Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,234
Waungwana salaam.
Kwa mujibu wa katiba ikisomwa pamoja na Sheria ya ukaguzi wa umma ya mwaka 2008 Rais ndiye mwenye mamlaka ya kumteua mtanzania kuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG. Mbali na sifa za kihasibu na ubobezi na uzoefu sifa nyingine ni lazima awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
Kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atadumu kwa muda wa miaka 5 na anaweza kuongezewa mkataba wa kipindi kimoja tu kingine cha miaka mitano. Kwa maana hiyo sheria inaruhusu mkaguzi kukaa vipindi viwili tu vya miaka mitano mitano.
Kwa kuwa Mheshimiwa sana CAG aliyepo Prof. Assad uteuzi wake ulianza rasmi baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete tar 5 November, 2014 basi miaka yake mitano itaisha mwaka huu November 5, 2019.
Kwa kuwa hakuna ubishi kuwa mtu huyu ni mwadilifu na mbobezi. Kwa kuwa hakuna mashaka kuwa CAG aliyepo amefanya kazi iliyotukuka iliyofanya mpaka UN wakampatia sifa, Je Mheshimiwa Rais atakuwa tayari kumuongezea mkataba wa miaka mingine mitano?
Wanajamvi au mnaonaje?