Prof. Mussa Assad: Nilipokuwa ofisini niliomba nyaraka za SGR, Air Tanzania na mradi wa Stiegler's Gorge lakini sikupewa hata moja

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Profesa Assad amefichua kuwa aliomba nyaraka za ununuzi wa ndege, reli ya SGR pamoja na Bandari ya Bagamoyo kwa kutumia technical reason lakini mkuu wa nchi wa wakati huo alikataa kuzitoa akawa anamtafutia sababu ya kumtoa ofisini.

Prof Assad amesisitiza kuna muda watu wanavunja katiba waziwazi lakini Taifa linashindwa kuwakosoa kutokana na hofu na uwoga.

Prof Assad amesisitiza kwa kukaa kwake ofsini alizihitaji sana hizo nyaraka ili azisome na atoe ushauri wa kibiashara kwani amefanya kazi hizo kwa miaka mingi kabla ya kuwa CAG kabla ya kuzikagua.

Prof Assad ametoa ushauri ni muda muafaka wa serikali kuweka nyaraka wazi kwa Raia wake ili wazichambue na kuboresha mapungufu kuliko Kuzificha Ikulu.

===

Wakati nipo ofisini, katika vitu ambavyo ni vitu vitatu: niliomba SGR, niliomba document ya Air Tanzania upya na niliomba project ya Stiegler's Gorge -- feasibility studies. Na sikupewa hata moja. Nilichopata ilikuwa ni barua kwamba mwaka haujamalizika na kwahiyo ukaguzi wa hesabu si wakati wake.

Na kila mtu mwenye akili alikuwa anajua nilichokuwa nataka kufanya si ukaguzi wa hesabu, lakini ilikuwa ni technical response ya kusogeza muda na kuniondoa katika reli tu. Kwahiyo, mpaka nimeondoka ofisini I never got that information na mpaka sasa hivi sijatafuta na sijasoma.

Wewe ni kama mimi. I'm a private citizen now. Ikitokea taarifa hii ipo wazi, tutaisoma na tutatoa commentary.


 
Aisee
JamiiForums475437714.jpg
 
Prof Assad kuna jambo anatupa ishara hapa kuhusiana na hizo nyaraka kufichwa Ikulu, kwa wenye akili wanaelewa ishara anayotoa. Ametumia fasihi kusema ya kwamba aliziomba hizo nyaraka ila hakupewa zimefichwa Ikulu.

Na pengine marehemu alishazichoma moto kitambo au alizipeleka kwake "CHATO" kuzificha chini ya uvungu wa kitanda. Aligeuza nchi ya kwake peke yake.
 
Kawaida ukishastaafu au kuondoka kwenye nafasi yako usipende kuongelea mambo ya ofisi uliyokuwa.

Ulishamalizana nao basi sababu wakikubana ukasema una ushahidi ukienda ofisini kuomba hata barua labda hawakupi. Si sahihi sana ukishatoka kuongelea mambo ya ofisi ulikokuwa achana nayo endelea na maisha mengine.
 
Nimemsikia Prof Assad, Huyu inatakiwa arudishwe ili aendelee kulitumikia taifa.

Amesema ATCL ivunjwe, ndege ziuzwe maana hamna kitu wanafanya.

Mkataba wa Bagamoyo uwekwe wazi watu wasome na kama kuna vitu vya kukubaliana vinaweza kurekebishwa ili mradi ujengwe.
 
Back
Top Bottom