Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,356
- 21,390
CCM tuache kuzuga kusahau. Tuache kuzuga kusifu uamuzi wa Rais uliochelewa na kuuita wa uthubutu bila ya kuona soni ya historia. Tuache kuzuga kuwa kuweka sawa uchimbaji wa madini ni sera za CCM.
Kwa anachofanya sasa Rais,kila mpendanchi anakipongeza. Kila mpendanchi anamuunga mkono Rais katika kusafisha sekta ili nchi ifaidike. Nchi inatamani kubaki na maendeleo kupitia uchimbaji. Kwa uamuzi wa Rais,wapendanchi tupo pamoja naye na kumtia shime.
Uwazi na uhalali katika sekta ya madini imekuwa ajenda ya wapinzani miaka nenda rudi. Wapinzani,pamoja na kuwa wachache Bungeni,wameshupalia uwazi wa mikataba ya madini na namna nchi inavyofaidika. Wapinzani wa enzi hizo Bungeni wakiongozwa na Dr. Slaa walishikia bango suala hilo
Wapinzani walibezwa na kutwezwa.CCM ikatumia wingi wetu Bungeni kukejeli,kuponda bila kupenda na kuchanachana kwa laana hoja za haja za wapinzani kuhusu madini. Zitto akalipua Buzwagi. Akasakamwa nusu ya kuhama. Wabunge wa CCM wakasema kwa kuhema kutetea usiri wa mikataba ya madini
Leo,wanampongeza Rais bila soni. Lahaula! Inashangaza na kuduwaza. Kwanini wapinzani wasipongezwe? WanaCCM wenzangu,tunaposhabikia sasa kauli na uamuzi wa Rais na Mwenyekiti wetu,tuwe na soni na kiasi. Mwaka 1997,sheria kuhusu uwekezaji na madini zilipitishwa kwa Hati ya Dharura. Upesiupesi bila wasiwasi. Leo,zinatugharimu.Tunachekesha kujifanya tunafanya mema sasa kwa taifa.
Hakika,opposition deserves credits for what is happening now nchini. Aibu na lawama na iwe kwetu wanaCCM!
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea,Ruvuma)
Rafiki inaonyesha jinsi CCM ilivyojaza kizazi cha kusifia bila kuhoji.Kizazi cha Chuki na ubaguzi.Kizazicha kufikiria tumbo kwanza mengine baadaye.
Lakini cha kushangaza tuansikia yule aliyekuwa Mwanasheria nguli wa wizara hiyo ambaye ndiye Naibu waziri leo anapewa ufull Naibu,halafu wale akina wakurugenzi wametumbuliwa hii nayo naona ni Changa la Macho.Naona ni mahali tu Mwenyekiti anatafutia kick.
Au yawezekana na yeye anatafuta mahali pakupiga mirahaba yake kama wenyeviti waliopita,maana ndiyo ADA na HULKA ya Chama chetu kikongwe kabisa kisicho na haya aka CCM