Prof. Mukandala wa udsm hana hatia - baraza la maadili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Mukandala wa udsm hana hatia - baraza la maadili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mabulangati, May 10, 2011.

 1. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wandugu, Baada ya sakata la watumishi wa umma takribani 16 kuitwa kwa mbwembwe bele ya baraza la maadili ya watumishi wa umma kwa kutowasilisha fomu za matamko ya mali na madeni waliyonayo, ni majuzi tu nilishangazwa na habari iliyotolewa na gazeti la mwananchi ikielezea kuwa baraza la maadili lamsafisha prof. mukandala. Gafla bin vuuu siku iliyofuata mliman TV wakatoka na taarifa hiyo pia.

  Kinacho nishangaza ni jinsi utaratibu mzima ulivyoendeshwa maana sijajua ni kwanini kuitwa kwao kulikua public yaani (press conference), kusomewa shtaka na kuhojiwa ilikuwa wazi kabisa lakini hukumu imetoka kisirisiri?!!!! Mwanzo nilidhani ni uongo lakini baada ya kufuatilia kwa umakini nimeipata barua rasmi kutoka chanzo nyeti (fungua attachment usome mwenyewe barua hii).

  Maswali ya msingi, je wengine wameishia wapi? Je hukumu imekua siri au kimyakimya kwa misingi ipi? Je ilikua siasa tu na kwa maslahi yapi? je gharama za kuendesha shughuli nzima pale karimjee zililipwa na nani? je JK anajua lolote kuhusu hukumu hizi, isije ikawa anadanganywa maana tukumbuke iliripotiwa kuwa washauri na marafiki wa JK wafikishwa kwa pilato kwa kutowasilisha fomu za mali na madeni? Je ni wangapi wamekutwa na hatia na wangapi hawana hatia na nini kitafuata?

  Mwisho wana JF hebu tujadili hatuoni umuhimi wa baraza na tume ya maadili kuitisha mkutano wa waandishi wa habari (press conference) kututoa hili wingu zito lililoni/tuzinga?
   

  Attached Files:

Loading...