Prof Mukandala "Hawa wanafunzi sijui walipenya vipi na hili bango"

Kiherehere

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,806
621
Hivi hawa watu wa kujipendekeza kwa viongozi sijui tunawapata wapi? Hivi Prof Mukandala anashindwa kuheshimu elimu yake aliyonayo KULIKO aliyonayo MWANSIASA PINDA? Kwani kupeleka ujumbe kwa njia ya mabango inaathiri nini? Au alitaka tuanze kusifia kuwa vyumba vya kulala VIMEENEA?.

Kwa mtazamo wangu wanasiasa na viongozi kwa ujumla wanapaswa kujua UKWELI Mukandala..., SIO KUUFICHA!

Kwa tabia ya kuficha ukweli HUPASWI KABISA KUWAA KIONGOZI!!!!!!!!

Mukandala anashangaa jinsi bango lililoandikwa "MTOTO WA MKULIMA TUNALALA NJE" na wanachuo wa UDSM je ni kweli "eti leo mukandala kushangaa wanachuo wanalala nje ya campus UDSM"

Nini mawazo yako kwa viongozi kama hawa?
 
Mukandala mbona ni mwanasiasa wa siku nyingi? Kuna mtu aliwahi kupendekeza kuwa inabidi tuwe na sheria inayowakataza watendaji wakuu wa serikali kuingia kwenye siasa baada ya kustaafu, mfano makatibu wakuu, magavana, wakuu wa majeshi, n.k. Mukandala ni miongoni mwa watendaji wa serikali wanaotaka kukandamiza haki za anaowaongoza ili aonekane anafanya kazi vizuri, hii kitu hatari sana
 
Huyo ni CCm na kazi yake ni kuona kila mtu anasema wanachuo wa UDSM wana makazi bora kuliko hata OXFORD. Mficha maradhi kifo humuumbua... Acha kwanza yalipuke magonjwa ya mlipuko(hatuombei litokee) ndio atasema kuwa vijana wetu hawana makazi
 
MCL The Citizen Mwanaspoti Nation Monitor Digital Paper

Ingia MwanzoContactsEmail

search0.png

Sat 27 Nov 3:56PM









rss.png

RSS







Home
arrow.png
Habari
arrow.png
Habari za Kitaifa
arrow.png
Pinda apokewa kwa bango UDSM


BOOKMARK THIS PAGE




.buttonheading { float: right; padding-left: 19px; width: 92px; }.buttonheading a { font-weight: bold; text-decoration: none; }
bot_tabimg.gif

Pinda apokewa kwa bango UDSM Send to a friend Saturday, 27 November 2010 08:12 0diggsdigg

chuokikuupinda.jpg
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa na bango lenye ujumbe kwa Waziri mkuu, Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho na mkutano wa mwaka wa jumuiya ya wahitimu uliofanyika jana ambapo Pinda alikuwa mgeni rasmi. Picha na Silvan Kiwale

