Prof. Mussa Assad: Nilipokuwa ofisini niliomba nyaraka za SGR, Air Tanzania na mradi wa Stiegler's Gorge lakini sikupewa hata moja

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,632
2,000
Alipaswa kujiuzuru immediately.

Kama umepewa kazi flani ufanye halafu ukanyimwa vitendea kazi, hapo utakua unafanya kazi gani? Unapaswa kuachana nayo haraka.

Sasa yeye hakujiuzuru halafu anakuja kulia lia hapa. Hizi ni chuki tu za kufumuzwa u cag.
Profesa anakuja kuongea wakati Bosi wake ameshafariki dunia. Unafiki ule ule tu.
 
chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
3,382
2,000
Mbona alikuwa kmy muda wote, kumbe naye mnafiki kama wengine

Ulisha fanya kazi jishini,polisi au serekalini unajua maana ya vyeo kuna mda unaweza kutulizwa kutokana na ngazi kwa vile hipo juu.dai katiba maana raisi kapewa madaraka makubwa ya mungu mtu
 
Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
6,527
2,000
Kawaida ukishastaafu au kuondoka kwenye nafasi yako usipende kuongelea mambo ya ofisi uliyokuwa.

Ulishamalizana nao basi sababu wakikubana ukasema una ushahidi ukienda ofisini kuomba hata barua labda hawakupi. Si sahihi sana ukishatoka kuongelea mambo ya ofisi ulikokuwa achana nayo endelea na maisha mengine.
Tu endelea kupigwa siyo..
 
misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
11,235
2,000
Kwanini hili la ndege na mnunuzi ambayo hayakupitishwa wala kuidhinishwa mnakwepa kujibu na kuyaongelea na mtu akiyaongelea anaonekana katumwa?

Acheni watu wapumuwe, tusaidieni uwazi na ukweli halafu hiki si kipindi cha kubwabwaja ni data tu.

Mkuu naomba unisaidie report ya CAG kama unayo kwa Pdf

Ulisoma report ya CAG ya mwaka 2015/16 na 2016/17

Majibu yako yako humo,

Sasa tusaidie na hili la sasa ili tujue hela zetu ziliingiaje na kutumikaje
La kuuziana nyumba za NSSF vipi?
 
nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
676
500
Kawaida ukishastaafu au kuondoka kwenye nafasi yako usipende kuongelea mambo ya ofisi uliyokuwa.

Ulishamalizana nao basi sababu wakikubana ukasema una ushahidi ukienda ofisini kuomba hata barua labda hawakupi. Si sahihi sana ukishatoka kuongelea mambo ya ofisi ulikokuwa achana nayo endelea na maisha mengine.
Kwa maana hiyo sina hata sifa za kutoa ushahidi mahakamani kama Kesi inaihusu Ofisi niliyo wahi kuifanyia Kazi?
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
482
500
Kawaida ukishastaafu au kuondoka kwenye nafasi yako usipende kuongelea mambo ya ofisi uliyokuwa.

Ulishamalizana nao basi sababu wakikubana ukasema una ushahidi ukienda ofisini kuomba hata barua labda hawakupi. Si sahihi sana ukishatoka kuongelea mambo ya ofisi ulikokuwa achana nayo endelea na maisha mengine.

Hakika tunapitia kipind kigumu sana kuwahi kutokea ila ni mapito tu mkuu.
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
36,403
2,000
Binadamu wa sasa ile kitu inaitwa aibu hakuna kabisa.

Yaani mtu anaitisha press kumsuta marehemu ilhali anajua kabisa mhusika hayupo na hataweza kujitetea.
Mwendazake hakuwahi kujitetea kwa hoja ila kwa risasi.

Assad alilijua hill ndio maana alikaa kimya ili aje aseme sasa.
 
Zenjiboe

Member
Aug 26, 2020
45
125
Profesa Assad amefichua kuwa aliomba nyaraka za ununuzi wa ndege, reli ya SGR pamoja na Bandari ya Bagamoyo kwa kutumia technical reason lakini mkuu wa nchi wa wakati huo alikataa kuzitoa akawa anamtafutia sababu ya kumtoa ofisini.

Prof Assad amesisitiza kuna muda watu wanavunja katiba waziwazi lakini Taifa linashindwa kuwakosoa kutokana na hofu na uwoga.

Prof Assad amesisitiza kwa kukaa kwake ofsini alizihitaji sana hizo nyaraka ili azisome na atoe ushauri wa kibiashara kwani amefanya kazi hizo kwa miaka mingi kabla ya kuwa CAG kabla ya kuzikagua.

Prof Assad ametoa ushauri ni muda muafaka wa serikali kuweka nyaraka wazi kwa Raia wake ili wazichambue na kuboresha mapungufu kuliko Kuzificha Ikulu.

===

Wakati nipo ofisini, katika vitu ambavyo ni vitu vitatu: niliomba SGR, niliomba document ya Air Tanzania upya na niliomba project ya Stiegler's Gorge -- feasibility studies. Na sikupewa hata moja. Nilichopata ilikuwa ni barua kwamba mwaka haujamalizika na kwahiyo ukaguzi wa hesabu si wakati wake.

Na kila mtu mwenye akili alikuwa anajua nilichokuwa nataka kufanya si ukaguzi wa hesabu, lakini ilikuwa ni technical response ya kusogeza muda na kuniondoa katika reli tu. Kwahiyo, mpaka nimeondoka ofisini I never got that information na mpaka sasa hivi sijatafuta na sijasoma.

Wewe ni kama mimi. I'm a private citizen now. Ikitokea taarifa hii ipo wazi, tutaisoma na tutatoa commentary.

View attachment 1749054
Miongon mwa waoga ni yeye.huon alikaa kimya Leo ndio anasema alinyimwa. KWA nini hakusema muda ule na kujiuzulu.Mnakatisha tamaa sana
 
Heavy equipment

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,056
1,500
Usitoe hasara nyingine hadharani tumechoka na lmetosha

Nchi hii wenye akili ndogo wanaongoza wenye akili kubwa
IMG-20210409-WA0055.jpg
IMG-20210409-WA0000.jpg
IMG-20210408-WA0130.jpg
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
482
500
Ulitaka ajipime ubavu na Rais au? Vitu vingine vinahitaji fikra yakinifu kabla ya kumu attack mtu.
Miongon mwa waoga ni yeye.huon alikaa kimya Leo ndio anasema alinyimwa. KWA nini hakusema muda ule na kujiuzulu.Mnakatisha tamaa sana
 
Heavy equipment

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,056
1,500
Miongon mwa waoga ni yeye.huon alikaa kimya Leo ndio anasema alinyimwa. KWA nini hakusema muda ule na kujiuzulu.Mnakatisha tamaa sana
Tundu lisu mlimpiga risasi 30 bado unataka na mwingine ajitokeze aseme ukweli?

Wapi yupo Azory gwanda jamani?

Wapi yupo ben saa8 jamani?

Nyiie tumieni mitutu sisi tutafunga na kuomba na hii ndio Dawa ya maraisi wakorofi nchini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom