali so hakukuwa na haja ya mjadala wa bunge zima kwani si wao walioagiza uchunguzi. Ahsante!
Sasa na huyu dereva wetu tumuiteje maana walikuwa wote barazaniHuyu ni mpumbavu sana. Ushenzi wao ndo umetugarimu leo anauliza unafiki. Prof wa Tz wengi ni matahila.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ameulizwa kwa sababu amegeuka nyani haoni ...Hili ndio jibu la swali lake? Usihamishe goli
Na ipo siku mawe yataongeaNaona Wazee yamewafika shingoni,wanaanza kuuliza maswali "indirect" ya juu ya uvunjwaji wa sheria na katiba.
Tundu Lissu alishasema sana...Wakati anasema wengi tulikuwa kimya,sasa naona hata waliokuwa kimya nao wameanza kusema yaleyale ambayo Lissu alianza kuyasema miaka miwili iliyopita.
Mwisho wa siku,wazee wote wataibuka na kuanza kurudia kusema yale ambayo Lissu alishayasema huko nyuma,akaishia kuitwa mchochezi!!
Duuuh....A Novice has been given a task of his/her Senior!!No doubt he/she will never meet a target
Hili jambo nami niliuliza hapa jamvini katika mtindo wa kuomba mwongozo kwa Mhe. Spika. Bunge letu lijitathmini kweli ama la, linatekeleza matakwa ya Kikatiba, Kisheria na Kikanuni.View attachment 584627
Mwanasiasa mkongwe na waziri mwandamizi wa zamani,Prof Mark Mwandosya ameandika katika "tweet" akihoji kuwa,huu utaratibu wa kamati ya Bunge kuundwa na Spika kuchunguza jambo fulani,na baadae badala ya kuliwasilisha bungeni na wabunge kupata muda wa kujadili,safari hii kamati zimewasilisha taarifa zao nje ya bunge lakini katika viwanja vya bunge,na baadae taarifa hiyo kukabidhiwa kwa Rais.
Prof Mwandosya anahoji anasema "Je Kanuni za Bunge zimabadilika?"...Maana ilivyozoeleka na kwa mujibu wa kanuni,kamati kama hizi huwasilisha taarifa zao ndani ya bunge,bunge hujadili na baadae kutoa maazimio ambayo Serikali hupaswa kuyafuata na kuyatekeleza.
Hivi ndivyo ilivyofanya kamati ya Mwakyembe juu ya suala la Richmond,Kamati ile ya Operesheni Tokomeza na hata kamati hizi mbili za kuchunguza Tanzanite na Almasi zilipaswa kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge.
Nami niungane na Prof Mwandosya kuuliza "JE KANUNI ZA BUNGE ZIMEBADILIKA"
barafu wa JF
Dah! Afadhali yeye zimemrudia. Bunge lote kimya wao wanavuta posho tu na mishahara. Wao ndo walitakiwa kuidai ripoti. Ni muhimu mihimili iweze kuwa independent kama katiba inavyotaka.Hawa wazee wakishatoka madarakani ndo akili zinawarudia. Strange indeed!
Huyu ni mpumbavu sana. Ushenzi wao ndo umetugarimu leo anauliza unafiki. Prof wa Tz wengi ni matahila.
Sent using Jamii Forums mobile app
Anachosema mkuu ni sawa, lakini kwanini raisi asingeunda kamati kama ile ya Prof.Mruma badala yake akatumia bunge? Hapo ndipo panaleta shida kwa sababu kamati ikishakuwa ya bunge hata kama raisi ndiye aliomba iundwe lazima kikanuni repoti ya kamati hiyo iwasilishwe kwenye bunge na kujadiliwa na bunge, na mapendekezo ya bunge yapelekwe serikalini kwa utekelezaji.Kanuni hazijabadilika na wala hazijavunjwa. Tofauti na kamati hizo nyingine alizotaja prof Mwandosya ambazo ziliundwa kwa utashi wa bunge lenyewe, hizi za juzi ziliundwa kwa ombi la Rais. Kama ulimsikia Spika Ndugai wakati anawasilisha alisema wazi aliunda kamati zile kutokana na ombi la Rais kwamba bunge limsaidie kuchunguza. Kimsingi kamati ya bunge ndio bunge lenyewe na taarifa hii ilikuwa ni hitaji la serikali so hakukuwa na haja ya mjadala wa bunge zima kwani si wao walioagiza uchunguzi. Ahsante!