Prof. Muhongo kajiuzulu Uwaziri, vipi Ubunge wa kuteuliwa?

Kaduguda

JF-Expert Member
Aug 1, 2008
724
641
Wadau ninajiuliza hapa sipati majibu, Prof. Muhongo aliteuliwa mahsusi kwa ajili ya kupewa huo uwaziri, na nakumbuka hata kuanza kazi alianza hata kabla ya kuapishwa kitu ambacho baadhi ya wanasheria walikuwa wanapingana nacho. Sasa ndio hivyo, kajiuzulu huo uwaziri, suala la ubunge linakuwaje hapo? Au ndio ataendelea kuvuta posho mpaka hatima ya hili Bunge letu?

Ufafanuzi tu wadau!
 
Ataendelea kuwa mbunge wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Mbatia. Kimsingi alitakiwa ajiuzuru hata ubunge, lakini kama ujuavyo nchi za Kiafrica
 
Ni vitu vwili tofauti. Mbona mbatia bado yumo
 
Mkuu,

Kwanza nianze kwa kusema, swali /hoja yako inamfanya msomaji anadhani ina hoja nyuma yake ambayo imejificha kwa sababu kama unafuatilia siasa au somo la civics utakuwa unaelewa aina ya wabunge na maisha yao ya ubunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

Kwa kukusaidia, Rais amepewa mamlaka kikatiba ya kumteuwa Mtanzania yoyote ambaye anakidhi masharti ya ubunge lakini asimpe uwaziri kama ilivyofanyika kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Prof. Muhongo ataendelea kuwa Mbunge mpaka pale bunge litakapovunjwa na Rais.

Hii ndiyo aina ya wabunge wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya 1977

66.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;

(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais, watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya
78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;

(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;

(d) Mwanasheria Mkuu;

(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b)
 
Wadau ninajiuliza hapa sipati majibu, Prof. Muhongo aliteuliwa mahsusi kwa ajili ya kupewa huo uwaziri, na nakumbuka hata kuanza kazi alianza hata kabla ya kuapishwa kitu ambacho baadhi ya wanasheria walikuwa wanapingana nacho. Sasa ndio hivyo, kajiuzulu huo uwaziri, suala la ubunge linakuwaje hapo? Au ndio ataendelea kuvuta posho mpaka hatima ya hili Bunge letu?

Ufafanuzi tu wadau!

ubunge wake unabaki palepale, kwani Mbatia ni waziri??
 
Ila kwa jinsi alivyo na dharau,sidhani kama atakua anahudhuria bungeni.halafu si nasikia kapata kazi UN?
 
Ataendelea kuwa mbunge wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Mbatia. Kimsingi alitakiwa ajiuzuru hata ubunge, lakini kama ujuavyo nchi za Kiafrica
Hivi Edward Lowasa alivyojiuzulu uwaziri mkuu alijiuzulu na ubunge vile? Pia tuna akina Shamsi Nahodha, Emannuel Nchimbi, Hamisi Kagasheki, William Ngeleja, Anna Tibaijuka, Nk ambao wameachia ngazi uwaziri ila wanaendelea kuwa mbunge. Kwa nini kwa Prof Muhongo?
 
Mkuu,

Kwanza nianze kwa kusema, swali /hoja yako inamfanya msomaji anadhani ina hoja nyuma yake ambayo imejificha kwa sababu kama unafuatilia siasa au somo la civics utakuwa unaelewa aina ya wabunge na maisha yao ya ubunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

Kwa kukusaidia, Rais amepewa mamlaka kikatiba ya kumteuwa Mtanzania yoyote ambaye anakidhi masharti ya ubunge lakini asimpe uwaziri kama ilivyofanyika kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Prof. Muhongo ataendelea kuwa Mbunge mpaka pale bunge litakapovunjwa na Rais.

Hii ndiyo aina ya wabunge wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya 1977

Asante sana Ng'wamapalala kwa ufafanuzi wako. Kwa nini nimeuliza hiki swali, ukirejea uteuzi wake ni kama ulikuwa wa special mission, Nidhati na Madini. Kumbuka pia aliombwa kuja hakutaka yeye binafsi. Alikuwa na kazi yake nzuri tu kabla ya kuitwa. Sasa mission ime-abort, hivi unadhani hata huo ubunge atautumikia kwa moyo? Maana kwanza aligoma kujiuzuru sasa yametimia, kuna maana gani ya kuwa nae bungeni?
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa Prof Makini Muhongo angepiga chini kila kitu, lakn vile na njaa imo hawezi piga chini ubunge ile hali pia aliteuliwa na rais, katiba ingesema huyu kwa case yake inapaswa ubunge pia aachie ili kumpa fursa rais iwapo anamtu nje amuingize ndani ya bunge kisha uwaziri, sasa anaziba nafasi za rais bila tija
 
Ataendelea kuwa mbunge wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Mbatia. Kimsingi alitakiwa ajiuzuru hata ubunge, lakini kama ujuavyo nchi za Kiafrica
Hakutakiwa kujiuzulu alitakiwa kuwajibishwa(kufutwa kazi) then mahakamani
 
Asante sana Ng'wamapalala kwa ufafanuzi wako. Kwa nini nimeuliza hiki swali, ukirejea uteuzi wake ni kama ulikuwa wa special mission, Nidhati na Madini. Kumbuka pia aliombwa kuja hakutaka yeye binafsi. Alikuwa na kazi yake nzuri tu kabla ya kuitwa. Sasa mission ime-abort, hivi unadhani hata huo ubunge atautumikia kwa moyo? Maana kwanza aligoma kujiuzuru sasa yametimia, kuna maana gani ya kuwa nae bungeni?
Ni mwanasheria Mkuu wa Serikali pekee ambaye anateuliwa na Rais lakini akipigwa chini au kujiudhuru uanasheria Mkuu wa serikali hata bungeni hawezi tena kuingia.

Ndiyo maana Rais hahitaji kumteua kwanza kuwa mbunge ili baadaye amteuwe kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Prof.Muhongo analazimika kuingia Bungeni kwa mujibu wa Katiba na kama atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika basi hata ubunge wake utakoma.
 
Wadau ninajiuliza hapa sipati majibu, Prof. Muhongo aliteuliwa mahsusi kwa ajili ya kupewa huo uwaziri, na nakumbuka hata kuanza kazi alianza hata kabla ya kuapishwa kitu ambacho baadhi ya wanasheria walikuwa wanapingana nacho. Sasa ndio hivyo, kajiuzulu huo uwaziri, suala la ubunge linakuwaje hapo? Au ndio ataendelea kuvuta posho mpaka hatima ya hili Bunge letu?

Ufafanuzi tu wadau!

= kajiudhuru
 
Asante sana Ng'wamapalala kwa ufafanuzi wako. Kwa nini nimeuliza hiki swali, ukirejea uteuzi wake ni kama ulikuwa wa special mission, Nidhati na Madini. Kumbuka pia aliombwa kuja hakutaka yeye binafsi. Alikuwa na kazi yake nzuri tu kabla ya kuitwa. Sasa mission ime-abort, hivi unadhani hata huo ubunge atautumikia kwa moyo? Maana kwanza aligoma kujiuzuru sasa yametimia, kuna maana gani ya kuwa nae bungeni?

Ukirejea aina za wabunge kama alivyonukuu Kaduguda kwenye post yake hapo juu toka katika katiba ya JMT unaweza kuona kuwa maana ya mbunge wa kuteuliwa inaweza kupimwa na aliyemteuwa kama anakidhi au la! Sisi tuna hadidu za rejea na wale tuliyowapigia kura kama wanapwaya then tunahitaji kula sahani moja nao. Na hapo ndipo wananchi walipokuwa wamependekeza kwa Warioba kuwang'oa hata kabla ya kumaliza miaka mitano. Wamejivisha uungu mtu eti majimbo wanayaita jimbo langu wakati wakishachaguliwa wanaishia kinondoni na vichochoro vingine vya Dar huku Makongolosi wanakuja mwakwa wa nne na kuanza kupiga piga porojo mshenzi na kuhudhuria misiba.

Lakini hawa wa kuteuliwa mmmh anayemlipa mpiga zomali ndo anachagua wimbo bhana. Huu ni miongoni mwa udhaifu wa katiba tuliyonayo. Mkuu wa kaya katwishwa vitu viiingi vya kuteua na kuapisha na hawezi kuhojiwa maana ni sheria mama inayompaka hayo mamlaka/madaraka
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom