Prof. Muhongo kutoka si suluhisho: Tatizo mikataba ikoje?

Ttz sio mtu now ttz n chama kilichomadarakan...hata aje malaika ila bila ccm kupata muda wa Kukaa bench hatutonyooka
 
Tatizo sio kupimwa akili..!! Tatizo ni uhalisia wa mikataba iliyopo kwenye madini..! Prof ulitaka aibadilishe yeye?
Mkuu hujaelewa saga zima la mchanga wa dhahabu kama ripoti ilivyoainisha leo. Prof. Muhongo hawajibishwi kwa sababu aliingia mikataba tata, bali kwa sababu alishindwa kusimamia au kuharakisha zoezi la ununuzi wa Smelter kama ilivyoagizwa tangu 2009.
Pili sababu nyingine kubwa ni kushindwa kufuatilia usahihi wa kinachojazwa ktk taarifa za usafirishaji mchanga, kazi hiyo ilitakiwa isimamiwe ipaswavyo na TMAA ambayo ilikuwa chini yake na alikubali vipi hoja ya kwamba hatuwezi kuweka smelter yetu kwa sababu hatuna makinia ya kutosha kuendana na gharama ya uendeshaji hiyo smelter wakati huo yeye ni Professor aliebobea ktk sekta hiyo.
Tatu kwa taaluma yake alipaswa kujua ukweli kwamba kuna madini mengine mengi yanayokuwamo ktk mchanga wa dhahabu zaidi ya yale waliyokuwa wana ainisha ktk nyaraka zao za kusafirishia mchanga.
ZINGATIA: Hawajibishwi sasa kwa sababu mikataba mibovu, kwani jambo hili ni la kisheria na tume inayohusika na kipengele hicho bado haijatoa ripoti yake ya uchunguzi. Tume hii maalum iliyokuwa chini ya Prof. Maruma haikuhusika na mambo ya kisheria au mikataba.
 
Duh! Mleta mada katumbuliwa mapema leo. Pole kwa kutumbuliwa ulipotea humu sasa naona umeamua kurudi tena maskani karibu sana.

Tatizo sio kupimwa akili..!! Tatizo ni uhalisia wa mikataba iliyopo kwenye madini..! Prof ulitaka aibadilishe yeye?
 
Na ameshapatikana ili kukwepa lawama.
Lakin cha ajabu.. hali itaendelea kuwa vile vile hata kama watamchagua malaika kutoka mbinguni
Hata aje binadamu mwenye akili kupita wote duniani kuongoza wizara ya Nishati na madini,haiwezi hata kidogo.ivi kwa mfano mm nauliza baada ya kutumbua hao waheshimiwa tutaweza kujinunulia izo mashine za kuchakata na kuchambua madini?ni ghali na zitatumia umeme mwingi hatuweziiiiiiiii.tunawaumbua hao wazungu,accacia na wengine but mwisho wa siku tunaenda kwao kuomba misaada.yaan sisi bado nchi changa tunawategemea hao hao wazungu kwa karibu kila kitu so ilibidi tuwe wapole tupunguze jeuri
 
Ukweli ni kwamba viongozi wa CCM waliokuwa wamepewa dhamana ya kuongoza nchi hii kwa miaka mingi pamoja na wabuge wa CCM ambao wamekuwa wakipitisha sheria za hovyo hovyo kwa mtindo wa ndioooo wote wanastahili kuwajibika na watendaji waliohusika wanastahili kwenda jela na si kupewa nafasi ya kujirekebisha kama wanavyotaka kutuhadaa sasa.

Inakera na kuudhi sana kuona watu walioshiriki katika hizi serikali eti mambo haya hawakuyaona ila leo hii ndio wanashituka na wanataka tuwaunge mkono wao na chama chao.Kiukweli waliohusika wote walipaswa kuwa jela na si kupewa nafasi ya kujirekebisha vinginevyo hata wafungwa wote walioko magerezani nao waachiwe wajirekebishe wakiwa uraiani.

Jambo baya kabisa na la kusikitisha ni wapinzani waliokuwa wakipinga upitishiwaji wa sheria hizi za hovyo hovyo Bungeni walivyokuwa wakipuuzwa na watu ambao leo hii eti wamegeuka wema.Huu kwakweli ni unafiki wa kiwango cha juu sana.

Kwa mfano,hata Mbowe Alhamisi iliyopita alimuuliza Waziri Mkuu Bungeni juu ya utekelezaji wa maazimio mbambali ya Bunge yaliyowasilishwa serikali lakini majibu
aliopewa hayaridhishi kabisa alafu eti ndio niamimi wamepatikana watu wa kukomboa Taifa hili.

Hata leo hii kuna maamuzi yanafanywa bila hata Bunge kushirikishwa alafu kesho mambo yakiharibika atoke mwingine ajidae kusafisha nae tumpigie makofi.Sijui yumelogwa!!

Miswaada hii inapita kwenye cabinet wanakaa wanaijadili na kisha wanaileta Bungeni na huko wanajadili na kuitetea kwa kila hali kuhakikisha inapitishwa na baadae Raisi kuisaini na kuwa sheria.

Sheria zikishapitishwa na kuanza kutumika ndipo matatizo yanaanza kujitokeza na wapinzani wanaendelea kuhoji mapungufu ya sheria hizo Bungeni na nje ya Bunge lakini wanapuuzwa.

Leo hii tunavuna tulichopanda na baada ya madhara ya muda mrefu,watu wale wale kutoka chama kile kile ndio sasa wanashituka na kutaka tuwaunge mkono.This is joke!

Kwa kifupi CCM haiwezi kukwepa lawama katika yote haya na waliohisika wote wanastahili kuwa jela na si kupewa nafasi ya kujirekebisha wakiwa uraiani.

Hawa watu wangekuwa waungwana kwanza wangetuomba radhi watanzania wote kabla ya kutaka tuwaunge mkono.

Cha ajabu katika hali hii watu hawa wanatuambia Mahakama ya Mafisadi imekosa watu.Kweli!!

Nimalizie kwa kusema tangu nianze kupiga kura hiki chama sijawahi hata kuchagua diwani wake na kamwe sitofanya hivyo.
 
Mikataba mibovu imetoka mbali sana!!
image.png
 
HONGERA SANA M/KITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Na Peter Dafi

Ni Tangu mwaka 1894 wakoloni waligundua Kuwapo kwa Dhahabu pembezoni mwa Ziwa Victoria, Walichukua madini kwa Kudanganya Wazee wetu na Mgodi wa Dhahabu wakwanza uliitwa SEKENKE MINE Mwaka 1909, Wazungu waliendelea kuchukua madini kama yao kwa umasikini na Ujinga wetu watanzania!
Mwaka 1990 makampuni Rasmi yakigeni yaliingia Nchini nakuanza utafiti wa madini.
Kampuni ya SAMAX ilikuwa yakwanza kupata Mkatapa kufanya Utafiti wa kuchimba nakuchukua Sampuli nakusafirisha Nje ya Nchi, Nakumbuka Ndege zilikuwa zinatua Uwanja wa Ndege wa Nzega Mjini kwa wiki zaidi ya mara 2-3wakibeba vibox vilivyojaa mchanga, wana safirisha nje ya Nchi wakidai Wanapeleka Kupima Nje ya Nchi tena Australia.
Kampuni ya SAMAX ilifanya hivo lakini baadae iliingia ubia na BHP mwaka 1998 na Kisha Baadae Mgodi ulifungukiwa kwa USD $ 48 Million ilikuwa ni Tarahe 7 February 1999.
Kipindi hicho Mimi ni Mdogo nasoma Shule ya Msingi.
Na Nakumbuka Mgodi wa Kwanza Ulikuwa Nzega Sehemu inayoitwa Lusu.
Tangu Kipindi Hicho wawekezaji Sijawai Sikia Wanafaidika na Madini ya Nchi yetu, na Wanaendelea kuchimba nakuongeza Ulinzi na Usiri Mkubwa wa Kazi zao, Leo Kila Mgodi una uwanja wa ndege Huko huko ndani, Ili Ndege itue Ibebe Madini Halisi nakuondokea huko huko.

Mh Rais Nasema Hongera sana kwa Jitihada hizi unazoendelea nazo, Hawa Wawekezaji wa Migodi Waliahidi Kusaidia Jamii husika zinazozunguka Migodi yao laki hakuna Kilichofanyika na kikalingana na Mali wanazochukua.
Kampuni ya RESOLUTE iliyokuwa ikichimba Nzega Mpaka Leo Tunaidai Na Hawana Mpango wakulipa Pesa zetu kwa Serikali, Inauma sana.

Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa nakuomba Endelea Kutusaidia nakupambana kuhakikisha Nchi yetu inasonga mbele.

Makondeta yamesafiri Tangu Miaka ya 2000+ mpaka leo Ni Pesa Nyingi sana Zimepotea.
Nimeishi Nzega Nimeona Mgodi Ukianza mpaka Umefungwa tumeachiwa Mashimo na Hakuna La Maana Lililoachwa kwa wana Nzega kama Kumbukumbu, Lakini Enzi za miaka 1980 Migodi Midogo midogo ya Lusu, Isunga, nk.. Ilinufaisha Wanachi wa Maeneo husika zaidi ya Leo hii.
Manake leo pesa Nyingi inatoka na Madini mengi yanatoka nakuisha kabisa na hakuna Tunachokipata kulingana na Mali Inayondoka.

Leo Hii Mgodi wa Buzwagi chini ya ACACIA wanatarajia kuufunga Mgodi wakiwa washamaliza Madini tunaachiwa Shimo na Matangazo yauwongo na ukweli katika TV, Radio na Magazeti yakwamba eti wametusaidia Sana vijijini laa hashaa Tunaliwaaa..!

Mh Rais nasema Mungu akubariki sana na azidi kukupa Maono, Hekima na Busara uzidi kulitumikia Taifa hili, kwani Maisha ya Watanzania yalitamani kupata Rais kama wewe ili Utusaidie tunaoishi leo na Vizazi vijavyo.

Kwa Jitihada hizi Nikupongeze sana Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kwani Ilani ya CCM 2015 imesema itasimamia nakuboresha Mikataba ya hovyo lakini kuhakikisha inapitia Mifumo ambayo ilinyonya Taifa letu.
Hongera sana na Vijana wa CCM tuko Imara kulitumikia Taifa na Chama kwa ujumla.

Mwisho Niseme, Mh Rais Tengua na Vunja Mikataba ya Hawa Wawekezaji Waongo, Wizi na Majambazi ambao wametuibia kwa Muda Mrefu huku wakijifanya wema sana kuwa wao wanakula hasara sana.

Nimeona Kampuni Moja Kubwa sana Nchini Eti nayo inashangaa juu ya Taarifa hii ya Jana, jamani Hawa Watanzania walioajiliwa Ndani ya Migodi Hii Nao wamekuwa Sio Watanzania wazalendo kisa Mishahara minono nao wanasahau Utaifa wetu.

Mh Rais Vunja Mikataba na Vijana Wasomi wa Sheria Watakusaidia Kutetea Hoja za Kisheria ili Kuboresha Mikataba hii.

Nibora Tugaramike Kununua Wanasheria Wabobezi Lakini Tuinusuru Nchi Hii dhidi ya Upotevu wa Rasilimali hizi tunazopoteza ambazo Zingesaidia Taifa hili.

Watanzania Tuungane kama Taifa Kumsaidia Mh Rais kwa Hali na Mali Kupambana katika Vita Hii ya Uchumi.

Ni Mimi Katibu wa UVCCM Chamwino.
Ndg. Peter. L . Dafi
 
Safi Nimeshangaa Wimbi la Vijana Wa UKAWA tulivyokua Tunasifia Wote Usiku wamepewa pesa na ACACIA Sasa Hivi Wanawatetea ACACIA.
 
rais afahamu akipelekwa katika international court kwa kuingilia mkataba litakua janga kuu.

tazama wale samaki waliokamatwa tukagaiwa what happened.

kampuni Za wazungu zinajali sana mikataba, kuvunja au kutotekeleza mkataba Na pia kudestroy brand ionekane km wanaiba ilihali wameingia mkataba Na kutekeleza huo mikataba we r going to pay.

issue nikuwafikisha mahakamani walioiingia hiyo mikataba Na sio kumfanya victim aliepewa mikataba.

ni muda tu, let us wait.
 
Ukweli ni kwamba viongozi wa CCM waliokuwa wamepewa dhamana ya kuongoza nchi hii kwa miaka mingi pamoja na wabuge wa CCM ambao wamekuwa wakipitisha sheria za hovyo hovyo kwa mtindo wa ndioooo wote wanastahili kuwajibika na watendaji waliohusika wanastahili kwenda jela na si kupewa nafasi ya kujirekebisha kama wanavyotaka kutuhadaa sasa.

Inakera na kuudhi sana kuona watu walioshiriki katika hizi serikali eti mambo haya hawakuyaona ila leo hii ndio wanashituka na wanataka tuwaunge mkono wao na chama chao.Kiukweli waliohusika wote walipaswa kuwa jela na si kupewa nafasi ya kujirekebisha vinginevyo hata wafungwa wote walioko magerezani nao waachiwe wajirekebishe wakiwa uraiani.

Jambo baya kabisa na la kusikitisha ni wapinzani waliokuwa wakipinga upitishiwaji wa sheria hizi za hovyo hovyo Bungeni walivyokuwa wakipuuzwa na watu ambao leo hii eti wamegeuka wema.Huu kwakweli ni unafiki wa kiwango cha juu sana.

Kwa mfano,hata Mbowe Alhamisi iliyopita alimuuliza Waziri Mkuu Bungeni juu ya utekelezaji wa maazimio mbambali ya Bunge yaliyowasilishwa serikali lakini majibu
aliopewa hayaridhishi kabisa alafu eti ndio niamimi wamepatikana watu wa kukomboa Taifa hili.

Hata leo hii kuna maamuzi yanafanywa bila hata Bunge kushirikishwa alafu kesho mambo yakiharibika atoke mwingine ajidae kusafisha nae tumpigie makofi.Sijui yumelogwa!!

Miswaada hii inapita kwenye cabinet wanakaa wanaijadili na kisha wanaileta Bungeni na huko wanajadili na kuitetea kwa kila hali kuhakikisha inapitishwa na baadae Raisi kuisaini na kuwa sheria.

Sheria zikishapitishwa na kuanza kutumika ndipo matatizo yanaanza kujitokeza na wapinzani wanaendelea kuhoji mapungufu ya sheria hizo Bungeni na nje ya Bunge lakini wanapuuzwa.

Leo hii tunavuna tulichopanda na baada ya madhara ya muda mrefu,watu wale wale kutoka chama kile kile ndio sasa wanashituka na kutaka tuwaunge mkono.This is joke!

Kwa kifupi CCM haiwezi kukwepa lawama katika yote haya na waliohisika wote wanastahili kuwa jela na si kupewa nafasi ya kujirekebisha wakiwa uraiani.

Hawa watu wangekuwa waungwana kwanza wangetuomba radhi watanzania wote kabla ya kutaka tuwaunge mkono.

Cha ajabu katika hali hii watu hawa wanatuambia Mahakama ya Mafisadi imekosa watu.Kweli!!

Nimalizie kwa kusema tangu nianze kupiga kura hiki chama sijawahi hata kuchagua diwani wake na kamwe sitofanya hivyo.
Mbaya zaidi kocha wa sasa alikuwa mchezaji pia
 
rais afahamu akipelekwa katika international court kwa kuingilia mkataba litakua janga kuu.

tazama wale samaki waliokamatwa tukagaiwa what happened.

kampuni Za wazungu zinajali sana mikataba, kuvunja au kutotekeleza mkataba Na pia kudestroy brand ionekane km wanaiba ilihali wameingia mkataba Na kutekeleza huo mikataba we r going to pay.

issue nikuwafikisha mahakamani walioiingia hiyo mikataba Na sio kumfanya victim aliepewa mikataba.

ni muda tu, let us wait.
Au tuvunje mikataba tulipe tu...
 
Back
Top Bottom