Prof. Muhongo atua Dar, aeleza sababu za kupata mradi wa bomba la mafuta

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo ametua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kuelezea jinsi mapambano yalivyokuwa makali katika kuhakikisha Tanzania inapata mradi wa kusafirisha mafuta kutoka Uganda.

Muhongo amemsifu Rais Magufuli kwa kufanikisha juhudi zilizopelekea kupata mradi ambapo amesema utawanufaisha watanzania na taifa.

Muhongo amesema kazi ya Rais Magufuli ya kusimamia ujenzi wa barabara nchini wakati akiwa Waziri wa Ujenzi imechangia kwa kiasi kikubwa kuwashinda Wakenya katika mpambano ambapo vifaa vya ujenzi wa bomba vitaweza kusafirishwa kwa urahisi na gharama ndogo nchini ukilinganisha kama mradi wangepewa Wakenya.

''Tanzania tuna barabara nzuri, tuna reli na pia tuna bandari ambazo kwa pamoja zinafanya gharama ya ujenzi wa mradi kuwa ndogo ukilinganisha na Kenya'' Alisema Muhongo.

Muhongo amesema, hata kwenye suala la usalama, Tanzania tunaongoza kwa uwepo wa usalama ikilinganishwa na Kenya.

Hata kwenye uzoefu wa mabomba tunaongoza ikilinganishwa na Kenya kwa sababu tuna mabomba kama TAZAMA, Songosongo, Mtwara-Mnazibay na Mtwara/Dar es Salaam.

VIDEO



20160424080013.jpg
 
Back
Top Bottom