Prof. Muhongo bora ungeendelea kuwa mchimbaji kwa mzee Madiba

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
3,792
2,000
Hii ripoti ya professor mwenzako imekuondolea heshima yako uliyojijengea kwa gharama kubwa toka utotoni ukizingatia ulikua na hamu ya mafanikio ikapelekea kuamua kurudia darasa la saba Mara tatu.

Na mungu akakusikia akakupa ulichotaka kwa sababu hukukata tamaa na wala hukuona aibu kujiunga na wadogo zako ambao ukiwa darasa la saba wao walikua darasa la tatu.

Ulikubali kuwasubiri hadi ukamaliza nao std 7 na hicho ndisho hata Mungu akaona aibu akaamua kukuvusha kwa kuona juhudi zako za kutaka mafanikio, kwa kuwa ulipenda Elimu ukaamua kujenga familiar iliyoelimika kama wewe.

Sijui nani alikuroga ukakubali kuchukua taaluma yako ambayo kwa maoni yako hapa Tanzania ni wewe tu ndiye mwenye Elimu aina yako ukaingia kwenye siasa sasa unadhalilika bila sababu.

Nikikumbuka kipindi unataka urais kati ya wana CCM ukiondoa bwana Mwigulu ni wewe ndiye ulikua unatoa hoja ambayo iliweza kunikuna na ku ahidi kimoyomoyo kukuunga mkono kwa sababu nilikuona mwadilifu mwenye maono ya kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati kupitia gesi peke yake.

Uliitumia taaluma yako kuchambua gesi tuliyonayo na utafiti ambao ulishafanya na kukuta kuwa hadi 2020 tayari umaskini wa nchi ungepungua kwa %6O kutokana gesi, na nilipenda uliposema kuwa wewe hutakubali kuambiwa Bali utaingia field mwenyewe na hakuna atakaekudanganya bila fact ambayo utaithibitisha kwanza ndipo uikubali.

Juzi wakati unatajwa nikajiuliza ni wewe mzee wa fact hau nani? Kwa kweli umeniangusha sana, sikutegemea kama unaweza kuangushwa kirahisi kama embe lililoiva.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom