dr.malulu
Senior Member
- Jun 26, 2013
- 133
- 60
Tarehe mbili leo, Drama Mpya.
Nimemsikia Prof Muhongo akizungumzia mabadiliko ya bei ya Umeme. Amegusia mambo matatu muhimu.
1. Amesema TANESCO walikua na kawaida ya kujilipa bonus kila mwisho wa mwezi/mwaka. Akaongeza kuwa, mwaka jana alifanikiwa kuokoa mamilioni ya pesa yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya bonus (Mbona hakusema siku zote?)
2. Kuhusu madeni kulipwa kwa kuwapandishia bei wananchi, amesema haitawezekana tena TANESCO kulipa madeni kwa kutegemea bei kupanda. Serikali inafanya mpango wa kukopa pesa nje ya nchi ili kulipa madeni ya TANESCO ikiwemo IPTL (Baada ya kukopa nje nani atalipa hayo madeni?)
3. Amesema hakupata taarifa yoyote kuhusu kupanda kwa umeme, ameshitushwa na matangazo ya EWURA. Hakujua kinachoendelea, yaani toka September to December hakuwa na taarifa. Yaani mimi wa kijijini taarifa nilikuwa nayo kuwa TANESCO wamepeleka mapendekezo EWURA juu ya kupanda bei ya units ifikapo 2017 January halafu Waziri hakuwa na taarifa. Hii imenikumbusha mbali pesa za Escrow sio za umma. Huyu mzee namkubali sana ila akiamua kufanya drama ni zaidi ya Michael Jackson.
Naenda kazini