Fredy Azzah
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walimkaribisha chuoni kwao Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa bango lililoandikwa "Mtoto wa Mkulima, Tunalala Nje", kilio kilichomsukumu mtendaji huyo mkuu wa serikali kuahidi kukichangia Sh10 milioni kila mwaka kwenye ujenzi wa malazi yao hadi ukomo wa uongozi wake.Wanafunzi hao wanalazimika kupanga kwenye hosteli na nyumba zilizo nje ya chuo hicho kikongwe kutokana na tatizo kubwa la upungufu wa malazi. Hata wale wanaolala chuoni hapo, hulazimika kujazana wengi kwenye chumba kimoja tofauti na zamani wakati chumba kimoja kilikuwa kikitumiwa na wanafunzi wawili tu.
Kutokana na upungufu huo, wanafunzi hutumia muda mwingi kwenye safari za kati ya chuoni na maeneo wanayoishi.
Hali hiyo ndio iliwasukumu waamue kumfikishia ujumbe mtendaji huyo mkuu wa serikali jana kwenye Ukumbi wa Nkurumah wakati Pinda alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya UDSM ambayo yamepangwa kufanyika Oktoba mwakani.
Iwapo Pinda atamaliza miaka mitano ya uongozi akiwa Waziri Mkuu atakuwa amechangia jumla ya Sh50 milioni katika jitihada za kukiwezesha chuo hicho kikongwe nchini kutatua tatizo la malazi kwa wanafunzi.
Katika tukio hilo la kwanza la aina yake kumkuta Pinda tangu alipoteuliwa tena kuwa waziri mkuu na kuapishwa wiki iliyopita, wanafunzi waliokuwa wameketi kwa utulivu sehemu ya juu ya Ukumbi wa Nkrumah walibandika bango hilo lililokuwa na maandishi hayo makubwa.
Pinda pamoja na baadhi viongozi waliokuwa meza kuu, walionekana kulisoma bango hilo lililoonyesha kilio cha wanafunzi hao kukosa maeneo ya kulala eneo la chuo na kulazimika kuishi nje ya chuo ambapo gharama za maisha ni kubwa.
Alipoanza kutoa hotuba yake, Pinda alianza kwa kulizungumzia bango hilo huku akieleza kuwa ujumbe walioukusudia wanafunzi hao umefika.
“Nilipokuwa nimeketi (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard) Membe aliniandikia ujumbe kwenye karatasi akaniambia 'umeona massage (ujumbe) yako?', nikamwambia 'niliiona toka zamani,'” alisema.
“(Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza) Mukandala naye akaniambia akihoji: 'Hawa wanafunzi sijui walipenya vipi na hili bango'.
"Nikamwambia 'itakuwa wametumia kaujanja kadogo tu kwa kulikunja likawa kama madaftari, kwa hiyo mtu akabeba kama kitabu anachoenda kujisomea', lakini pamoja na mwandiko na bango lao baya baya, nasema massage imefika.”
Kutoka na hali hiyo, Pinda alitoa ahadi ya kuchangia Sh10 milioni kila mwaka mpaka pale muda wa uongozi wake utakapomalizika.
Hata hivyo, baada ya kutoa ahadi hiyo Pinda alimtaka Membe naye kutoa ahadi yake na waziri huyo wa mambo ya nje akaahidi kutoa Sh5 milioni kila mwaka mpaka pale muda wa uongozi wa Pinda utakapomalizika.
“Natumaini utanikubalia ili na mimi niende nikawabane mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na mabalozi wote waliosoma hapa ili nao watoe michango yao na ikiwezekana kiwango kiwe ni hiki hiki (Sh5 milioni kila mwaka),” alisema Membe.
Baada ya kauli hiyo ya Membe, Waziri Mkuu Pinda aliahidi kuwabana mawaziri na manaibu wote ili kuweza kuchangia chuo hicho.
“Desemba saba nitakutana nao, nitawabana mpaka watoe michango yao... nyie wakuu wa wilaya na mikoa zamu yenu inakuja,” alisema Pinda.
Hata hivyo, alimtaka Profesa Mukandala kuweka mpango madhubuti wa kutafuta watu mbalimbali waliosoma kwenye chuo hicho ili watoe michango ya kumaliza matatizo yanayokikabili chuo hicho.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Saturday, 27 November 2010 08:27 Comments




+1 #7 Mlala hoi 2010-11-27 13:34 UDSM The best university TZ. Watoto wenye akiri; Siyo ma[NENO BAYA] kama UDOM. Bigup.
Quote









0 #6 mwakindole 2010-11-27 13:13 Mchango wake na watu anaotaka kuwachangisha pesa hazitoshi hata kidogo. Ningemwelewa kama angesema anakusudia kubana matumizi ya serikali ili hela hiyo itumike kwa ujenzi wa hostels. Mabilioni ya pesa yanahitajika kujenga hostels
Quote









0 #5 Laurent 2010-11-27 13:08 Hata bwana mhariri.

Maoni ni maoni, kwani mnahofia gazeti lenu kufungiwa?

Madamu yatakayoandikwa yataonekana ni maoni ya wasomaji wenu, hapana sababu ya kuogopa. Acheni kubana, toenei maoni bila woga
Quote









0 #4 Mushi Henry 2010-11-27 12:58 Haki inatafutwa wana UDSM Msilale Wanangu lazima viongozi wajue ni watumishi wa UMA na siyo Chama
Quote









0 #3 alex 2010-11-27 12:01 Watanzania tuwe jasiri kutatua matatizo yetu,tusiwangoj e watu toka nje!
Quote









0 #2 angel k 2010-11-27 11:26 hi inatuonesha wanachuo hawana ruksa ya kuonesha matatizo yao,'Hawa wanafunzi sijui walipenya vipi na hili bango'.
ukisikia demokrasia ya kihuni ndiyo hii.
Quote









+3 #1 elibariki Yerald 2010-11-27 08:55 HONGERA WANA UDSM UJUMBE UMEFIKA HATA KAMA MUKANDARA AMEBANA.HUU NDIO USALITI WA WASOMI WETU AMABO WANAKUBALI KUTUMIKISHWA NA WANASIASA UCHWARA.
"MAPINDUZI DAIMA" HUU NDIO UJUMBE WETU SIKU ZOTE MSICHOKE KUPIGANIA HAKI,
Quote







Refresh comments list

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!
Name (required)
E-mail

laugh.gif
lol.gif
smile.gif
wink.gif
cool.gif
normal.gif
whistling.gif
redface.gif
sad.gif
cry.gif
surprised.gif
confused.gif
sick.gif
shocked.gif
sleeping.gif
tongue.gif
rolleyes.gif
unsure.gif

7000 symbols left
Notify me of follow-up comments

index.php

Refresh


Send

Cancel







bot_tabimg01.gif


























© 2007 - 2010 Mwananchi. All Rights Reserved. A product of Mwananchi Communications Ltd.​


Created by Affordable Webdesign company
 
Pinda si Usalama wa Taifa?

Hii danganya toto ya kusema eti HAJUI kuwa watu wanalala nje ni kichekesho.

Wanafahamu kila kitu na wasijifanye eti Mtoto wa Mkulima hajui kitu.

Ukweli ni kuwa UDSM imezirwa na sasa ni midii ya kujenga Chuo chao cha CCM huko Dodoma aka UDOM.
 
Hivi hawa watu wa kujipendekeza kwa viongozi sijui tunawapata wapi? Hivi Prof Mukandala anashindwa kuheshimu elimu yake aliyonayo KULIKO aliyonayo MWANSIASA PINDA? Kwani kupeleka ujumbe kwa njia ya mabango inaathiri nini? Au alitaka tuanze kusifia kuwa vyumba vya kulala VIMEENEA?.

Kwa mtazamo wangu wanasiasa na viongozi kwa ujumla wanapaswa kujua UKWELI Mukandala..., SIO KUUFICHA!

Kwa tabia ya kuficha ukweli HUPASWI KABISA KUWAA KIONGOZI!!!!!!!!

Mukandala anashangaa jinsi bango lililoandikwa "MTOTO WA MKULIMA TUNALALA NJE" na wanachuo wa UDSM je ni kweli "eti leo mukandala kushangaa wanachuo wanalala nje ya campus UDSM"

Nini mawazo yako kwa viongozi kama hawa?

Prof. Mukandala ni bonge la kiongozi.

Ni moja wa wasaidizi wa Mkwere wenye moyo wa utu. Ana huruma sana.

Tatizo ni mabosi wake(including JK). Ni wala-rushwa.

Ndiyo maana kwenye ishu za REDET siyo mtu wa kupiga matarumbeta sana.

Amemuachia Benson Bana. Mwenye roho mbaya.
 
Hivi hawa watu wa kujipendekeza kwa viongozi sijui tunawapata wapi? Hivi Prof Mukandala anashindwa kuheshimu elimu yake aliyonayo KULIKO aliyonayo MWANSIASA PINDA? Kwani kupeleka ujumbe kwa njia ya mabango inaathiri nini? Au alitaka tuanze kusifia kuwa vyumba vya kulala VIMEENEA?.

Kwa mtazamo wangu wanasiasa na viongozi kwa ujumla wanapaswa kujua UKWELI Mukandala..., SIO KUUFICHA!

Kwa tabia ya kuficha ukweli HUPASWI KABISA KUWAA KIONGOZI!!!!!!!!

Mukandala anashangaa jinsi bango lililoandikwa "MTOTO WA MKULIMA TUNALALA NJE" na wanachuo wa UDSM je ni kweli "eti leo mukandala kushangaa wanachuo wanalala nje ya campus UDSM"

Nini mawazo yako kwa viongozi kama hawa?


Komedi Orijino
 
Back
Top Bottom